Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, March 12, 2010


Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda (Kushoto) akiongea na Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mh. Joseph Mungai katika viwanja vya Bunge, Dodoma .

Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda anatarajiwa kuitembelea Japani kuanzia Jumatano ijayo th.24/3/2010 mpaka th.27/3/2010. Pamoja na kukutana na Viongozi wa Juu wa Serikali ya Japani pia anatarajiwa kukutana na Watanzania wanaoishi hapa siku ya Ijumaa tarehe 26/3/2010. Kwa mujibu wa taarifa Kutoka kwa uongozi wa Jumuia ya Watanzania wanaoishi Japani -TANZANITE , Mkutano huo utafanyika katika Hotel ya New Otani iliopo jijini Tokyo wakati wa jioni.

Posted by BM. on Friday, March 12, 2010


Picha aliyopiga Mh. JK , ikiingia kwenye mnada inalipa...Nadanganya? (Na Mo Blog)

Posted by BM. on Friday, March 12, 2010

Vijana Jazz ya sasa! Baby white , Mgonahazelu na Shomari ally soloist tangu ...mpaka!
Toleo Jipya la Enzi hizo...Kama wa wakati huo unakumbuka?

Posted by BM. on Friday, March 12, 2010


Mkono wa Presda...(Nani?)
Bibi wa Obama Sarah" We Baraka mzima!, acha masihara yako".

Posted by BM. on Friday, March 12, 2010



Raisi wa Sierra Leonne Ernest Baikoroma, Mwenyeji Kaimu Raisi wa Nigeria Dr. Goodluck Jonathan , Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda wakisikiliza wimbo wa taifa wa Nigeria ukipigwa mwanzoni wa Mkutano wa biashara na usindikaji vyakula uliofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Transcorp nchini Nigeria.

Waziri wa Viwanda na Masoko Dr. Mary Nagu , Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Naibu waziri wa mambo ya Nje Balozi Iddi seif wakitoka nje ya ukumbi baada ya kumalizika kwa Mkutano huo.

Posted by BM. on Friday, March 12, 2010


Mwanaume wa nchini Marekani ambaye alitoboa tundu kwenye ukuta wa bafu lake na kuchukua video kwa siri wakati mkewe akioga amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja.
Richard Perez mkazi wa Minnesota nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kurekodi video kwa siri wakati mkewe akioga.Mahakama iliambiwa kuwa Perez alitoboa tundu kwenye ukuta wa bafu lake na kisha kutegesha video kamera ambayo aliitumia kurekodi video za siri wakati mkewe alipokuwa uchi akioga.
Mkewe ambaye alitajwa kwa kifupi kama KP, aliwaita polisi baada ya kukuta video zake akioga kwenye kompyuta iliyopo nyumbani kwao.Wapenzi hao walikuwa kwenye taratibu za kuivunja ndoa yao wakati video hizo zilipogundulika.Polisi walizikuta video nne za KP akivua nguo zake na kuingia kwenye bafu kuoga. Pia polisi walifanikiwa kuzipata video kadhaa zilizopigwa na Perez kwenye maeneo ya hadhara ambapo alichukua video za wanawake chini ya sketi zao.Perez alipatikana na hatia januari mwaka jana kutokana na makosa ya kuchukua video ya mke wake akiwa mtupu akioga bila ya yeye mwenyewe kujua."Mke anaweza akawa na masuala binafsi anapokuwa peke yake bafuni na hiyo haimaanishi kuwa kwasababu ya ndoa haki zake za masuala binafsi ndio zipotee", alisema jaji wa kesi hiyo wakati akimhukumu Perez kwenda jela mwaka mmoja.Perez alikata rufaa lakini juzi mahakama ilitupilia mbali rufaa yake kumuamuru aende jela akatumikie kifungo chake cha mwaka mmoja.



Source: News Agencies

Posted by BM. on Thursday, March 11, 2010

Bofya hapo upate kisa na ushauri wa Msondo Ngoma....

Posted by BM. on Saturday, March 06, 2010


Mahakama ya jiji la Nagoya hapa Japani imempiga faini dereva wa lori na kampuni yake ya usafirishaji Yeni 2.9 Millioni sawa na takriban Shillingi za kitanzania Millioni 42 kwa kumgonga kwa gari lake mbwa ambaye aliyekuwa akitumika kuongozea watu barabarani hasa kwa watu wasioona.Shirika linalommiliki mbwa huyo ya Chubu Modekan Kyokai ilifungua kesi mahakamani dhidi ya dereva huyo na kampuni yake akidai alipwe Yeni Millioni 6 sawa na fedha za Kitanzania Millioni 87 kwa kifo hicho cha mbwa akidai ametumia gharama kubwa kumfundisha hadi kufikia hapo.
Jaji Atsuko Matsuda alisema kuwa "Mbwa kiongozi wana thamani kubwa na kwamba gharama za kumfundisha hazina budi kuzingatiwa." Japani wakali , hebu fikiria ingelikuwa binaadamu ingekuwaje hapo.

Posted by BM. on Saturday, March 06, 2010

Mjukuu wa Mfalme wa JAPANI Mwana wa mwana wa Mfalme Princess Aiko ameshindwa kwenda shule kutokana na kile kilchosemwa kuwa ni kusumbuliwa na wavulana.

Binti huyo pekee wa mwana wa Mfalme Crown Prince Naruhito na Mkewe Princess Masako, amekuwa hafurahii kwenda shule tangu Jumatatu wiki hii baada ya "kusumbuliwa" na wavulana wa darasa lake na taarifa hizo kutolewa na Wahudumu rasmi wa makazi ya mfalme.Binti huyo mwenye miaka 8 inasemekana amekuwa akichokozwa na wanafunzi wenzake.Inaelezwa kuwa anasoma katika shule ya msingi Gakushuin eneo la Shinjuku na siku ya kwanza baada ya kupata mkasa huo alionekana kutahayari na kulalamikia maumivu ya kichwa , jambo alilolizungumzia Mhudumu mkuu wa Kasri ya kifalme katika Mkutano wa kawaida na waandishi wa habari.
Mwana wa mfalme Prince Naruhito na mkewe Princess Masako wazazi wa Princess Aiko.
Princess Aiko alikuwa haonekani shule tangu mwishoni mwa mwezi Februari akisumbuliwa na homa na jumanne aliondoka mapema shuleni na hajaonekana tena. Tayari Uongozi wa shule umepewa maagizo kushughulikia suala hilo.Katika Mkutano mwingine na waandishi wa habari Mkurugenzi wa shule hiyo ya msingi Gakushuin Motomasa Higashisono amesema kuwa hana taarifa juu ya kuwepo kwa usumbufu huo.Usumbufu unaotajwa ni pamoja na kupiga kelele kwa watoto, kuusha mabegi, kukimbia kwa kishindo kwenye makorido jambo ambalo Princess Aiko halipendi.
Shule hiyo imekuwa ikitumika na wanafamilia wa kifalme kujiendeleza kimasomo ikiwa ni pamoja na Mfalme mwenyewe Akihito na mkewe Naruhito kama wanavyoonekana katika picha hapo chini..
Suala hilo si dogo limemfikia Waziri Mkuu wa Japani naye amekaririwa akisema kuwa "Aiko kama raia wa kawaida wa Japani ,ninatumaini atapata nafuu na kurudi katika hali yake mapema iwezekanavyo".Nchini Japani Mfalme ni alama ta nchi. Hakuna jambo dogo katika familia ya kifalme. (Habari ; Mainichi Japan)

Posted by BM. on Saturday, March 06, 2010

Msichana Linda Ogutu mkazi wa jijini Nairobi, majuzi alijikuta yuko mikononi mwa Polisi baada ya kuhusika na vitendo kadhaa vya kuiba vitu kwenye magari. Amekuwa mkweli mbele ya wanahabari juu ya uhalifu wake huo anaofanya na wenzake lakini kubwa amesema ni kupata pesa za kujikimu na kupata kete za madawa ya kulevya.

Najaribu kupata picha; binti huyu angechukua mkondo mwingine wa maisha pengine angekuwa mbali sana badala ya kuchukua njia hii ya mkato...wewe je unasemaje!

Posted by BM. on Saturday, March 06, 2010

Jacob Zuma and his wife Thobeka Madiba Zuma arrive at London's Heathrow airport at the start of his state visit. Photograph: Ben Stansall/AFP/Getty Images

South Africa's president, Jacob Zuma, has lashed out at British attitudes to "barbaric" Africans as he begins a state visit in London.The remarks came after scathing British media coverage of the polygamous president and his chequered past, including the recent scandal of his 20th child, born out of wedlock. A Daily Mail article described him as a "sex-obsessed bigot" and "vile buffoon".Zuma, due to meet the Queen and Gordon Brown today, countered with an attack on what he described as culturally superior views reminiscent of the British empire in South Africa."When the British came to our country, they said everything we are doing was barbaric, was wrong, inferior in whatever way," he told South Africa's Star newspaper."Bear in mind that I'm a freedom fighter and I fought to free myself, also for my culture to be respected. And I don't know why they are continuing thinking that their culture is more superior than others, those who might have said so.
I am very clear on these issues, I've not looked down upon any culture of anyone, and no one has been given an authority to judge others."The British have done that before, as they colonised us, and they continue to do this, and it's an unfortunate thing. If people want an engagement, I'm sure we will engage on that issue." Zuma's statement was condemned by South Africa's main opposition party, the Democratic Alliance, as insulting to his hosts. Kenneth Mubu, the party's shadow international relations minister, said: "The treatment of President Jacob Zuma at the hands of a certain portion of the British press – most notably the Daily Mail and Daily Mirror – does not excuse his quite extraordinary attack on Britain and the British people."
He added: "Instead of rising above predictable criticism from a particular quarter of the British press, he has allowed himself to be dragged down to the level of the tabloids. "By accusing the British people of believing that Africans are barbaric and inferior, he has insulted his hosts, and no doubt undermined the entire purpose of the state visit – which is to strengthen relations between South Africa and the United Kingdom." Zuma was backed, however, by the youth wing of his party, the African National Congress. It issued a statement saying it was disgusted by the British reports. "British media seem to have developed a habit of rubbishing our president and constantly portray him as barbaric and of inferior belonging," the youth league said. "It is quite apparent that the British media is the one that is characterised and defined by the worst form of barbarism, backwardness and racism.
"These British racists continue to live in a dreamland and sadly believe that Africans are still their colonial subjects, with no values and principles. They believe that the only acceptable values and principles in the world are British values of whiteness and subjugation of Africans." Zuma, on a three-day visit, will press the British government for international sanctions on Zimbabwe to be lifted. He is accompanied by the newest of his three wives, Thobeka Madiba Zuma, on her first trip abroad. Protocol on which wife attends which state event is unclear and Zuma operates an unofficial "rotation" between spouses.
Una maoni gani hapo!
Unaweza kusikia maelezo yake kwa undani katika masuala mengine pia kwa kusikiliza mahojiano na Mwandishi wa CNN Amanpour.

Kp.

Posted by BM. on Friday, March 05, 2010


Maswaalii!.

Posted by BM. on Friday, March 05, 2010


Umeelewa ; hapo ni HongKong; Thanks Wilna.

Posted by BM. on Friday, March 05, 2010


Du Anko Bahati nitapenda niione hiyo picha , bila shaka itakuwa bomba tu!

Posted by BM. on Friday, March 05, 2010



Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe aliyezaliwa tarehe 21 Februari mwaka 1924, hivi sasa ana miaka 86 amesema yuko tayari kugombea urais kwa mara nyingine kuliongoza taifa la Zimbabwe.Akiongea na waandishi wa habari mjini Harare, rais Robert Mugabe ambaye anaendelea kuiongoza Zimbabwe kwa miaka 30 sasa, alisema kuwa yuko tayari kugombea tena urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika miaka miwili ijayo.Mugabe alisema kuwa iwapo chama chake cha ZANU-PF kitampitisha kugombea urais basi atasimama kwa mara nyingine kugombea urais.

Mugabe ambaye alianza kuitawala Zimbabwe tangia ilipopewa uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1980, alishinda uchaguzi wa urais uliopita ingawa kambi ya upinzani iligoma kukubali matokeo ya uchaguzi ikisema kuwa hila zilifanyika.Hali hiyo ilisababisha mtafaruku nchini Zimbabwe ambapo uchumi wake uliyumba kutokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na mataifa ya magharibi.
Pesa ya Zimbabwe ilipoteza thamani yake na kuifanya Zimbabwe izitose pesa zake na kuanza kutumia dola za kimarekani na Rand za Afrika Kusini kama mbadala wa pesa zake.