Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, December 31, 2009

Mzee Rashidi Mfaume Kawawa katikati akisalimiana na Raisi Jakaya Kikwete amefariki dunia asubuhi katika hospitali ya Muhimbili katika chumba cha wagonjwa mahututi. Kulia ni mke wa Marehemu kawawa. Kwa kifupi; Mzee Rashidi Mfaume Kawawa alizaliwa tarehe 27 February, 1926 katika kijiji cha Matepwende, Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Tanzania. Alianza elimu ya msingi huko Liwale, Lindi mnamo 1941 - 1942 na kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya skondari Dar es salaam,. Huyu ni mwanasiasa mwenye historia ndefu lakini itoshe kusema tu kwamba kuanzia tarehe 22 Januari, 1962 hadi tarehe 13 Februari, 1977 alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Alifuatwa na Edward Sokoine. Baadaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. Raisi Jakaya Kikwete akilihutubia taifa mchana wa leo wakati akitangaza kifo cha Mzee rashidi Mfaume Kawawa . Taifa litakuwa kwenye maombolezo kwa siku saba ambapo bendera zitapepea nusu mlingoni. Mungu ailaze roho ya Mzee Kawawa peponi Amin. Nyumbani kwa Mzee Kawawa Madale, Dar es salaam.

Posted by BM. on Thursday, December 31, 2009

!
Kuna ubaya gani tukapiga kigelegele kuukaribisha mwaka mpya?...Happy New year!

Posted by BM. on Wednesday, December 30, 2009

Moja ya ziara ya Viongozi ni hii ya Rais wa zamani wa Marekani George .W.Bush ambapo hapa alikuwa na mwenyeji wake Raisi Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Amana jijini Dar es salaam. QUIZ!Hebu kisia nini walichokuwa wakiteta.

Posted by BM. on Wednesday, December 30, 2009

St. Augustine University-Mwanza tawi la Mtwara ...upo hapo?
Bandari ya Ntwara kutoka Juu.
Soko kuu la Mkoa wa Mtwara! Nyanya Zimeingia sokoni Ntwara!
Kazi niliyotumwa na taifa huku Ntwara imemalizika sasa narejea Mwanza...5 Mgosss! Precision Air ikijiandaa kuruka NTWARA Int. Airport. Mwandishi wa habari Peter Omari akiwa ndani yake baada ya kumaliza majukumu.<

Posted by BM. on Tuesday, December 29, 2009


Naenda Kuzungumza na waajiri wangu laiv!

Posted by BM. on Tuesday, December 29, 2009

Umefika soma bango hapo. Mchakato wa kuipata waini unaleta bidhaa saba; Juice, Cyrup, Pickle, Jam, Tutty fruit, Chartney na WINEEEE .

Waini ya kwetu...Ushaionja hiyo!

Posted by BM. on Monday, December 28, 2009

Jiji a Morogoro limerindima kwa Sherehe kabambe ya harusi ambapo Bw. Khalifa Msulwa na Bi. Naima walikata shauri la kuanza maisha ya ndoa mke na mume. Safari katika ukurasa mpya imeanza..Hongereni sana!
Bw. na Bi. Msulwa Kh..href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyP5x3sWQ-ikyOGTAQd_Xs5txvaqj0tdmB756AF-i1gHQhortYcWd7e-4nNaDdOyKi-Z1YrMV3r1GxhxhhX2juovof8Nlpg4FC-KZiXmrneyonakJOSXDl5icJzJrdDwEoarFo8X-3Uzo/s1600-h/saha+.m+528.jpg">
Bwana na Bibi harusi wakitoka ukumbini baada ya Sherehe kumalizika..Hongereni sana na karibuni katika changamoto za maisha ya ndoa..

Posted by BM. on Monday, December 28, 2009

Krismas imekuja na kupita ...mwaka mpya unajongelea. Wacha tukumbukie siku ile...Nguo za sikukuu!

Ilifana...japo kibaridi.

Posted by BM. on Monday, December 28, 2009

Msosi wa Mtwara villa Resort; Utamu wa Menyu mwangalie mlaji usoni...5 mgosss! Penyee ndio hapo! Kma hujafika hapa hujafika Mtwara! Mjasiliamali Mtwara huko!
TANESCO imekabidhi libeneke la umeme kwa hao jamaa ...soma hapo!Ntwara hiyo.

Posted by BM. on Monday, December 28, 2009

Baadhi ya Idhaa za Redio Japani zinaendelea na sherehe za kuukaribisha mwaka mpya ambao unakaribia kupiga hodi. Leo ilikuwa idara yetu inayojumuishaidhaa zaidi ya 10. Kwa ujumla NHK ina idhaa 18. Fuatilia sherehe hiyo kwa njia ya Picha. Idhaa ya kihispaniola... Upande wa Idhaa ya Kipersia...Lugha maarufu Iran na baadhi ya sehemu za Iraq.. Mwakilishi wa idhaa ya Kiarabu akizungumza Idhaa ya kiindonesia na Thailand... Benchi la Ufundi idhaa ya kiswahili ..du namii nipo ila nimeshika amera..nawakilisha!.
Mandhali ya ukumbini...

Posted by BM. on Monday, December 28, 2009

Injinia wa Shirika la Utangazaji la Japani Hoshiya Kihonda amestaafu rasmi kazi baada ya kuifanyika kazi Redio Japani kwa miaka 35. Ana historia ndefu katika NHK lakini kubwa amefanya kazi zake kwa uaminifu mkubwa na ametokea kupendwa na wafanyakazi wenzake hususan wale wa mataifa ya kigeni. Kila la kheri .
Akiwa na Komred Ndesika...
Baadhi ya wadau wa RJ pamoja na Bw. Yoshia Kihonda.

Posted by BM. on Sunday, December 20, 2009

Wapenzi wa MIRINDIMO, nawatakia kila la kheri ya Krimas na maandalizi ya Mwaka mpya.....Naomba radhi mtandao huu umepatwa na kwikwi kidogo lakini marekebisho yanaendelea na utakuwa barabara muda mfupi ujao....tuko pamoja-BM.

Miaka 85 mguu unatanuka...najua weye hujafika hiyo miaka iga uone !

Posted by BM. on Sunday, December 20, 2009

Dar Leo J2 Mchana! Kama hujafika hapa hujafika Dar ...Uongo , Kweli?...Usijibu! Unaikumbuka Gogo Hoteli enzi zake , wajanja lazima wafike hapo. Leo mchana ilikuwa katika sura hii ...ukarabati! Chombocha kuelekea kwetu Kigamboni ! Kumuenzi mwalimu J.K.Nyerere kwa ofisi mpya...Dar.
Mwandishi wa habari wa Kimataifa mgosi Peter Omari akiwa tete na Mwakilishi mkazi wa mashirika ya UN nchini Tanzania Alberic Kacomara ofisi kwake Kinondoni Dar es Salaam.
Foleni ya Buguruni Bandari ya salama hii leo....

Posted by BM. on Saturday, December 19, 2009


Mdada huyu huko Vwawa , Mbozi alipanda ndani ya basi na kitoweo chake na alipokuwa akishuka ndio nguruwe alipoguna na watu wakagutuka . Lakini kwa furaha alisema kuwa alikuwa rafiki yake wa karibu na hakuwa na tatizo naye. Duh!.

Posted by BM. on Saturday, December 19, 2009

WATU 18 wamefariki dunia papo hapo na wengine 35 kujeruhiwa vibaya baada basi la Kampuni ya Mohamed Trans kugongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Coaster. Habari ambazo zilipatikana kutoka eneo la ajali zinasema, tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 10:30 jioni katika Kijiji cha Kandoto kilichopo nje kidogo ya mji wa Same. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’obhoko aliwaeleza waandishi wa habari kuwa chanzo cha ajali hiyo kinasemekana kuwa ni kupasuka kwa tairi la mbele la basi la Mohamed Trans. Alilitaja basi la Mohamed Trans lililohusika katika ajali hiyo kuwa ni lenye namba za usajili T 810 BCB lililokuwa likisairi kutokea Nairobi, Kenya kuelekea Dar es Salaam wakati basi dogo lilikuwa na namba za usajili T 810 AQM lililokuwa likitokea barabara ya Dar es Salaam - Moshi. Kamanda Ng’obhoko alisema miongoni mwa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni dereva wa Coaster ambaye katika gari alilokuwa akiendesha ndiko waliathirika abiria wengi. Alisema miili yote ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Same wakati ikisubiri taratibu nyingine. “Tunafanya jitihada kubwa kuhakikisha majeruhi wote wanapatiwa tiba haraka kabla ya kuwahamishia Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi na ile ya Rufaa ya KCMC,” alisema. Kamanda Ng’obhoko, alisema miongoni mwa watu waliofariki dunia ni watoto wawili huku majeruhi wakiwa wanawake 20 na wanaume 15. Alisema dereva wa basi la Mohamed Trans, Waden Abdallah Kiyungi aliumia vibaya miguu yote. Akizungumzia mazingira ya ajali hiyo alisema, baada ya tairi la Mohamed Trans kupasuka, basi hilo liliyumba kisha likapoteza mwelekeo kabla ya kuparamia basi dogo. Naye Mkuu wa Wilaya ya Same, Ibrahim Marwa aliiambia Tanzania Daima kwa njia ya simu kuwa, juhudi kubwa za kutoa tiba zilikuwa zikifanyika kwa kushirikisha taasisi zote za serikali wilayani hapa. “Tuko kwenye operesheni ya kuona ni namna gani tunaweza kuwasaidia Watanzania wenzetu hawa, wapo wenye hali mbaya, tunalazimika kuwakimbiza KCMC kwa ajili ya matibabu zaidi,” alisema Marwa. Alisema kazi hiyo ilikuwa ikifanywa na vikosi vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na watu mbalimbali.(Picha na habari na Grace Masha wa Tanzania daima)

Posted by BM. on Saturday, December 19, 2009

Raha ya kilaji inaonekana katika paji la uso.

Posted by BM. on Friday, December 18, 2009


Picha ya Kumbukumbu baada ya kuwaapisha Mabalozi wapya wa Tanzania nje ya nchi. Kutoka kushoto Dr. James Nzagi, Balozi mpya nchini Burundi, Mh. JK, Mh Salome sijaona (Japani)na Balozi mpya wa Saudi Arabia Prof. Abillahi Omari.

Posted by BM. on Thursday, December 17, 2009


...."Kiongozi anayetufaa Tanzania , ni yule anayejua kuwa nchi yetu ni masikini na watu wake ni masikini. Na ukimwangalia usoni ...uone anaguswa na umasikini wetu. Vinginevyo hatufai...." J.K.Nyerere.
Ndio maana yake...

Posted by BM. on Thursday, December 17, 2009

Raisi Barack Obama wa Marekani hivi majuzi aliipokea rasmi nishani yake ya Nobel huko Norway. AAh safi...kumbe ndio hii!
Nishani yenyewe hii hapa.
Raisi Obama , Mkewe na familia ya kifalme huko Norway.

Posted by BM. on Thursday, December 17, 2009

ATC nao wamo ...kama unavyomuona Intl PP.P.O.
Tumefika

Umeshafika hapo!