Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, July 25, 2010

FUATANA NAMI KATIKA SAFARI YANGU YA ARUSHA , ; Funga mkanda.



Nikielekea Arusha , daraja la wami likionekana kupitia kioo cha dereva...




Mapumziko kwa ajili ya chakula cha mchana ...Mombo vifaa vya usafiri vikitusubiri...




Mombo njiani kwenda Arusha ..matunda tele kijikapu mia tano na mfuko mrefu elfu. Maumivu ya kichwa kwa wakulima matunda yanaharibika shamba...




Nimekutana na Afande wangu wakati wa mapumziko ya shule ...


Niko na mdau maarufu wa habari jijini Arusha Mr. Mchau tukionja soda mpya ambaye kwa-Tz ilitoka

kitambo...na nyama ile ya kukausha kidogo..sina maswali..




Eneo la makao mapya Arusha wenyeji wanatuambia kunataka kuwekwa lami ...sijui lini labda kuelekea Oktoba ..du!




Tunaingia stendi kuu -Arusha..




Haya unakwenda wapi mkubwa!...

Posted by BM. on Wednesday, July 21, 2010


Samahani wapenzi wa Mirindimo kwa ukimya...niko likizo Bongo..jiandae kupata habari nyingi kwa njia ya picha...kwa sasa anza na hizo!...

Posted by BM. on Wednesday, July 21, 2010

Onyesho la wana Twanga pepeta mjini Morogoro eneo la nane-nane Grones Pub juzi usiku...ilikuwa pata shika nguo kunanihii...pata picha chache za eneo la tukio...



Hatumwi mtu hapo...

Posted by BM. on Wednesday, July 21, 2010


Milima ya Uluguru..


Chips dume kabla ya kukwea pikix2


Njia panda ya Kinole, Morogoro...

Posted by BM. on Wednesday, July 21, 2010


furaha inaanzia kwenye screen saver

Madizini -Turiani...mtaa wa sikukuuu . Karibu na geti la kuingilia Kiwanda cha sukari cha Mtibwa, Morogoro.

Posted by BM. on Wednesday, July 21, 2010


Eneo la kwanza kulifikia ni hapa ...kaburi la baba yangu na ndugu zangu wengine. Nimefarijika sana...

Posted by BM. on Wednesday, July 21, 2010


Safari ya mjini Dar es salaam.

Posted by BM. on Wednesday, July 21, 2010


Keki ya kunikaribisha nyumbani...
On transit...DUBAI


Uwanja wa ndege wa Dubai ...kiwango mwananchi..

Posted by BM. on Saturday, July 10, 2010


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Raisi Jakaya Kikwete akikaribishwa kwenye Jukwaa kuu mjini Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Bw. Yusufu Makamba ili kuongoza kikao cha Halmashauri kuu ya chama hicho.

Dr. Ally Mohamed Shein ,Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ameteuliwa na Chama chake cha CCM kupitia Mkutano wa Halmashauri kuu-NEC kuwa Mgombea wa Uraisi wa Zanzibar.



Dr. Shein ndiye atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa mwezi Oktoba wa mwaka huu utakaofanyika huko Tanzania.


Taarifa za awali zilizochapishwa na blog ya Jamii zinasema kuwa Wajumbe wa NEC walimpa kura 117 Dr. Shein ambapo Dr. Gharib Billal alipata kura 54 na Mh. Shamsi Vuai Nahodha , Waziri kiongozi wa sasa wa Zanzibar akiambulia kura 33.Unaweza kufuatilia wasifu wa wagombea hao walioingia tatu bora hapo chini;

The three finalists' profile
Dr Ali Mohammed Shein
Few people know that the incumbent Vice President, Dr Ali Mohammed Shein, is a medical doctor by training. He holds a PhD in clinical biochemistry and metabolic medicine, specialising in “Inborn errors of metabolism.”Being a medical doctor, Dr Shein has been a member of various professional organizations, including the Association of Clinical Biochemists of the UK, the Association of Clinical Pathologists for Eastern, Southern and Central Africa(APESCA), the Association of Clinical Pathologists of Tanzania and the International Association of Inborn Errors of Metabolism. The VP’s political career began way back in 1966 when he joined Afro-Shiraz Party Youth League (ASPYL) before he was named ASPYL publicity secretary at Lumumba Collage in Zanzibar. He joined CCM eight months after the party was born. He become a member of the CCM National Executive Committee for Pemba, South Region.


Many Tanzanians were caught by surprise when the former President Benjamin Mkapa appointed Dr Shein on July 13, 2001, to become the Vice President following the death of Dr Omar Ali Juma. Dr Shein's experience as a civil servant stretches back to 1969 when he joined the Isles’ Ministry of Education as assistant to the deputy principal secretary. Since then, he headed various government departments until October 1995 when he was nominated by the former Zanzibar President, Dr Salmin Amour, as a Member of the House of Representatives. A month later, he was appointed deputy minister in the Ministry of Health. On November 6, 2000, he was elected Member of the House of Representative for Mkanyageni constituency in Pemba, and on November 22, 2000, was appointed by President Amani Abeid Karume minister of State in the President's Office, responsible for Constitution and Good Governance.
Born in March 13, 1948 in Chokocho, Pemba, Dr Shein, apart from being a loyal civil servant, is a married man and a father. Those who happen to be close to him say he loves sports such as athletics and football. As an intellectual, he also loves reading.His critics say he is a “hard sale” because he is rather withdrawn, though he is known to be very pro-Union. Again, he is viewed by some of his close associates as a stickler to regulations and procedures.

Dr Mohamed Gharib Bilal
Born on February 6, 1945, in Unguja, Dr Bilal is a scientist who obtained his first degree in nuclear science from Howard University in the US in 1967.In 1969 he obtained a master’s degree in nuclear science from California University also in the US. He obtained his doctorate degree in physics from California University in 1976.
Between 1990 and 1995 he served as the permanent secretary in the Ministry of Science, Technology and Higher Education in the Union government. From 1976 to 1990, he was a lecturer at the University of Dar es Salaam Department of Physics. In 1982 he became the head of the Faculty of Science at the University of Dar es Salaam.
Between 1993 and 1990 he served as a member of the National Radiation Commission Board. After the 1995 General Election, Dr Bilal was appointed Zanzibar Chief Minister by President Salmin Amour. During 2000 General Election, he contested the Zanzibar presidency but lost. Although CCM in Zanzibar had given him high marks, subsequent top party meetings deleted his name in favour of Mr Amani Abeid Karume who went on to win the Isles’ presidency.“Zanzibaris should expect major changes in development if I win the post. I will strengthen the Union and ensure that its problems are addressed,” says Dr Bilal.

Mr Shamsi Vuai Nahodha
Born on November 20, 1962, Nahodha is Zanzibar Chief Minister. He holds a diploma in languages from the Institute of Kiswahili and Foreign Languages in Zanzibar.
He speaks fluent French, a language he studied at Bujumbura University after graduating with a bachelor’s degree from the University of Dar es Salaam in 1987. He received his master’s degree from the Open University of Tanzania in 2008.
In 2000 he was elected the Mwera House of Representative before he was appointed chief minister in the same year. In 2005 he was elected the Representative for Mwanakwerekwe constituency and President Karume retained him as the Chief Minister.
“The Chief Minister is the chief executive of the government, but the head of government is the President. I am asking my party to give me the opportunity to serve as the head of the State so that I can use my experience as the chief executive officer to push the development agenda forward,” he says.


Wagombea kabla ya kupigwa kura!..

Posted by BM. on Thursday, July 08, 2010

Hatimaye sasa imejulikana kuwa ule mpambano wa fainali Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini utakuwa baina ya Uhispania na Uholanzi.


Mechi iliyochezwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban ulimalizika kwa Uhispania kuinyuka Ujerumani goli moja kwa bila na hivyo kufuzu kuingia katika fainali kwa mara ya kwanza katika historia.
Bao pekee la mechi hiyo lilifungwa kwa kichwa na mlinzi Carles Puyol katika dakika ya 73, alipopanda mbele kucheza mpira wa kona.
Ujerumani walionekana kikosi tofauti kabisa na timu ambayo iliiondoa England kwa kuifunga mabao 4-1 na baadaye kuitandika Argentina mabao 4-0 kwenye mechi ya robo fainali.


Pengo la mshambuliaji Thomas Muller ambaye alikuwa nje kutokana na adhabu ya kadi mbili za njano lilikuwa wazi kabisa kwenye safu ya ushambuliaji ya Ujerumani.
Muller ambaye ameshafunga mabao manne kwenye Kombe la Dunia alipata kadi ya pili ya njano kwenye mechi kati ya Ujerumani na Argentina, na bila yeye, kocha Joachim Loew alikosa kabisa mbinu za ushambuliaji kwa timu ya Ujerumani.Hispania walidhibiti mchezo katika muda wote, na wangeweza kufunga mabao mengi zaidi lakini umaliziaji ukawa mbaya, pamoja na mlinda lango wa Ujerumani, Manuel Nuer kuokoa mipira kadhaa.
Fainali ya siku ya Jumapili kati ya Hispania na Uholanzi katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg itawakutanisha wafungaji wanaaongoza kwa sasa; Wesley Snijder na David Villa.Ni mara ya kwanza kwa Hispania kucheza fainali ya Kombe la Dunia, na kwa upande wa Uholanzi itakuwa mara ya tatu, ingawa bado hawajapata kushinda Kombe hilo.Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na wanne itachezwa Jumamosi kati ya Uruguay na Ujerumani.

Posted by BM. on Thursday, July 08, 2010

Ikaribishe weekend yako hapo kwa zilipendwa....mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya..

Posted by BM. on Wednesday, July 07, 2010


Nje ya majukumu makubwa ...familia na hususan mwenza ni muhimu..
Barack Obama and his wife Michelle celebrated the 4th of July by having a barbecue for military members and families and government employees and families on the South Lawn on Sunday.The first family open there home to the public this 4th of July as they do every year, barbecue, fun, family and fireworks were all on the menu to those who took in the 4th of July festivities.

Posted by BM. on Wednesday, July 07, 2010


Mwanariadha wa Afrika Kusini Castor Semenya amepata idhini kutoka shirikisho la riadha duniani IAAF kurejea kushiriki mashindano ya riadha kama mwanamke.
Semenya mwenye umri wa miaka 19, hajashiriki mashindano yoyote katika muda wa karibu mwaka mmoja kutokana na utata kuhusu jinsia yake, na amekuwa akisubiri matokeo ya kubaini ikiwa ni mwanamme au ni mwanamke.ata huo ulizuka Agosti mwaka uliopita kwenye mashindano ya mbio za ulimwengu mjini Berlin wakati Semenya aliposhinda mbio za mita 800 kwa wanawake huku akimwacha mpinzani wa karibu kwa zaidi ya mita 20.
Kufuatia utata huo ambao pia ulikuwa umejitokeza kwenye mashindano ya riadha kwa vijana barani Afrika, IAAF iliagiza uchunguzi kufanyika kubaini jinsia ya Semenya ili kuamua ikiwa ataruhusiwa kuendelea kushindana kama mwanamke.


Taarifa kutoka IAAF imethibitisha uamuzi huo wa kumpa idhini Semenya kuendelea kushiriki katika mashindano ya riadha kama mwanamke, baada ya kamati ya wataalamu wa afya kukamilisha uchunguzi wake.Taarifa hiyo imesema, ''Mchakato ulioanzishwa mwaka 2009 kuhusu Castor Semenya umekamilika. IAAF inakubali kauli ya kamati ya wataalamu wa afya kwamba anaweza kuanza kushiriki mashindano ya riadha mara moja.''
Hata hivyo taarifa hiyo imesema maelezo ya afya kuhusu jinsia ya Semenya yatabakia kuwa siri, na IAAF haitasema chochote kuhusu swala hilo.Kufuatia idhini hiyo Semenya anaweza kuamua kushiriki mashindano ya kimataifa ya vijana nchini Canada baadaye mwezi huu, lakini huenda akapendelea kuanza kujiandaa kwa michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika mjini New Delhi, India mwezi Oktoba.
Mjini Berlin Semenya alishinda mbio za mita 800 kwa muda wa dakika moja sekunde 55.45, na kumwacha kwa karibu mita 20 aliyekuwa bingwa wa dunia wakati huo Janeth Jepkosgei kutoka Kenya.Rekodi ya dunia ya mbio za mita 800 ni dakika moja sekunde 53.28 iliyowekwa na Jarmila Kratochvilova wa Jamhuri ya Czech mwaka 1983 na haijapata kuvunjwa tangu wakati huo.Kuidhinishwa kwa Semenya kuendelea kushiriki mbio za mita mia nane kama mwanamke huenda kukatoa fursa ya rekodi hiyo kuvunjwa.

Posted by BM. on Wednesday, July 07, 2010


Shule ya watoto wadogo umasaini kilipo kijiji chetu...Samaki mkunje angali mchanga...

Posted by BM. on Monday, July 05, 2010


Bingwa wa dunia wa zamani wa ndondi, Mike Tyson ambaye alibadili dini kuwa muislamu alipokuwa jela kwenye miaka ya 1990 yupo nchini Saudi Arabia kwaajili ya hija ndogo.Bingwa wa dunia wa zamani wa ngumi za uzito wa juu, Mike Tyson anatembelea miji mitakatifu ya waislamu Makka na Madina kwaajili ya kuhiji.
Tyson ambaye alikuwa bingwa dunia kuanzia mwaka 1986 hadi 1990, aliwasili Madina siku ya ijumaa akiwa na maafisa wa umoja wa Daa'wa wa Kanada kwaajili ya Umrah ambayo ni hija ndogo.
Baada ya kutoka Madina, Tyson ataenda Makka na gazeti la Okaz la Saudia limeripoti kuwa Tyson ana mpango wa kutembelea pia miji mingine ya Saudia.
Tyson mwenye umri wa miaka 44 alibadili dini kuwa muislamu wakati alipokuwa jela akitumikia kifungo cha miaka 10 jela kwa kumbaka mrembo wa Marekani mwaka 1991. Hata hivyo alitumikia miaka mitatu jela na kuachiwa huru.

Mike Tyson akizungumzia uamuzi wake wa kuwa muislamu na jinsi anavyotekeleza ibada zinazohitajika katika dini hiyo.....

Posted by BM. on Monday, July 05, 2010

Kumbuka; taarifa hii imenakiliwa neno kwa neno kutoka blogi ya nifahamishe-BM.
Msanii mkongwe hapa chini wa muziki wa Bongo Fleva, Mr II aka Sugu anatamba na albamu yake Anti Virus ambayo ndani yake kuna nyimbo ambayo ametaja watangazaji wa radio Clouds anaodai wanasambaza ukimwi huku wengine akiwataja kuwa ni mashoga.
Msanii mkongwe hapa nchini Joseph Mbilinyi aka Mr 11 Sugu, ameliteka jiji la Dar kutokana na albamu yake ya Anti Virus ambayo ndani yake amewapaka live watangazaji na viongozi wa redio ya Clouds FM.KWa mujibu wa Mr II watangazaji hao wanadaiwa kutumia redio hiyo kwa kuwatongoza wanawake wanaokwenda pale kuomba kazi pia kuzibania kazi za wasanii ambao hawapo katika listi yao.Mr II pia amewachana live kundi la THT Kituo cha kukuza vipaji Tanzania Kuwa kituo hicho kinatumika kinyume na ilivyotarajiwa.Albamu hiyo ya Sugu ina nyimbo zaidi ya 14 lakini hapa nchini haziwezi kupigwa katika vituo vya redio kutokana na kujaa matusi ya hadharani, hivyo albamu hiyo imekuwa ikiuzwa chini kwa chini na watanzania wengi wamekuwa wakiishambulia kwa kuinunua hasa wale wapenda mapinduzi katika fani hiyo ya muziki wa kisasa kwani vijana wengi wamekuwa wakibaniwa kazi zao kutokana na kutofahamika au kutokana na kutokuwa na uhusiano muzuri na watu wa redio na Tv.Majuzi Sugu alikamtwa na polisi na kupelekwa makao makuu ya jeshi la polisi kwa mahojiano, lakini baadaye aliachiwa kwa dhamana.MR II amewaweka njia panda watangazaji wa Clouds hasa kwa kuwataja live baadhi ya watangazaji kuwa wanasambaza Ukimwi kwa makusudi huku wakijua kuwa wao ni waathirika wa ugonjwa huo.Pia aliwataja baadhi watangazaji kuwa ni wasenge jambo ambalo limewafanya watu wengi wajiulize imekuwaje hadi Mr II ameamua kutunga nyimbo hiyo na kuisambaza kwa watanzania?.



Mmmh Mi sichemi!

Posted by BM. on Sunday, July 04, 2010

Jioni ya leo J2 Mjapani mmoja ambaye ana mapenzi makubwa na waafrika alitualika nyumbani kwake. Huyu ni Hiroshi Ikeuchi ambaye anazifahamu sana nchi za Afrika ya Mashariki, mtaa kwa mtaa.Kwahakika ilikuwa hafla nzuri sana iliyowajumuisha washiriki kutoka mataifa ya Tanzania, Uganda, Botswana na zambia na karibu wote walikuwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali vikuu hapa Japani isipokuwa wachache kama miye....Ilikuwa jioni njema tulikunywa , kula na kuzungumza na kubadilishana taarifa .

Mdau kutoka Tz...


Wadau wakijikusanya M-Zambia kushoto na M-Tz kulia.


M-Tz Bi. Recho..

Posted by BM. on Sunday, July 04, 2010


Mwenyeji wetu Bw. hiroshi Ikeuchi...akitukaribisha kupata chakula...

Posted by BM. on Sunday, July 04, 2010


Sijui nianzie wapi...acha tu!

Wacha nishughulike na hiki kwanza....

hai tebo...wananchi walikuwa bize kwenye chakula...

Huyu jamaa wa Kiganda mcheshi sana alifurahisha baraza..


Mwenyeji wetu alipita kila kona kuhakikisha kila kitu kinaenda barabara...


Ufafanuzi wa menyu..

Posted by BM. on Sunday, July 04, 2010


No ..no.. sahani moja si yangu jamaa kaiacha..ane wei..!


chakula na stori....Jmaa mwenye t-shirt nyekundu M-Uganda, Mdada wa kati kati M-Botswana na kulia mdada wa Tz.


Dr. Kibusi Kushoto na da Recho katika menyu...