Mwanamuziki huyu Malkia Nvannungi ni moto wa kuotea mbali kule nchini Uganda unaweza kusikiliza nyimbo zake hizo mbili....ya kwanza Doctor na ya pili hapo chini ameimba na Q-Chillar kutoka Tanzania ... kama wewe ni mpenzi wa rumba la taratibu naamini utasuuzike......take 5, Nvannungi nakukubali...
Nakupenda...
Ni hapa...
Kocha maarufu kwa jina la Super Coach Sylversaid Mziray 'Mwanangu' amefariki dunia jana asubuhi katika hospitali ya AgaKhan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwasiku kadhaa zilizopita.
atakumbukwa na wapenzi wa soka kwa mchango wake mkubwa wa mawazo na wa kivitendo . Amewahi kuzifundisha timu za simba na Yanga pamoja na Taifa Stras kwa nyakati tofauti. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Aiweke roho ya Mziray peponi , Amin...
Marehemu Syllersaid Mziray, enzi za uhai wake.
Taarifa ya MAKAMU Mkuu WA Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Tolly S.A. Mbwette, kwa niaba ya Menejimenti yote ya Chuo,imetoa tamko juu ya msiba huo wa mkufunzi wake wa michezo, Syllersaid Mziray.
"Mziray alifariki dunia alfajiri ya kuamkia leo Jumamosi katika hospitali ya Aga Khan alikokuwa amelazwa kwa karibu wiki mbili kutokana na Malaria na baadaye matatizo ya figo.Taratibu za Mazishi zinaendelea nyumbani kwake Tabata Magengeni. Mziray atazikwa Jumatatu kwenye Makaburi ya Kinondoni.
Mazishi hayo yatatanguliwa na utoaji wa heshima hapa chuoni.Mungu ailaze roho ya marehemu Syllersaid Mziray Pema Peponi Amen!", taarifa hiyo ilimaliziwa na kusainiwa na KURUGENZI YA MAWASILIANO NA MASOKO kwa niaba ya Chuo hicho
Mtangazaji wa Redio Japani Bi. Anna Kwambaza hivi karibuni alipata fursa ya kutembelea eneo la kihistoria la Hiroshima ambako bomu la atomiki lilidondoshwa na majeshi ya Marekani mwaka 1945 , mwishoni mwa vita vya pili ya dunia.
Hii ni sehemu pekee duniani ambako silaha ya maangamizi ya atomiki imetumika...unaweza kufuatilia historia hiyo kwa muda wako hapo chini.
Mdau hapo akiwa mbele ya Kuba la bomu la atomiki Hiroshima. Lilidondoshwa hapo na kuacha mabaki hayo
Safari ya kileleni kwa kutumia rope car huu ni mlima Misen ili kuuona mji wote wa Hiroshima kutoka Juu
Watangazaji wa Redio Japani; Anna kwambaza na Chiho Yamada wakiwa Hiroshima , Japani....
Baada ya kazi...msosi...chakula kinaitwa okonomiaki inataka uvumilivu ulozoea pilau na samaki wa tui bubu
Vimbwanga vya mzee Yusuf...."Nataka paja mie sitaki kipapatio...
Watu bwana Uuuh!
Mke wa Raisi w Iran Mahmoud Ahmadinejad, Azam Farahi (wa pili kutoka kulia), Mke wa raisi wa Lebanon Bi. Wafa Sleiman (watatu kutoka kulia ) na mke wa Spika wa Bunge la Lebanon Nabhi Berri, Bi. Randa (Kulia), katika Chakula cha Usiku kilichoandaliwa huko Beirut , Lebanon ambako Raisi Ahmed Nejad anafanya ziara!
Raisi Sebastian Pinera wa Chile katika picha ya pamoja an wachimbaji 33 waliokolewa kwenye migodi baada ya kufukiwa na udongo , hapo wapo katika hosiptali moja ya Copiapo nchini humo
Mchimba madini aliyeokolewa nchini Chile Osman Araya akimfariji mkewe baada ya kuvutwa kutoka ardhini . yeye alikuwa mtu wa sita kati ya 33 kuokolewa baada ya kukaa chini ya ardhi kwa siku 69. Hebu fikria nyoyo zao zilikuwa zikiwaza nini hapo!
Muda mfupi uliopita tumetoka kwenye tamasha la kijadi la kila mwaka la wajapani huko Saitama eneo la Kawagoe-shi ambapo tulialikwa Nyumbani mwa mhadhiri wa lugha ya Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Soka hapa Japani na ndugu yangu Edward Kadilo Mtangazaji mwenzangu wa NHK hapa Tokyo pamoja na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili.
Safari ilianza kwa uopigaji wa picha...
Tulipigwa picha kwanza ...Ni Haluka nakamura na Melisa..
Kadilo, Ruci,Mie,Haruki...
Baada ya kushuhudia tamasha la ngoma za kijadi za kijapani...tukaalikwa nyumbani kwa Bi. Midori Uno na dada yake Lumiko Uno kwa ajili ya chakula cha mchana...
Haruki , na Melisa...
Chiazzz, Ruci,Kadilo na Haruki...
Kabla ya kufunga menyu kwa kahawa tulikula hili tunda...Watambuzi tambueni laitwaje hilo tunda?
Tulikwenda kutembelea mnada wa magari katika mkoa wa Gumna , eneo la Ooyama kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya MAEJI ya uuzaji wa magari yenye makao yake hapa Japani ambayo Mkurugenzi wake mkuu ni Mkenya Jeff Musyoka. Fuatilia picha hizi na baadaye ukitaka kuijua kampuni hiyo bofya; www.maeji-kaiho.com
Tumeshuka Mushashi-Urawa kuanza safari ya kwenda Mkoani Gumna kwenye huo mnada wa magari, kipande cha safari , takriban saa moja na nusu kwa gari inayotimua mwendo.
Magari ya watu wanaokuja mnadani hupaki hapa...
Tuanzie hapa kwenye pikipiki...
Mwenyeji wetu Jeff Musyoka akituongoza tuangalia vifaa ...
Imetulia au!
Huwa kuna vyumba maalum ambavyo wanunuaji wa magari wanaotambuliwa na Makampuni ya uuzaji magari huingia ambako kuna komputa maalum zenye taarifa zote juu ya kila kitu kilicho kwenye mnada ...wao wanauwezo wa kujua bei na kufuatilia...Ugeni tena nilishindwa kupiga picha ndani nikatoka nje...
Baadhi ya wanachama wa minada hii na waalikwa hukaa jengo la nje kufuatilia aina za magari na bei na hutoa taarifa kwa njia ya mtandao kuwa wako tayari kuchukua kifaa hicho...Mabango hayo ndio huttoa picha na bei..