Polisi nchini Japani wamepeleka ripoti yao kwa waendesha mashitaka kuhusiana na Maafisa wa uhamiaji 10 wanaotuhumiwa kumshambulia raia mmoja kutoka nchini Ghana , wakidai kuwa mghana huyo aliyekuwa akisafirishwa kwenda kwao mwezi Machi aliteswa jambo lililosababisha kifo chake.
Vyanzo vya uchunguzi huo vilibainishwa jana Jumanne na kuchapishwa katika mitandao kadhaa hapa Japani. Ingawa hawajakamatwa , maafisa hao wanatuhumiwa kuhusika na kifo cha Abubakar Awudu Suraj mwenye umri wa miaka 45 aliyekufa baada ya maafisa kadhaa kutumia nguvu alipoonekana kuleta ‘Upinzani’ wakati wa kumuingiza ndani ya ndege katika Uwanja wa ndege wa Narita. Ndege hiyo ilikuwa ikielekea ikielekea Cairo nchini Misri. Mgahana huyo anadaiwa kuwa alikuwa akiishi nchini Japani kinyume cha sheria na hivyo ilikuwa harakati za maafisa hao za kumrudisha kwao na hii ilikuwa mwezi machi, vyanzo vya habari vilibaini.
Polisi huko Chiba nje ya Jiji la Tokyo walisema mapema kuwa uchunguzi wa mwili wake katika Postmortem ulibaini kuwa hakukuwa na majeraha nje ya mwili wake , wala kuvunjwa kwa mifupa, ugonjwa na sababu nyingine zinazoweza kusababisha kifo hicho lakini mwezi Juni Mjane wa Suraj mwenye umri wa miaka 49 alifungua shauri hilo pamoja na waendesha mashitaka dhidi ya maafisa hao wa uhamiaji. Tuhuma kulingana na shauri hilo linawashutum maafisa wa uhamiaji kumjeruhi na kusababisha kifo chake wakati wakati wakimsafirisha kwenda kwao.
Ofisi moja katika kitengo cha uhamiaji cha jiji la Tokyo ambayo maafisa hao wanaotuhumiwa wanafanyia kazi jana jumanne walieleza utayari wao wa kushirikiana katika uchunguzi wa suala hilo.
Tamko hilolinasema kuwa “Tutaendelea kushirikiana katika uchunguzi na kwamba watatoa ushirikiano unaohitajika kwa watu wote wanaohusika na suala hilo ikiwa ni pamoja na familia yake kuhusiana na ucunguzi wa suala hilo.
Ni hapa...
Supu bia , thupu thoda ….kumbe supu ya mbwa! Watu bwana .Wakazi wa mjini Tabora, wamejikuta wakila mbwa bila kutaka baada ya baadhi ya bar kuaanza kutumia mbwa kwa supu na nyama choma.
Maafisa afya waandamizi katika halmashauri ya manispaa ya Tabora, ambao hata hivyo wameoomba majina yao yahifadhiwe juzi walikuta mbwa akiwa amekatwakatwa viungo, kutolewa utumbo na kuhifadhiwa kwenye mfuko wa sandarusi kwa ajili ya kupelekwa bar.
Maafisa hao walikuta mkasa huo jirani na bar moja maarufu kwa nyama choma na supu ambapo maafisa hao walituma watu vibarua kufanya usafi katika eneo hilo lililokuwa na nyasi nyingi.
Hata hivyo wahudumu hao waliokuwa wakifyeka, walikuta mfuko huo wa sandarusi ukiwa na nyama ndani ambayo hata hivyo ilikuwa bado inavuja damu kitu ambacho kiliwafanya wawe na hofu huenda ikawa ni mtoto amecharangwa mapanga na kutupwa.
Wahudumu hao waliamua kuwasiliana na maafisa hao wa afya, ambao walifika na kujionea hali halisi ambapo nao walipata fikra kama hizo, hivyo kulazimika kupiga simu polisi kwa ajili ya ufumbuzi zaidi.
Polisi walipofika eneo la tukio, walikuta hali kama hiyo na walipoamua kutoa kitu hicho katika mfuko, awali walidhani kuwa ni nyama ya mbuzi, baada ya kuona nyama iliyochunwa vizuri na kukatwa kwenye magoti.
Lakini ilipotoka ngozi kichwa na miguu mambo yakawa tofauti, hali ya kutayahari ikaiibuka na ukweli kuhusu supu na nyama choma ukabainika. Askari mmoja alisema kumbe tumekuwa tukilishwa nyama za mbwa jamani watu hawana huruma.
Huku afisa afya akilalamika kwa sauti kuu Lahaula. Jamani dunia sasa imefikia hatua mbaya watu wanatulisha nyama za mbwa kulikoni. Hata hivyo nyama hiyo ya mbwa haikuweza kufika sokoni kwani iliharibiwa kwa mafuta ya taa na kufukiwa.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi (Dullonet)umebaini kuwa mbwa waliokuwa wakizurula hovyo mitaani (Maarufu kama Mbwa koko)katika mji wa Tabora, sasa wametoweka na pengine sababu kuu ya kupungua kwao ni kugeuzwa kitoweo katika bar maarufu na zile za mitaani.
Hii ni habari mbaya kwa wakazi wa Tabora, ambao sasa watalazimika kuchunguza kwanza kabla ya kuvamia supu na nyama choma mitaani katika kipindi hiki cha kuelekea Mwaka mpya. Du! Thanks Dullonet…
Hili ni behewa la treni ambalo ni maalum hapa Japani ambalo limetengwa kwa ajili ya wanawake tu katika nyakati fulani fulani hasa inapokuwa kuna misongamano....asubuhi, usiku na siku za sikukuu..
Jioniy ya jana wakati ambapo ilikuwa ruhsa ya kupanda humo watu wote bila kujali jinsia zao..ndipo nikakutana na familia moja ...Mtoto wa kike wa kizungu wa miaka saba hivi alimuuliza mama yake "Kwanini wanawake tu...kwanini baba haruhusiwi kupanda humu"?.
Wazazi wake walitumia muda mrefu kufafanua ...na mara kadhaa alikuwa akirudia swali lake ...kwanini baba na kaka(mdogo wake wa kiume aliyekuwepo) asipande?. Nadhani alielewa...nilifurahia mjadala ule , hususan udadisi wa watoto.
Wadau katika maadhimisho ya miaka 49 uhuru wa Tanganyika hapa Japani; (L-R) Mwombeki Jn, Katibu Mkuu TANZANITE, Fresh Jumbe Mkuu wa TANZANITE Band, Kamarade Jonas Songora .....
Kutoka kushoto, Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya watanzania nchini Japani-TANZANITE bw.Njenga , Bi . Maryam almaarufu, na Mdau Jumbe Bagilo...
DR Congo side TP Mazembe failed in their attempt to win the Club World Cup on Saturday after a 3-0 defeat at the hands of Inter Milan in final.
Goals from Goran Pandev and Samuel Eto'o and a late strike by substitute Jonathan Biabiany sealed the win. The win was Inter's third world title after they won the former Intercontinental Cup in 1964 and 1965.
Mazembe were hoping to become the first African side to win the tournament but the Italians were too strong.
Mazembe had already made history by becoming the first African team to reach the final after a 2-0 upset win over Copa Libertadores champions Internacional of Brazil in the semi-finals, the biggest surprise in the 10-year history of the event.
But wily Inter proved a bridge too far as the experienced Italians struck early and then soaked up what limited and sporadic pressure the African champions were able to produce thereafter. The European champions jumped out to an early 2-0 lead after Cameroon striker Eto'o chipped a pass to forward Goran Pandev who opened the scoring in the 13th minute. Eto'o added the second himself four minutes later when he picked up a loose ball in the area and slotted it home.Mazembe didn't settle into the game until the final 20 minutes, when striker Dioko Kaluyituka had several chances.
However, Inter's Joseph Biabiany put the match away with a goal in the 85th.
Source: BBC
Abuu Semhando , mwanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta amefariki dunia alfajiri ya kuamkia leo akitoka katika shughuli zake za muziki maeneo ya Africana akielekea Mwananyamala , nyumbani kwake. ni huzuni na majonzi kwetu sote. Kazi ya Mungu..
Marehemu Abu Semuhando (Mwenye fulana nyekundu)akiwa katika mazishi ya Dr. Remmy jana ...
DAISO INDUSTRIES CO. LTD ni moja ya makampuni makubwa ya kibiashara nchini Japani yanayouza bidhaa zake kwa bei inayofanana. Kila kitu unachokiona dukani bei yake ni yeni mia moja na yeni tano ya kodi ambayo ni sawa na Shilingi za kitanzania 1,700 hivi. Kampuni hii ina maduka aina ya super market yapatayo 2500 nchini Japani na mengine zaidi ya 550 katika nchi mbalimbali duniani zikiwemo Marekani na ujerumani na nchi nyingi barani Ulaya na duka moja jingine kubwa lipo Ushelisheli barani Afrika. Raisi wa kampuni hii ni Bw. Hirotake Yano ambaye pia ndiye mmiliki wa kampuni hii. Nilibahatika kukutana naye (kama inavyoonekana pichani )katika pilikapilika za hapa na pale, hapa ni ofisini mwake. Ni mtu mkarimu na asiye na makuu.
Baada ya wakenye kusubiri kwa miezi kadhaa hatimaye Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - International Criminal Court (ICC) imetaja majina ya Wakenya sita anaowatuhumu kuhusika kupanga vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu nchini humo mwaka 2007.
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Fedha Uhuru Kenyatta, ni mmoja ya waliotajwa.Waziri wa Elimu aliyesimamishwa William Ruto, Mkuu wa uendeshaji wa Radio Kass FM, Joshua Arap Sang, katibu wa Baraza la Mawaziri Francis Kirimi Muthaura na Mkuu wa zamani wa jeshi la polisi Mohammed Hussein Ali, nao majina yao yametajwa na Bw Ocampo.Polisi nchini Kenya wamewekwa katika hali ya tahadhari iwapo baada ya kutangazwa majina hayo kunaweza kuibuka ghasia mpya.Kila mmoja kati ya hao sita, watatumiwa hati ya kuitwa mahakamani, lakini wakigoma au wakijaribu kuingilia uchunguzi, mathalan kuwatisha mashahidi, Bw Ocampo amesema ataomba kibali cha hati ya kuwakamata.
Katika taarifa yake baada ya tangazo hilo la Bw Ocampo, Rais Mwai Kibaki amesema ana matumaini mahakama hiyo ya kimataifa, mchakato wake utatimiza wajibu wake kwa maslahi ya taifa la Kenya.Amewahakikishia Wakenya kwamba serikali imeimarisha ulinzi nchi nzima.
Jumla ya wattu 1200 walikufa katika ghasia hizo...
Mwanamuziki Dr.Remmy Ongara amefariki dunia alfajiri ya kuamkia leo nyumbani kwake Sinza jijini Dar .Katika siku za karibuni alilazwa hospitalini akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi. Tayari mwili wa marehemu Remmy Ongara umeshapelekwa hospitali ya Muhimbili kuhifadhiwa ukisubiri taratibu za mazishi. Mungu aiweke roho ya Marehemu ongara peponi …amin.
Hebu tuangalie historia yake kwa kifupi yamwanamuziki huyu ambaye alijitengenezea umaaufu mkubwa katika uhai wake.
Ramadhani Mtoro Ongala alizaliwa mwaka 1947 Jamuhuri ya kidemokrasi ya kongo ?DRC eeo la kivu kaskazini, wakati huo ikijulikana kama Kongo Zaire. Baada ya kuzaliwa familia yake ilihamia Kisangani. Mzee Mtoro Ongara , baba yake Remmy alikuwa mpiga ngoma na mwimbaji na pia alikuwaakipenda sana kucheza mpira.
Ipo habari kwamba kabla ya kuzaliwa kwake mama yake alipata ujauzito mara mbili lakini kwa bahati mbaya kila mara mtoto alifariki. Alipopata ujauzito mara ya tatu alienda kwa mganga wa kienyeji kumuomba ushauri afanye nini ili mtoto atakayezaliwa asiiage dunia pia. Bila kusita mganga wa kienyeji akampa ushauri wake. Akamwambia kwanza asiende kujifungulia hospitali bali akajifungulie maporini. Pia alipewa ushauri kwamba mtoto akishazaliwa asije akamkata nywele zake. Yote hayo yalitendeka na ndio kisa cha Remmy Ongala kutokata nywele zake kwa muda mrefu sana.
Kwa bahati mbaya baba yake huyo alifariki dunia na kumuacha Remmy akiwa na miaka sita tu akiwa tayari ameshaanza shule. Lakini kutokana na ukosefu wa fedha na kwa sababu mama yake hakuweza kuendelea kumlipia shule, Remmy ilibidi aache shule.
Ilipofika miaka ya 60, Remmy tayari alikuwa ameshajifunza mwenyewe kupiga gitaa. Mwaka 1964 ulikuwa sio mwaka mzuri kwa Remmy kwani mama yake mzazi alifariki dunia jambo ambalo lilimuacha Remmy na mzigo wa kuwalea wadogo zake kwani yeye sasa ndio alikuwa mkuu wa familia.
Mwaka 1978 Remmy aliingia jijini Dar-es-salaam baada ya kuitwa na mjomba wake ili aje ajiunge na bendi maarufu ya wakati huo,Orchestra Makassy, iliyokuwa chini ya uongozi wa mjomba wake huyo, Mzee Makassy. Huo ndio ukawa mwanzo wa maisha ya Remmy nchini Tanzania. Akiwa na bendi ya Orchestra Makassy, aliandika wimbo wake wa kwanza uliojulikana kama “Siku ya Kufa”, wimbo ambao aliuandika kumkumbuka rafiki yake aliyefariki. Wimbo huo ulianza kumpatia umaarufu.
Alidumu na bendi ya Ochestra Makassy kwa kama miaka mitatu hivi kabla ya mwaka 1981 kuhamia katika bendi ya Orchestre Super Matimila iliyokuwa ndio inaanza kuchipukia miaka hiyo. Hiyo ilifuatia Mzee Makassy kuhamishia bendi yake nchini Kenya. Jina la bendi hiyo, Matimila, lilitokana na jina la kijiji kimoja kilichoko kusini mwa Tanzania. Baada ya kujiunga kwa Remmy, bendi ya Matimila ilijiongezea umaarufu katika anga za muziki nchini Tanzania wakati huo.
Miaka iliyofuatia ilishuhudia umaarufu wa Remmy ukiongezeka hususani kutokana na mashairi ya nyimbo zake ambayo yaliegemea katika kuzungumzia mambo halisi ya kijamii kama vile umasikini, siasa nk.
Pamoja na yote hayo, miaka michache iliyopita Dr.Remmy Ongala aliamua kuachana na muziki wa dansi kwa madai ya kwamba umejaa mambo mengi ya kishetani. Remmy akaokoka, akatubudu dhambi zake na hivi sasa anamuimbia bwana. Mapema mwaka huu alikuwa mbioni kukamilisha albamu yake ya pili. Bado anaishi Sinza (Kwa Remmy) mahali ambapo panaitwa hivyo kwa heshima yake.(Habari kwa msaada wa mitandao mbalimbali)
Watanzania wanaoishi nchini Japani , wakati huu ndio wanaondoka kutoka kwenye ukumbi wa PPP karibu na kituo cha treni cha Sagamino uliopo mkoa wa Kanagawa nchini Japani walipokuwa wamejumuika kusherehea miaka 49 ya uhuru wa taifa lao la Tanganyika na baadaye Tanzania ... Mgeni wa heshima alikuwa Mh. Salome Sijaona , Balozi wa Tanzania hapa Japani.
Meza Kuu; pichani katikati Mh. Salome Sijaona , Kulia kwake Mumewe Bw.Sijaona na kushoto kwake , Dr. Ally Simba mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi Japani.Na kulia kabisa ni Katibu Mkuu Tanzanite Mwombeji jr.
Ulikuwa mchanganyiko wa Muziki wa dansi ulioporomoshwa na Fresh Jumbe Mkuu na Bendi yake ya TANZANITE na Disco chini ya DJ Pembe. Chakula , hotuba na uzinduzi wa tovuti ya Jumuia ya watanzania hapa Japani, Tanzanite society.Balozi Salome katika hotuba yake alikumbusha kuwa watanzania walio nje wana wajibu wa kutoa mchango wao wa kulijenga taifa lao, na wasiishi kwa kujisahau, kwani maendeleo yanaletwa na watu wenyewe. Alihimiza umoja baina ya Watz waliopo Japani na kuwakumbusha wajibu wao wa kufanya kazi kwa bidii kama wanavyofanya wajapani wenywe pamoja na utajiri walio nao.
Baadaye Mwenyekiti wa Tanzanite Dr. Ally Simba aliwahimiza watanzania ambao hawajajiunga na Jumuia hiyo wafanye hivyo kwani Umoja ni nguvu , utengano ni udhaifu. Ulifuata muziki, chakula na vicheko kila upande. Fuatilia tukio hilo kwa njia ya picha.
Muziki wa nyumbani kutoka kwa mtoto wa nyumbani , fresh Jumbe Mkuu.Ulikuwa muziki wa kuchangamsha , kundi zima lililosheheni wanamuziki wenye majina lilitumbuiza , fuatilia taratibu...
Endelea tu...
Safi kila mtu alifurahia siku hii , hongereni kamati ya maandalizi...picha nyingine zaidi zitafuata.....