Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, December 31, 2011

Mwandishi mkongwe wa BBC Johnn Ngahyoma aliyefariki dunia jana Ijumaa asubuhi baada ya vita virefu na kansa ya ini anatarajiwa kuzikwa leo jumamosi katika makaburi ya Kinondoni siku ya Jumamosi .

Taarifa kutoka kwa kaka yake marehemu Bw. Ngalimecha Ngahyoma zimethibitisha hivyo.
Mpaka alipofariki dunia John alikuwa akifanya kazi na shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, mjini Dar es salaam.John alifanya kazi pia huko Daily News, baadaye alijiunga na ITV/Radio One halafu pia alifanya kazi na shirika la NSSF na baadaye alijiunga na BBC.Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pahala pema peponi. Amen.

Posted by BM. on Saturday, December 31, 2011

Zamani ikijulikana kama kisukari kisichotokana na upungufu wa INSULINI (non-insulin-dependent diabetes mellitus (NIDDM) au kisukari kitokanacho na umri na mfumo wa maisha, hasa ulaji na unywaji na ukosefu wa mazoezi (adult-onset diabetes)
Aina hii ya kisukari ni rahisi kuondokana navyo, japo inahitaji elimu na uvumilivu kuhusu aina gani ya chakula na kinywaji mtu anapaswa kula na kunywa bila kusahau umuhimu wa mazoezi angalau dakika zipatazo 30 kwa siku.
Siku za karibuni kumekuwa na vifo vingi vinavyochangiwa na maisha ya kiselule (Sedentary lifestyle ) yaani kula na kunywa chochote kile bila ya mazoezi, MKAZO ( STRESS), unyogovu (Depression). Ushauri wa kitabibu unatuambia kuwa kula kiwango kidogo cha chakula sahihi kila baada ya masaa manne ni tiba ya aina hii ya kisukari. Watu wengi hasa waliopo kwenye tabaka la juu yaani wenye fedha wemekuwa wakihangaika kutafuta wachawi wa afya zao bila kujua kuwa ulaji unaopitiliza bila ya kujua madhara yake ndiyo MCHAWI namba MOJA

Utanachotakiwa kufanya, kama utapenda afya yako iimarike, achana vitu vyakula aina ya wanga, mfano wali mweupe n.k , punguza matumizi ya chumvi, ulaji mikate aina nyeupe, unywaji pombe na ulaji wa matunda yenye sukari nyingi. Japo inaonekana ni adhabu kidogo lakini kama utazingatia basi ujue kuwa utaangamiza kabisa aina hii ya kisukari.Matumizi ya vyakula vilivyotajwa hapo pamoja na kula kiwango kibwa cha chakula na muda mrefu kupita kiasi baada ya mlo hadi mlo, hufanya sukari kupanda na kushuka ( BLOOD SUGAR FLUCTUATIONS), na zaidi kuongezeka kwa uzito, kitambi na mwishowe kuishia kwenye msukumo mkubwa wa damu ( HIGH BLOOD PRESSURE) na hata mashambulizi ya moyo ( HEART ATTACK).
N.B: Vyakula vinavyoshauriwa ni kama vile wali wa kahawia ( BROWN RICE), Mkate kahawia ( Brown bread) , njegere, karoti, samaki na nyama aina zote ni safi. Bila kusau kunywa maji angalau lita mbili kwa siku.Kwa hisani kubwa ya blog ya sauti ya mnyonge...thanks bro Melkiory..

Posted by BM. on Friday, December 30, 2011

Nilisikia nikasita kuamini. Baada ya muda habari zikasambaa mitandaoni, nikaanza kuamini. Sasa nimeamini kuwa da yangu Halima Mchuka amefariki dunia. Halima Mchuka ni dada yangu halisi kiukoo, na sote tulilijua hilo, hivyo tulielewana kama ndugu wawili . Kwa upande mwingine alikuwa mfanyakazi mwenzangu na mpendwa wote. Watu wa rika lake na marika mengine walimkubali na kumpenda. Mungu amemchukua na kazi ya Mungu haina makosa. Mungu aiweke roho ya dada halima, peponi ...amin.
Alipolazwa mara ya kwanza mara baada ya kupatwa na matatizo la kiharusi , wengi walikwenda kumjulia hali hospitalini..ikiwa ni pamoja na Raisi JK na mkewe(Pichani).

Picha ya Chini ; Halima mchuka enzi ya uhai wake..akiwa na watangazaji wenzake Kuanzia kushoto Irene Bongi, nyuma kidogo Aisha Dachi na kulia mtangazaji mkongwe Edda Sanga.

Posted by BM. on Thursday, December 29, 2011

Posted by BM. on Sunday, December 25, 2011


Posted by BM. on Sunday, December 25, 2011

Posted by BM. on Sunday, December 25, 2011

Posted by BM. on Friday, December 16, 2011

Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja amebakia na uhai wake baada ya kurushwa kwa makusudi kutoka ghorofa ya 10 na baba yake katika eneo la viunga vya jiji la Tokyo jana alhamisi.Tukio hilo limetokea saa tatu asubuhi hiyo jana huko Kiba na polisi wamemkamata kijana mmoja mwenye miaka 37 ambaye ni baba wa mtoto huyo kwa kumuhusisjha na tukio hilo baya la kikatili. Baba huyo alijitaja jina lake mbele ya waandishi wa habari kuwa ni Shingo Hashimoto.
Alinukuliwa akisema na kunukuliwa na Shirika la Kyodo News la hapa Japani kuwa “Nilijaribu kumuua mtoto wangu wa kiume , nilimkaba kwa mikono yangu na kisha nikamrusha chini, kutoka dirisha la chumba ninacholala
Polisi wamesema kuwa kijana huyo alikutwa na majeraha machache usoni nay eye mwenyewe Hashimoto ndiye aliyewaita polisi baada ya kufanya tukio hilo. Familia ya Hashimoto iliwaambia Polisi kuwa , mtoto wao alikuwa na msongo wa mawazo kutokana na kukosa ajira. Kijana huyo alikuwa akiishi yeye na mtoto wake huyo wa kiume baada ya mkewe mwenye miaka 38 na mtoto wake mwingine wa miaka minne kwenda matembezini. Bado jiihada za kuokoa maisha yake zinaendelea.

Posted by BM. on Friday, December 16, 2011

Makundi ya haki za binaadamu nchini Bangladesh yamekuwa yakichagiza kutolewa kwa adhabu kali kwa mume wa binti mmoja nchini humo anayedaiwa kuvikata vidole vya mkewe vya mkono wa kulia.Polisi wamesema kuwa Rafiqul Islam,(Pichani) mwenye miaka 30 alimfanyia kitendo hicho mkewe kwasababu alikuwa amejiandikisha kuendelea na masomo ya juu bila ya kupata ruhsa ya mumuwe huyo.
Wamesema kuwa Mtuhumiwa Islam (Picha ya chini) , mfanyakazi mhamiaji alikiri kufanya kitendo hicho mara tu aliporejea kutoka uarabuni.Hata hivyo hakuna ushahidi ulio wazi juu ya kuhusika kwake na polisi wanasema kuwa Islam anayefanya kazi katika Shirika la ndege la Emirates alimfanyia unyama mke wake huyo anayeitwa Hawa Akther Jui, mwenye miaka 21 , akamfunga midomo yake kwa matambara na kisha kuvikata kabisa vidole vyake vitano.Kwa mujibu wa taarifa ilichopishwa kwenye mtandao wa BBC (http://www.bbc.co.uk/news/world-asia-16201961 ) madaktari wamesema kuwa madaktari wamesema kuwa hawawezi tena kuvirejesha vidole hivyo na kwa maana hiyo binti huyo ataishi bila kuwa na vidole vitano vya mkono kwa maisha yake yote.
Narsingdi aliiambia BBC kuwa “ baada ya kurejea hapa Bangladesh alitaka kufanya mazungumzo na mimi lakini ghafla akafunga matambara machoni na kunibana vidole vyangu, akaniziba mdomo na kusema anataka kunipa zawadi nzuri ya kupendeza , lakini badala yae alinikata vidole vyangu”. Binti huyo anasema kuwa mume wake si mtu aliyeelimika vyema na ndio maana hakutka yeye ajiunga na masomo. Kwasasa amekata shauri la kuachana kabisa na mume wake.

Posted by BM. on Friday, December 16, 2011

Posted by BM. on Thursday, December 15, 2011

Posted by BM. on Tuesday, December 13, 2011

Mwandishi wa habari maarufu nchini Kenya wa habari za uchunguzi apata jiko. Hongera bro!

Posted by BM. on Tuesday, December 13, 2011

Moja ya mabasi 20 ya kitalii yanalojulikana kama SKY DUCK la kiamfibia ambalo linaweza kusafiri majini na katika nchi kavu.Tarehe 14 mwezi Novemba lilifanya majaribio jijini Tokyo na kuvutia watu wengi sana.
Nyuma la basi hili kun propera na bila shaka itakujulisha kuwa hili si la kawaida. Likiwa majini linakwenda mwendo wa kilometa 11 kwa sasa lakini nchi kavu linaswaga mwenda kama kawaida. Watalaamu waliobuni basi hili wamekuwa na dhana na maisha ya bata anayeweza kuishi majini na nchi kavu. Basi hili limetengenezwa kwa gharama kubwa sana unaweza kupiga hesabu. Kama uko Tanzania hebu piga hesabu (Yeni Millioni 80 x20) utapata fedha za kitanzania ni kama Tsh. 1,600,000,000 . Kwa kawaida basi jipya lisilo la namna hii linagharimu Yeni Yeni million 30.Basi hilo lina magurudumu manne linayoyatumia kusafiri barabarani

Posted by BM. on Tuesday, December 13, 2011

Jumamosi ya tarehe 17 DISEMBA 2011 kutafanyika hafla kubwa nay a kupendeza katika Hoteli ya PAN PACIFIC iliyopo jijini YOKOHAMA hapa Japani kuanzia saa 11.00 JIONI HADI SAA 2.00 USIKU kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara. Ifuatayo ni taarifa kamili ya Mwenyekiti wa Jumuia ya Watanzania wanaoishi hapa JAPANI-TANZANITE Bw. Rashidi Njenga kuhusiana na hafla hiyo.
“Ndugu Watanzania wenzangu, Naomba nichukue nafasi hii kuwaarifu kuwa maandalizi ya tafrija yetu yanaelekea kukamilika. Kufikia leo idadi ya watu waliojiandikisha imefikia 94, kati ya waliojiandikisha watu 60 wamethibitisha kuhudhuria. Tumepata muitikio mzuri kwa Wajapan waliowahi kuishi Tanzania, au wenye interest na Tanzania baadhi yao watahudhuria. Tutakuwa na DJ ambaye ana vyombo maalum vya Disco na atatupigia mchanganyiko wa nyimbo nyingi kutoka BENDI mbali mbali za nyumbani. Chakula na Vinywaji vya aina vyingi vitakuwapo. Vyote vimejumuishwa kwenye mchango utakaoutoa. Mheshimiwa Balozi Mama Sijaona ndiye atakayekuwa mgeni rasmi.
STESHENI: 1. MINATOMIRAI (Minatomirai Line + Toyoko line)
2. SAKURAGICHO (Keihin Tohoku)
 TAFADHALI FIKA SAA 11.00 KAMILI (5:00pm). FIKA KWA WAKATI.
Kwa kuwa tunatakiwa kuthibitisha namba ya watakaohudhuria mapema ili watu wa hoteli wafanye maandalizi yao. Tunawaomba wote ambao wamejiandikisha kuhakikisha wanatoa michango yao kufikia JUMATANO JIONI. Tunawaomba wale ambao hawajathibitisha wafanye hivyo na kulipa michango yao. Wenzetu ambao hawajajiandikisha tunawaomba wajiandikishe na kulipa michango yao. Wanachuo/ wanafunzi Yen3,000 kila mmoja. Watu wa kawaida Yen 3,000 - 5,000 na kuendelea. Unaruhusiwa kuchanga zaidi.
Michango inaendelea kupokelewa hadi JUMATANO TAREHE 14 DISEMBA 2011. Wale wote ambao watachagua kulipia mlangoni siku ya sherehe watatakiwa kulipa Yen 9,000 au zaidi KWA MTU MMOJA – HAKUTAKUWA NA UPUNGUFU/ UNAFUU. Ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza tunaomba kila mmoja ajiandikishe, atoe mchango wake kabla au kufikia mstari-mfu. Mlangoni kutakuwa na walinzi ambao hawatazungumza lugha nyingine zaidi ya kupokea pesa. Unaweza kubofya hapo kwa taarifa za ziada kuhusiana na mahali patakapofanyika hafla hiyo..
(http://pphy.co.jp/).

NJENGA, R MBA
Mwenyekiti, Kamati ya Maandalizi.

Posted by BM. on Sunday, December 11, 2011

Bila shaka ni siku muhimu sana kwa Bi. Julia Mlwilo , ambaye leo J2, kwa mara ya kwanza ameanza kutangaza kupitia Idhaa ya kiswahili ya Redio japani-NHK WORLD. Mara tu baada ya kumaliza taarifa ya habari , taswira hiyo ikapatikana.
Picha ya Chini akiwa katika Chumba cha habari na watangazaji wenzake , Fatma Mohamed na Jonas Songora...Take 5, Julie , karibu katika fani...

Posted by BM. on Friday, December 09, 2011

Mbwa mwenye umri mkubwa zaidi ulimwenguni kulingana na rekodi zilizopo katika kumbukumbu za ‘Guinness World Records ‘ amekufa nchini Japani akiwa na umri wa miaka 26 na miezi nane.
Mmliki wake Bi. Yumiko Shinohara aliwaambia waandishi wa habari nyumbani kwake huko Sakura , jiji lililopo nje kidogo ya Tokyo kuwa mbwa huyo aliyekuwa akiitwa Pusuke ikiwa ni mchanganyiko wa mwenye manyoya mengi laini mchanganyiko alikufa siku ya jumatatu iliyopita baada ya kuugua ghafla na kuanza kukataa kula.
Shinohara alikiambia kituo cha Televisheni cha mtandao wa FNN hapa apani kuwa anashukuru na kufarijika kwa mbwa wake kuishi kipindi kirefu hicho. Wataalamu wanasema kuwa kipindi cha kuishi mbwa kwa miaka 26 ni sawa na miaka 125 kwa binaadamu.
Kulingana na rekodi za Guinness, mbwa Pusuke huyo alizaliwa tarehe 1, mwezi April 1, 1985 na kutambuliwa kuwa ni mbwa mzee kuliko wengine mwezi desemba mwaka uliopita. Umri wa juu kabisa wa maisha ya mbwa uliwekwa na mbwa Bluey aliyeishi miaka 29 nchini Australia ambaye alikufa mwaka 1939.

Posted by BM. on Thursday, December 01, 2011

Ndege ya Shirika la ndege la Japani ANA iliyokuwa isafiri kutoka Jiji la Fukuoka kwenda Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Haneda hapa Japani ililazimika kuacha safari yake jana Jumatano baada ya kiwango cha pombe kwenye damu ya rubani kuoneyesha kuwa kilikuwa cha juu kuliko kile kinachovumilika. Taarifa zilizotangazwa na Shirika la Utangazaji la Japani na kunukuliwa na mtandao wa http://www.japantoday.com zimebainisha kuwa ndege hiyo 246 ilikuwa iondoke Fukuoka saa mbili na nusu asubuhi , ilisitisha safari yake baada ya rubani wake msaidizi mwenye umri wa miaka 55 kuchukuliwa vipimo vya pumzi yake saa moja na nusu kabla ya kuanza safari. Viwango hivi vya pombe pia vinawahusu madereva kote nchini Japani ambapo kiwango kinachokubalika hakitakiwi kuzidi 0.15 mg/L.
Kutokana na kusitishwa kwa safari hiyo abiria wapato 240 walichelewa kwa dakika 40 na baadaye kuanza safari.
Shirika la ndege la ANA limesema kuwa rubani na msaidizi wake walikuwa wakipata kinywaji pamoja wakati wa asubuhi siku ya safari hadi kufikia saa 10 na nusu alfajiri . Inaelezwa kuwa walikunywa glasi sitaza pombe ya kijapani inayoitwa “shochu.” Msemaji wa Shirika hilo amesema kuwa ANA inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.