Seif Shaaban ...
Baada ya kumsikiliza kwa makini mwanamuziki huyu wa kizazi kipya ,sikiliza kazi yake inayoonyesha kipaji chake ...Baada ya kusikiliza nambie umepata ujumbe gani..
USIENDE!....
Ni hapa...
Picha ya kukumbukwa; Raisi Jakaya kikwete alipokuwa akizitembelea nyumba za wapigakura wake wa ki- Wahadzabe Mwaka mmoja na nusu uliopita. Kabila hilo linaishi msituni huku wakitegemea chakula kinachotokana na matunda ya porini pamoja na mizizi,
Rais aliagiza wanafunzi wa Kihadzabe ambao wanamaliza shule ya msingi wakifaulu, wapelekwe katika shule za sehemu nyingine ili waweze kuchanganyika na watu wengine.
“Hawa tukiwaacha waendelee kusoma wao peke yao hawawezi kujua kama kuna watu wengine humu duniani…mimi wakati nasoma pale Msoga kisha nikapelekwa Lugoba nilikuwa najua dunia hii ni ya Wakwere tu, lakini nilipoenda Kibaha Sekondari nikaona kumbe pia kuna watu wa kabila nyingine.Alisema JK...Picha na Maelezo
Raisi wa Afrika kusini Jacob Zuma akiwasili katika eneo lililofanyika sherehe ya harusi ya kijadi ili kumuoa Bi. Tobeka Madiba kama mke wake wa tano katika kijiji cha Nkandla kaskazini ya kwazulu Natal na hiyo ilikuwa juzi J3, January 4, 2010. Zuma mwenye miaka 68 amemuoa mwenye miaka 37 kutokana na mila za Wazulu.Tobeka alikuwa naye kwa kipindi kirefu lakini sasa amehalalisha ndoa yake kimila. Hii ni ndoa ya tano . Japo kwa sasa ana wake watatu. Mke mmoja aliwahi kumtaliki siku za nyuma na mke mwingine alikufa. Wageni 2000 walihudhuria japo waandishi wa habari walikataliwa. Unasemaje…Inapendeza au!…Jambo linalowavutia watu ni jinsi Rais Zuma anavyochangamkia hobi yake ya kucheza kwa umahiri Mkubwa . Unaweza kuangalia video hiyo hapo chini kabla ya kuwaona kwa karibu wake zake watatu.
Katikati ya burudani...
Katikati ya sherehe ya harusi akiwa na Bi harusi...
Wake watatu wa Mh.Zuma.Wa mwisho kushoto ndiye aliyeolewa juziwakiwa na mume wao..
Kituo kikuu cha mabasi ya Express kiitwacho SAHARA..Maarufu katika jiji la mwanza ...Upo?
Aah inapendeza; Makutano ya Mtaa wa Kenyatta na station Road ...kweli...
Tangazo la dhahabu nyeupe mpaka skuli...watani zangu bwana!
Almaaruf Mtaa wa Rwegasore, MWZ.
Kama unaifahamu Mwanza kwa sanaaa utakuwa umefika hapa!
Uwanja wa Ndege wa kwetu...soma hapo juu ya bati kuna jibu...
Shughuli ni watu...Wadau wa habari Jijini Mwanza; Raphael Shiratu (L)Afisa mwandamizi Sahara communication Mwanza na John Dotto mwandishi wa gazeti la Mwananchi, wakiwa katika mjadala muhimu wa kitaifa.
Mapaparazi waandamizi mkoa wa Mwanza katika picha ya pamoja...Mkono huo, Kheri ya mwaka mpya makomred!
Mdau Malkiory Matiya kushoto hapo muda mfupi baada ya kukabidhiwa nondo zake(M.Sc in Public Health) katika Chuo Kikuu cha Tampere, Finland . Wenzake hapo ni katikati M-Nigeria( Bioinformatics) na M-Cameroon( Bioinformatics). Badala ya joho huko ufini graduation husherekewa kwa suti nyeusi, ua na wine nyepesi.Take five Bro...Nje ya jengo la Sherehe kukoje...Kibaridi!
Barafu inadondoka...hiki kibaridi lawama!Thanx Matiya.
MAZISHI ya Simba wa vita Mzee Rashid Mfaume Kawawa yanatarajiwa kufanyika leo kuanzia majira ya saa 7 adhuhurihuko nyumbani kwake Madale Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Marehemu Kawawa alifariki jana, majira ya saa 3:20 za asubuhi, katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako juzi alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kuangalia afya yake.Akiongea na waandishi wa habari kwa huzuni Ikulu, Raisi Kikwete alisema Mzee Kawawa alifika hospitalini hapo juzi kwa ajili ya kwenda kupima malaria kwa kuwa alikuwa na safari na alienda hapo ili aweze kujitambua kama angekuwa na malaria ajitibie kabla ya kwenda safari yake hiyo.Alisema alipofika hospitalini hapo alipima malaria na kukutwa kuwa hakuwa nayo, na alianza safari ya kurudi nyumbani kwake, kabla hajafika nyumbani kwake hali ilibadilika na waliongozana nae walimrudisha hospitalini hapo na jopo la madaktari walianza kumpima kutambua alikuwa akisumbuliwa na nini. Katika vipimo vya haraka haraka madaktari hao waligundua kuwa sukari yake ilikuwa imeshuka sana na kufikia 0.6 hali ambayo iliwafanya madaktari wafanye jitihada kubwa kumshughulikia kurudisha hali yake ikae sawa. Mbali na kumshughulikia sukari, pia waliweza kugundua kuwa vigo zote mbili zilikuwa hazifanyi kazi na pamoja na jitihada zote mwenyezi mungu alichukua uamuzi wa kumchukua majira hayo. Mwili wa Mzee kawawa unaingizwa Karimjee
ktika ukumbi wa karimjee
Viongozi wakuu wa kitaifa walikuwepo Karimjee Hall.Mapema Raisi jakaya kikwete alisema kuwa taifa limempoteza kiongozi shupavu aliyepigania uhuru wa Tanganyika na alikuwa ni kiongozi mshauri wa karibu wa taifa enzi za uhai wake.Marehemu aliweza kushika nyadhifa nyingi enzi za uhai wake kama vile Makamu wa Kwanza wa Rais, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na vyeo vingine kadhaa.Marehemu Kawawa alizaliwa mkoani Ruvuma Wilaya na Namtumbo, Februari 27, mwaka 1926. Alifariki jana akiwa na umri wa miaka 83.(Picha na M.Michuzi na Full Shangwe)
Mzee Rashidi Mfaume Kawawa katikati akisalimiana na Raisi Jakaya Kikwete amefariki dunia asubuhi katika hospitali ya Muhimbili katika chumba cha wagonjwa mahututi. Kulia ni mke wa Marehemu kawawa. Kwa kifupi; Mzee Rashidi Mfaume Kawawa alizaliwa tarehe 27 February, 1926 katika kijiji cha Matepwende, Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Tanzania. Alianza elimu ya msingi huko Liwale, Lindi mnamo 1941 - 1942 na kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya skondari Dar es salaam,. Huyu ni mwanasiasa mwenye historia ndefu lakini itoshe kusema tu kwamba kuanzia tarehe 22 Januari, 1962 hadi tarehe 13 Februari, 1977 alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Alifuatwa na Edward Sokoine. Baadaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. Raisi Jakaya Kikwete akilihutubia taifa mchana wa leo wakati akitangaza kifo cha Mzee rashidi Mfaume Kawawa . Taifa litakuwa kwenye maombolezo kwa siku saba ambapo bendera zitapepea nusu mlingoni. Mungu ailaze roho ya Mzee Kawawa peponi Amin.
Nyumbani kwa Mzee Kawawa Madale, Dar es salaam.
!
Kuna ubaya gani tukapiga kigelegele kuukaribisha mwaka mpya?...Happy New year!
St. Augustine University-Mwanza tawi la Mtwara ...upo hapo?
Bandari ya Ntwara kutoka Juu.
Soko kuu la Mkoa wa Mtwara!
Nyanya Zimeingia sokoni Ntwara!
Kazi niliyotumwa na taifa huku Ntwara imemalizika sasa narejea Mwanza...5 Mgosss!
Precision Air ikijiandaa kuruka NTWARA Int. Airport. Mwandishi wa habari Peter Omari akiwa ndani yake baada ya kumaliza majukumu.<



