Ni hapa...
Wananchi wa Ludewa ambao ni wateja wa benki ya NMB tawi la Ludewa wametinga nyumba kwa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wakitaka awasaidie kuishtaki benki hiyo kwa madai ya upotevu wa fedha zao katika mazingira tata.
Agnesi Mapunda ni mtumishi wa Halmashauri ya Ludewa idara ya ardhi ambaye ni mteja wa benki hiyo mwenye akanti namba 6012400590 NMB tawi la Ludewa ambaye alidai kuwa akaunti yake ilikuwa na fedha zaidi ya shilingi milioni 1 ila mwezi wa sita alikuta akaunti hiyo ikiwa na salio la shilingi 144,000 pekee na baada ya kuuliza aliambiwa fedha zake zimetolewa kwa huduma ya pesa fasta na NMB Mobel huduma ambayo kwa upande wake hajawahi kuitumia toka awe mteja wa benki hiyo.
Hata hivyo alisema baada ya kuhoji sana ndipo benki hiyo ilipoamua kuchunguza suala hilo na kubaini majina ya watu waliohamisha fedha hizo na kuwa hadi sasa suala hilo lipo polisi linafanyiwa kazi.Huku baadhi ya wateja wakienda benki hapo na polisi kutaka kufunga akanti zao na kuhama uteja na benki hiyo .Walidai kuwa kuna uwezekano wa wafanyakazi wa benki hiyo kukopeshana fedha zao kinyume na utaratibu na baada ya muda kuzirejesha.
Kwani walisema kuwa wakati mwingine baada ya kufika na kulalamika katika benki hiyo na kuambiwa wafiki baada ya siku mbili ama tano wmekuwa wakikuta akaunti zao zinapesa kama walivyoziacha .Mbunge wa jimbo hilo Filikunjombe amekili kupokea malalamiko hayo na kuwa tayari amewasiliana na meneja wa kanda na meneja wa benki hiyo ili kutolea ufafanuzi suala hilo.
Hata hivyo alisema kuwa majibu ambayo ameelezwa na viongozi hao wa kuwa yawezekana fedha hizo zinachnukuliwa na jamaa wa wateja hao ambao wamekuwa wakiwapa namba zao za siri bila kujua ama kwa kujua ama ni kampuni ya simu ambayo inashughulika na huduma hiyo .
Pia alisema kuwa ameshangazwa na ushirikiano mdogo wa wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la Ludewa kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwa wateja wao wenye matatizo hayo kwa kuwataka waende polisi kufikisha malalamiko yao huku wakijua wazi kuwa wateja hao wameingia mkataba na benki ya sio polisi .
Hata hivyo meneja wa NMB tawi la Ludewa alipotafutwa kwa simu alisema kuwa hana mamlaka ya kulizungumzia suala hilo na kuwa uongozi wa juu wa benki hiyo ndio unaweza kuzungumzia suala hilo . Du! Thanx 'Mzee wa Matukio' -Iringa.
Leo ni Eid el Fitri. Jana jumanne waumini wa dini ya kiislamu wa madhehebu ya Answar suna katika eneo la Afrika Mashariki na kwingineko duniani walifanya ibada hiyo ya Eid-el fitri . Na waumini wengine wanaadhimisha siku hiyo hii leo... Eid Mubarak!
Barakat el Eid ndugu, marafiki na jamaa zangu wote kwa sherehe hizi za Eid el fitri. Nakupa mkono wa Eid, tafadhali nikubalie... Hii ni ishara ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Namuomba Mwenyezi Mungu atuzidishie mimi na wewe subra, atupe afya, atupe murua, atujaalie uvumivu , ustahimilivu, hekima , busara na ubinaadamu. Tushikamane kupitia maagizo ya Mwenyezi Mungu na atuwezesha kuachana na mabaya yaliyopita ili tusogeze mbele yaliyo mema. Blogi yako hii ya MIRINDIMO iko pamoja nawe katika hatua zote hizi. Tuombeane mema ,Inshallah.BM
(Picha mbili hapo chini ) zinawaonyesha baadhi ya waumini wa madhhab ya Answar suna wakiwa katika ibada ya Eid El-fitri jana Jumanne asubuhi katika viwanja vya Jangwani Dar es salaam. Shekhe aliyeiongoza ibada hiyo, Shekhe Juma Poli Amri akitoa mawaidha. Madhehebu mengine wataswali swala ya eid Fitri leo jumatano ...Inshallah
Bado hali ya kutatanisha imetanda nchini Libya hasa kufuatia kauli ya mkuu wa Baraza la mpito la taifa (NTC) Mustafa Abdul Jalil kuwa majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya, Nato, na washirika wengine lazima waendelee kuwaunga mkono waasi dhidi ya 'mtawala wa mabavu.' kwani bado Muammar QWadhafi ni tishio japo hajulikani alipo.Waasi wanasema wako katika mazungumzo na viongozi wa kikabila wa Sirte ili kuzuia umwagikaji damu, lakini mpaka sasa hawajafanikiwa.Lakini huyu Qadhafi ni nani hasa ...fuatilia makala hii..
Historia ya kisiasa ya kiongozi huyo wa Libya inaanzia mwaka 1942 . Huyu ni mto wa mkulima-bedui aliyekuwa akihama hama . Qaddafi alizaliwa katika Jangwa la Libya katika hema na akiwa kijana mdogo alionekana kuwa mwenye akili sana ambapo alimaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Libya mwaka 1963.
Akiwa safarini ng'ambo, huwa anakaa kwenye kambi iliyojengwa na hema yake ya kifahari ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume. Hema hiyo pia hutumiwa kuwalaki wageni wa Libya na Kanali Gaddafi huendesha mikutano na mahojiano yake humo humo akipepea usinga au tawi la mitende.
Ndoto yake kuwa ilikuwa kuuondoa madarakani utawala wa kifalme wa Mfalme Idris wa wakati huo hivyo alijiunga katika chuo cha kijeshi na kuhitimu mwaka 1965 na akaanza kupanda vyeo jeshini huku ndoto yake ikiwa ile ile ya kukamata nchi siku moja. Tarehe 1, Sept. 1, 1969, Qaddafi alifanikiwa kumpindua mfalme Idris . Na kujitangaza kutwaa madaraka ya kuwa Amiri jeshi Mkuu wa majeshi ya Libya na mkuu wa Baraza kuu la utawala nchini humo.Hatua ya kwanza ilikuwa kuviondoa vikosi vya wamarekani na Uingereza kutoka nchini humo mwaka 1970 na kuendesha sera ya ubinafshaji wa mali ya wageni zilizohusu biashara ya mafuta mwaka 1973.
Kwa watanzania wanamuangalia Kanli Qadhafi kwa sura mbili. Mtu anayewapenda waafrika wenzake na pia mtu aliyewajeruhi wakati wa vita vya Kagera vya mwaka 1979. Kwa sura ya kwanza , amekuwa akizisaidia sana nchi za kiafrika kwa hali na mali kupambana na umasikini na zaidi ya hilo amejenga misikiti mingi sana barani Afrika na hivyo kuwafanya waumini wengi wa kiislamu kupata mahali pazuri pa kuabudia.
Tukiviangalia vita vya Kagera , Kati ya Uganda ya Iddi Amini Dadaa nay a mwalimu Nyerere , Qadhafi alituma vikosi vyake kumsaidia Amini ambavyo vilikuwa na mchanganyiko wa wapiganaji, wanajeshi na wanamgambo lakini hatimaye walikwama kumtikisa mwalimu…
Utawala wa miongo minne wa Qadhafi umefikia mwisho wake… haijulikani hatima ya Libya kwa sasa na nini hasa Afrika imejifunza…wacha tusubiri…
Chama tawala nchini Japani cha Democratic kimemchagua Waziri wa fedha wa hapa Japani Yoshihiko Noda kuwa raisi wake, hali inayoonyesha ishara dhahiri kuwa muda mfupi ujao atashika nafasi ya Waziri Mkuu itakayoachwa na Waziri Mkuu wa sasa Naoto Kan abaye alijiondoa katika wadhifa huo ijumaa iliyopita.
(Naoto Kan Kulia- kushoto Yoshihiko Noda)Ilikuwa patashika kwa wagombea , katika uchaguzi uliofanyika leo Jumatatu, ambapo katika duru ya kwanza ya kujieleza na kupigiwa kura hakuna aliyetoka na ushindi wa mija kwa moja. Katika duru ya kwanza iliwashindanisha wagombea watano Waziri wa Uchumi Banri Kaieda na mh. Noda waliongoza na ikabidi wapigiwe tena kura ambapo Noda alipata kura 215 kati ya 395 huku mwenzake akiambulia kura 177.
Baraza la mawaziri litajiuzulu hivi karibuni na Bunge ndipo litakapomchagua Waziri Mkuu. kama ilivyotarajiwa aliwaambia waandishi wa habari mara tu baada ya kutangaziwa ushindi kuwa anataka kuzidisha kasi yabujenzi wa maeneo yaliyoathirika na tetemeko na tsunami , machi 11 mwaka huu.
Ni kawaida kwa Japani kubadilisha mara kwa viongozi wake wa juu na mabadiliko haya hayawashangazi sana Wajapani ...labda wageni kama akina siye!.Noda anakuwa waziri Mkuu wa Sita katika kipindi cha miaka mitano...
Nikiwa na Raisi wa moja ya makampuni makubwa ya maduka ya vyakula na vifaa vingine nchini Japani (supermarkets) kampuni ya DAISO nilipomtembelea ofisini kwake.. Pamoja na nafasi aliyonao amenionyesha ukarimu sana na kutojikweza na pia anajichanganya na wafanyakazi wake katika kazi za kila siku...Anavaa sare kama wao na kubeba makasha bila shida..imenifurahisha sana hii..'Nawaza nyumbani!'
Kituo cha Sheria na haki za Binaadamu nchini Tanzania LHRC , hivi sasa inaendesha semina kwa waandishi wa habari juu ya masuala ya binaadamu kwa waandishi wa habari mjini Dodoma.Mmoja wa washiriki wa semina hii ni mwandishi wa habari Latifa Ganzel , pichani kushoto, mmoja wa waandishi wanaojituma sana katika kutimiza majukumu yao.
Baada ya semina...majukumu yanaanza ya kusaka habari...katika mazingira yote. paparazi Latifa Ganzel katika bodaboda...take 5 mdau.
Vikosi vya waasi nchini Libya wameshakamata jiji la Tripoli hivi sasa na wanaendelea kumsaka Kanali Muammari Qadhafi. Kwa sasa wanakabiliana na kikosi cha watunguaji ambacho wapiganaji wake wamesambaa jiji zima. Picha ya pili inaonyesha ndani ya mmoja wa watoto wa Qadhafi , Bi aisha...vikosi vya waasi vilifanikiwa kuyateka makazi hayo.
Wafuasi wa vikosi vya waasi wa Libya wakiulaani utawala wa Qadhafi baada ya swala ya ijumaa 26/08.
Mwanamke mmoja nchini Japani mwenye umri wa miaka 65 mwaka huu amejikuta akiiingizwa mjini baada ya kuhamisha mara kadhaa fedha bila kujua , ambapo alihamisha Yeni million 29 (sawa na Tsh. 580 Millioni) kwa mwanamume mmoja asiyefahamika ambaye amejifanya kuwa mwanawe wa kiume.
Polisi wameripoti jumamosi iliyopita kuwa utapeli wa aina hii unaofahamika hapa Japan kama ‘ “ore ore sagi,” ulihusisha mawasiliano kwa njia ya simu na mtu aliyekuwa akiamini kuwa ni mwanawe.Mtu huyo alimwambia huyo ‘mama yake’ kuwa amuhamishie fedha kwenye akaunti yake ili kulipa madeni yanayomkabili na ndipo alipoanza kumwaga pesa.Kulingana na ripoti iliyoonekana kwenye kituo cha televisheni cha Asahi, mama hyo anakaa maeneo ya Suginami na kwamba tukio hilo lilikuwa la June 17. Kwanza aliomba apelekewa Yeni laki sita na baada ya kumkubalia akawa anamuingizia fedha kwa zaidi ya mara 30 na zikafikia Millioni 29 kabla hajakutuka kuwa ameibiwa. Du!
Hii ilitokana na mama huyo kupokea simu ya mtoto wake wa ukweli wiki hii na baada ya kuripoti suala hilo Polisi , ikagundulika kuwa mtu huyo alikuwa akitumia akaunti tofauti za benki kwa kila hamisho moja la pesa.
Shirika la Polisi nchini Japani limetoa ripoti wiki hii inayobainisha kuwa kati ya mwezi Januari na Juni mwaka huu , idadi ya ndoa bandia zilizobainishwa na Polisi zilikuwa 88 ikiwa ni ongezeko la asilimia 49.2 kama hizo zilizofungwa mwaka jana.
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi nyingi za ndoa hizo zimewahusisha raia wa Japani na wengine kutoka China, Ufilipino na raia wachache kutoka mataifa mengine.
Shirika hilo la Polisi nchini Japani limesema kuwa linapanga kufanya kampeni nchi nzima kusukuma jitihada za kuzibaini ndoa bandia, utengenezaji wa pasipoti za bandia , vitendo vya kughushi maarufu Japani kama ‘Alien Card’ pamoja na shighuli za kibenki zinazofanywa chini kwa chini.
Hivi karibuni (1/8-8/8) kulikuwa na maonyesho ya kilimo ya nane nane katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Kwa kanda ya Mashariki yalifanyika mjini Morogoro. Kulikuwa na pilika pilika nyingi uwanjani , mabanda yalikuwa mengi , wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo walijitokeza kwa wingi na raia wa kawaida kama mimi pia tulijitokeza. Kiingilio kilikuwa shilingi elfu moja kwa mtu mmoja. Nilihudhuria kwa siku mbili mfululizo. Nilishuhudia magari mengi yakibaki nje. Nilipouliza kulikoni, waliniambia safari hii viwango vya ada ya magari vilikuwa vikubwa sana. Siku moja kuingiza gari ilikuwa elfu 35 , ingawa kwa wiki ni elfu 50. Nilipata hisia kuwa pesa nyingi ziliachwa nje ya geti…
Mama ntilie nao walikosa biashara , bila shaka mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ulichangia. Lakini msisimko ulibaki ule ule wa miaka yote, hakuna jipya sana. Wakulima wadogo walikodoa tu macho kwenye mashamba ya mfano, lakini walio wengi kilimo chao wanasema hakijabadilika. Lakini ukweli unabaki palepale , kuwa na ujuzi hata kama haujatumika ni hatua kubwa. Nabakia miongoni mwa waliofika ‘8-8’ morogoro mwaka huu.
Nilikuwa likizo fupi..nyumbani Tz. Haikuwa rahisi na isingewezekana kufanya kila kitu ikiwa ni pamoja na kumuona kila aliye na nasaba nami, naomba radhi kwa hilo. Safari hii nilikuwa salama zaidi kwani likizo nzima niliambatana na komandoo wangu. Kabla ya safari alifanya zoezi la nguvu ili kuwa fit. Ambana nasi taratibu kwa njia ya picha...
Safari ilianza...Nilipewa ruhsa ya kupeperusha bendera ya taifa kwa muda..(Asante kwa kutoniuliza) tukaendelea...Tukafika eneo la Mikese, mkoani Morogoro karibu na eneo la 'mizani'. Tukio la saa nane usiku, canter ina-overtake, uso kwa uso na scania la mizigo lilikuwa likitokea Mbeya. Canter inatoka Dar. madereva wawili hapo hapo, abiria wao watatu wafa, wawili wanusurika. Dereva wa scania alibanwa kwa saa tano (Picha ni hapo) . Hadi saa mbili asubuhi magari yakaanza kuondoka . tukio la huzuni. Inaelezwa kuwa ni uzembe...sijui bwana, mashahidi wamekufa. Itoshe tu kuwa kuna kitu uzembe au ajali. safari ikaendelea...
Kilometa chache kutoka eneo ambalo kulitokea ajali tulisimamishwa na polisi wa usalama barabarani akitaka kulikagua gari. Mara akamuita dereva nyuma ya gari ...akamwambia" Gari yenu halina kosa ila hamuwzi kuondoka hivi hivi , lazima muache kitu". Dereva akampa shillingi elfu tatu, jamaa akatia mfukoni. Nikajaribu kuchukua picha tukio hilo nikabahatisha hizi mbili. Ikaniuma sana . imeniuma kuelewa kwamba rushwa imefika pasipo pake. simulizi hii nitaiendeleza siku nyingine. hali ya nyumbani.
Napenda niwataarifu wapenzi na mashabiki wa Mirindimo kuwa nimerejea Tokyo baada ya mapumziko mafupi nyumbani Tanzania.
naomba radhi sana kwa kuwa kimya ...lakini yote yalikuwa na sababu, lakini kubwa nimerejea nikiwa na habari na picha Lukuki za nyumbani. Kuanzia kesho nitaanza kuzipakua...
Kwa ujumla likizo ilikuwa nzuri...na mambo yalienda kama yalivyopangwa. hakikisha kesho unapita hapa uone jipya!