Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, March 30, 2009

Jotty akiwa ndani ya TBC-tv....shurti kwa vidole.....!

Posted by BM. on Monday, March 30, 2009

Hawa jamaa wako smart sana na kazi yao. Ukionja robo kikombe tu ya laga...hakuna msamaha na hata ukipanda gari ambayo dereva wake amekunywa wewe faini ya mamilioni na yeye pia vinginevyo jela. Ole wako usifunge mkanda , au huna leseni . Hakuna rushwa , hakuna kupindisha sheria. Madereva wa Japani wanainyenyekea Sheria na wakifika kwenye zebra wanakuwa na adabu zao . Ukimpigia honi ya kumshitua mtu wakati ni haki yake kupita ...utamlipa. Tanzania Je. Nauliza ingekuwaje siku moja tu Trafiki wa Tanzania nchi nzima wakafuata na kusimamia kanuni zote za usalama barabarani nchi nzima kwa asilimia mia moja ...Faini tu ingetosha kuhudumia wizara ya mambo ya ndani....Thanx willy/wilna.

Posted by BM. on Monday, March 30, 2009

Huna ujanja...

Posted by BM. on Monday, March 30, 2009

Angalia sait mira...!

Posted by BM. on Sunday, March 29, 2009

Hakuna ramani hapo ya kukufikisha mpaka mlangoni ....Ni Ibungilo, maarufu Nyamanoro Jeshini, jijini Mwanza. Upoooo!

Posted by BM. on Sunday, March 29, 2009

Njia ya kwenda Aiport Mwanza ...Nilikaa maeneo hayo wakati fulani ni maarufu ...Uliza tu Kwa SULEIMAN NASSORO..

Posted by BM. on Sunday, March 29, 2009


Faya brigedi MWZ.

Posted by BM. on Saturday, March 28, 2009

Kwenye banda hilo ndipo atakapotoka Raisi wa Tanzania wa baadaye...

Posted by BM. on Saturday, March 28, 2009

Kama ilivyo Ntwala ...ndonya na chale, wenzetu Thailand kuna kabila linaamini mwanamke shingo si unaona springi hizoo! zinaanza kuwekwa toka mtoto anapofika miaka mitatu ...Urembo gharama.

Posted by BM. on Saturday, March 28, 2009

Shiko inaandaliwa.

Posted by BM. on Saturday, March 28, 2009

Tetemeko kubwa limepiga chini ya ardhi km zipatazo 17 katika kisiwa cha Java huko Indonesia karibu na moja ya jiji kubwa nchini humo lenye watu wengi la Yogyakarta

. Palikuwa hapatoshi. Darasa hili ni kwa wasomaji wa Blog hii wanaoishi katika maeneo ya matetemeko hususan nchini Japani.
Hii ni nchi yenye matetemeko mengi, ikiwa wewe unakaa Japani lazima uwe na taarifa juu ya nini cha kufanya pindi balaa hilo likitokea. Kwanza , usitaharuki sana. Mtangulize Mungu na kuwa mtulivu. Kama huna dini endelea na hatua inayofuata. Ukiwa nyumbani hatua ya kwanza kimbilia chini ya Meza ambayo si ya kuunga unga . Maana nyingine zinagawanyika. Usimsahau mumeo , mkeo ,watoto ama mpenzio hakikisha unakuwa naye wakati huu wa taharuki.
Kuna maadalizi ya mapema kabisa. Jiandae kuwa na begi la huduma ya kwanza. Weka dawa ndogo ndogo za maumivu, maji ,tochibetri, Radio ndogo mishumaa, kibiriti na vyakula vya makopo.Lazima ujue kwa hakika nyaraka zako muhimu umeziweka wapi kama vile passport, kitambulisho chako, simu ya mkononi na fedha taslimu. Usiache vitu milangoni kwasababu vinaweza kukandamiza mlango na jiefushe kuweka vitu vizito kwa kuvipanga kwenda juu na kama umefanya hivyo vipange vizuri.
Hakikisha unaondoa plugs zote mara baada ya matumizi ili kuepuka mlipuko. Weka nafasi kati ya vitu vinavyokaribiana na vilipuzi.Maeneo mengi ya Japani kuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kukimbilia watu wakati wa tetemeko na kama ni mgeni angalia wenyewe wanakimbilia wapi. Tetemeko ni tukio la kushitukiza kwahiyo hata unapotembea barabarani lazima uwe na uchaguzi mitaa ya kupita labda ikiwa hakuna budi. Kama huna mahali pa kuingia chukua mto ama nguo weka kichwani utakusaidia bila shaka. Mtikisiko mkubwa unapopita zima majiko ya gesi na vifaa vya umeme .Fungua milango na vaa viatu muda wote unaweza kukatwa na vioo vinavyovunjika.
La msingi usibabaike tetemeko lenyewe halilipuka linatingisha. Epuka kutumia lift kwenye majengo . Tembea usitumie gari, baiskeli wala pikipiki.Mara nyingi nchini Japani Matangazo kwa njia ya Redio na Televisheni hutolewa dakika tatu kabla ya tukio lakini kama ndio ulikuwa ukisikiliza Ndombolo ama Kijapani hakipandi kijasho kitakutoka ndugu yangu …
Usikimbie ovyo ovyo chini ya nyaya za umeme kuwa mwangalifu.
TRENI; Ukiwa ndani ya treni jisikize vyema usianguke na treni itasimama . Tulia subiri maelekezo ya wahudumu wa treni . Usiruke nje ya treni utaumia au kupoteza maisha tulia na kama hujui lugha angalia wenzako wanaelekea wapi nawe fuata.Kama una familia hebu tengeni siku moja ya kufanya mazoezi hayo …Bila shaka umefaidika na Mirindimo ya Jumamosi hii.

Posted by BM. on Saturday, March 28, 2009

Hawa SATO upo?

Posted by BM. on Saturday, March 28, 2009


Posted by BM. on Saturday, March 28, 2009

Bro. Koffi Annan na Peter Omari,....hapaharibiki neno.

Posted by BM. on Saturday, March 28, 2009

Intl.P Peter Omari , Koffi Anna na Mke wake kulia.

Posted by BM. on Friday, March 27, 2009

Utafiti wa kisayansi umethibitisha kuwa kucheka na kutabasamu mara kwa mara ni tiba ya mwili. Penda kufurahi , kucheka na kutabasamu .Watu wanaonuna na kukunja uso kila mara wanakabiliwa na magonjwa mengi msongo wa mawazo -stress, PB, kichwa na maji kupungua mwilini. Acha kununa wewe...Makala kamili siku nyingine.

Posted by BM. on Friday, March 27, 2009

IntlP.P.O Kushoto na Paparazi Shija Felician wa Kahama mkoani Shinyanga katika picha ya pamoja...Safiiiiii.

Posted by BM. on Friday, March 27, 2009

Spika wa Bunge la Kongo –DRC amejiuzulu baada ya kukosoa uamuzi wa Serikaali ya nchi hiyo kuviingiza vikosi vya Rwanda nchini humo mwezi january. Mamia ya askari waliitwa mashariki mwa Kongo kupambana na waasi
Ilikuwa ni chagizo kutoka kwa wabunge wa chama tawala anachotokea cha The People's Party for Reconstruction and Democracy ambacho kiongozi wake ni Raisi Joseph Kabila. Akihutubia Bunge Vital Kamerhe anasema anaondoka kwenye kiti bila mjadala wala upigaji kura .
Zamani huyu Jamaa alikuwa mshauri wa Kabila , na Raisi Kabila mwenyewe aliwahi kusema operesheni za kijeshi haziwezi kutangazwa kwenye bunge la watu mia tano na ushee. Aliwaambia wabunge kwa kisukuma "I ask you to please accept my resignation without debate or vote. God loves Congo, and I believe in my country's future," he told lawmakers.

Posted by BM. on Friday, March 27, 2009

Moja ya hoteli maarufu jijini Mwanza....

Posted by BM. on Thursday, March 26, 2009


Posted by BM. on Thursday, March 26, 2009

Dar Tambarare .....kwa raha zako nenda Mbagala...

Posted by BM. on Thursday, March 26, 2009

Ajali za barabarani zipo nchi Japani ingawa si nyingi sana mwaka uliopita wa 2008 ajali 760,000 zilitokea nchini Japani, taifa lenye watu takriban millioni 130. Watu waliopoteza maisha walikuwa 5,155. Jamaa wakali sana hapa kwa madereva walevi. Ukikutwa umekunywa hata nusu glasi tu ya pombe na unaendesha gari kifungo kisichozidi miaka mitano jela ama faini isiyozidi Shillingi za kitanzania Millioni 14 hivi na ukipanda gari linaloendeshwa na mtu aliyekunywa pombe jela miaka mitatu au faini millioni saba hivi za kitanzania kwakuwa umeshabikia kutendwa kwa kosa hilo upo hapo!

Posted by BM. on Thursday, March 26, 2009

Japani ni nchi ya milima na ina mishituko ya mara kwa mara ya matetemeko. Linapotokea inakuwa balaa hebu angalia picha hizi …hili lilitokea mwaka 2004 maeneo ya Hakozaki –Hapa Japani. Ni unatakiwa kufanya likitokea tetemeko. Habari zaidi utazipata katika makala ya kila wiki katika blog hii inayoitwa Mirindimo ya Jumamosi. Hakikisha kila wiki unapitia makala hiyo.

Posted by BM. on Thursday, March 26, 2009

Barabara inapokatika linapotokea tetemeko.

Posted by BM. on Thursday, March 26, 2009


Moja ya miundombinu iliyopo Japani...treni na magari juu na chini pamoja na ardhini na maduka tyamefunguliwa katikati hapo...eeh!

Posted by BM. on Wednesday, March 25, 2009

Binti mrembo wa Kijapani , mwenye sura ya aibu kidogo na kwa muonekano wa nje asiye na rabsha yoyote . Huyu ni Hatakeyama mwenye miaka 34,amehukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Japani kwa kumuua mtoto wake mwenye miaka tisa aitwaye Ayaka kwa kumtupa mtoni eneo la darajani.
Ilikuwa tarehe 9 mwezi April mwaka 2006 alimchukua binti yake anayenekana pichani kwenye gari katika mji wa Fujisato mkoa wa Akita na kwenda naye hadi kwenye daraja moja na kumuongopea kuwa anataka kumuonyesha mchezo Fulani. Akampandisha juu ya kingo za jaraja na kumsukumiza.
Kama hiyo haitoshi May 17,2006 alimuua mtoto wa jirani yake ambaye alikuwa akifika mara kwa mara hapo nyyumbani kumuulizia kwa lengo la kutaka kucheza naye. Hatakeyama akaripoti Polisi kwa kudai mtoto alimponyoka alipomuweka katikakingo za daraja lakini wapelelezi hapa wako makini wakagundua kila kitu bila hata kutumia kipigo kama kule…Alipohojiwa sana akadai kuwa ugumu wa maisha ulimchaganya . Mara kadhaa alikuwa akitokwa na machozi mahakamani. Na katika tukio lililowafanya wapelelezi wastuke alisema kuwa muda mfupi kabla ya kumponyoka mwanawe alimwambia mama usiniue …hee akasema amemponyoka …lakini baadaye akasema ..kweli nilimsukuma. Mwili wa mtoto wake umepatikana ndani ya maji na wa jirani pia umeonekana. Hakimu kamwambie akaishi jela MAISHA.

Posted by BM. on Wednesday, March 25, 2009

Unapajua Masabo...*Sipajui* ...Kumbe hujafika..

Posted by BM. on Wednesday, March 25, 2009

Jamaa wanapojidunga kilaji...

Posted by BM. on Tuesday, March 24, 2009

Mamia ya Nyangumi na Pomboo wanajikuta wako katika fukwe na wengi wao wanapoteza maisha. Huko Australia katika kipindi cha wiki moja tu zaidi ya wanyama hao 70 wamekufa . Haijulikani kwanini wanaogelea ufukweni na hatimaye kuzama mchangani. Pichani wafanyakazi wa kujitolea wa mazingira na uhifadi Huko Australia wakiwapa huduma ya kwanza kwa kuwamwagia maji ya bahari ili wanapopata nguvu kidogo wamweze kuwarudisha baharini. Ni wazito na kuwachukua kwa winchi pia unaweza kuwapa vidonda wakafia majini…Aisee

Posted by BM. on Tuesday, March 24, 2009

Cafenol, Aspro magonjwa 20, Lawalawa , eveready chapa paka....hebu nikumbushe...!

Posted by BM. on Tuesday, March 24, 2009

Jengo la mahakama ya Mwanzo Miguwa, Nzega...jengo muhimu...

Posted by BM. on Tuesday, March 24, 2009

Nzega Mjini ,....leo mchana(J4)

Posted by BM. on Tuesday, March 24, 2009

Peter Omari(L) -Sahara Communicationna John Doto (R)-Mwananchi hatimaye wamekutana viwanja vya Nzega. Hapaharibiki kitu...next makaribisho.

Posted by BM. on Tuesday, March 24, 2009

Nzega....

Posted by BM. on Monday, March 23, 2009

Hatimaye yule nyota wa Televisheni Jade Goody, aliyekuwa akikisubiri kifo kwa siku kadhaa baada ya madaktari kumwambia ajiandae kufa kutokana na na kufikia kiwango cha kutisha cha Kansa. Amefariki dunia jana Jumapili akiwa na miaka 27. Kilikuwa kifo kichungu na alijiandaa kwa ushujaa mkubwa wa kibinaadamu kwa kufunga ndoa ya kidini katika siku zake za mwisho. Mambo mengine ni kuandaa mazishi yake mwenyewe na kuingia mkataba na shirika moja la Tv kutangaza mazishi yake.
Waziri Mkuu wa Uingereza wa Uingereza anaongoza shughuli ya maombolezi.Kifo kilimkuta wakati akiwa usingizini huku amezungukwa na mume wake Jack Tweed na mama yake Jackiey Budden .Ameondoka duniani na kuwaacha watoto wake wawali wadogo wa kiume. Mazishi yatafanyika baada ya siku 10 na mwili wake umeshapelekwa nyumbani kwake.

Posted by BM. on Monday, March 23, 2009

Akielezea kifo cha binti yake, mama yake mrehemu aitwaye Jackiey Budden mwenye umri wa miaka 50 sasa alielezea jinsi alivyoung'ang'ania mkono wa binti yake wakati alipokuwa kwenye dakika za mwisho mwisho za kukata roho.Jade alifariki jana asubuhi akiwa nyumbani kwake kwenye kitongoji cha Upshire, Essex, nchini Uingereza akiwa amezungukwa na ndugu zake wa karibu na marafiki zake.
Hebu soma historia yake hapa; Jade alizaliwa mwaka 1981 na alijipatia umaarufu nchini Uingereza baada ya kushiriki mashindano ya Big Brother mwaka 2002 na tangia hapo alikuwa hakosekani kwenye udaku kwa vimbwanga vyake mbali mbali kikiwemo kile kilichotokea mwaka 2007 wakati aliposhiriki mashindano ya Big Brother ya watu maarufu duniani na kulaumiwa kwa ubaguzi aliomfanyia mwanadada Shilpa Shetty wa India.Jade aligundulika ana kansa wakati alipokuwa akishiriki mashindano ya Big Brother ya India mwaka 2008.Jade alirudi Uingereza kuanza matibabu na miezi miwili iliyopita madaktari wake walimwambia atafariki ndani ya wiki chache kwa kuwa kansa yake ilikuwa imeishaenea mwili mzima.Jade aliamua kufunga ndoa na mpenzi wake Jack Tweed wiki mbili baada ya kupewa taarifa hiyo na baadae aliamua kubatizwa yeye na watoto wake akiwa hospitalini hajiwezi.Kabla hajafariki Jade inasemekana alikuwa ameishapangilia mazishi yake yatakavyokuwa akitaka mazishi yake yawe kama sherehe kubwa ya kuwaaga watu kwa mara ya mwisho.Msemaji wake Max Clifford alisema kuwa Jade anataka jeneza lake lisindikizwe na msururu wa magari yatakayokatiza mitaa ya Esex alikokulia.Jade pia alitaka sala za mazishi yake zionyeshwe live kwenye televisheni kubwa zitakazowekwa nje ya kanisa atakalopelekwa.Inasemekana pia Jade pia alishagua nyimbo za kusindikiza jeneza lake.Kifo chake kimewahuzunisha wengi akiwemo waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown aliyeelezea kusikitishwa sana na kifo chake.Kifo chake kinasemekana kitaokoa maisha ya wanawake wengi kutokana na kuongezeka kwa jitihada za kupambana na Cervical Cancer iliyosababisha kifo chake.Mamia ya watu wameendelea kumiminika nyumbani kwa mama yake kuweka maua na kutoa salamu zao za pole.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu Jade peponi , Amin.

Posted by BM. on Monday, March 23, 2009

Alipoelezwa wazi kuwa ajiandae kufa...

Posted by BM. on Sunday, March 22, 2009

Wanasayansi nchini Japani wamefanikiwa kutengeneza roboti mithili ya binti mrembo wa kijapani , ambaye ana uwezo wa kutabasamu , kukasirika kuhisi uwepo w a mtu karibu na kukaribisha wageni na kuwaelekeza mahali pa kupita.Waandishi wa habari hapa Tsukuba Japani walikusanyika kuuona uvumbuzi huu wa aina yake . Hawa jamaa kuweka roho imewashinda…watundu sana. Itafika siku unaingia ofisi ya mtu unakuta maroboti matupu ole wako mshindwe kuelewana hutoki…

Posted by BM. on Sunday, March 22, 2009

Baba mtakatifu Benedict XIV akiwasili katika makazi ya Raisi wa Cameroon Raisi Paul Biya na mwanamama mrefu ni Mkewe raisi Bi. Chantal. Biya amekuwepo madarakani tangu mwaka 1982.

Posted by BM. on Sunday, March 22, 2009

Pope Benedict XVI akipungia waumini katika gari lake maalum la Usalama alipoingia katika Uwanja wa michezo wa Younde , Cameroon .

Posted by BM. on Sunday, March 22, 2009

Shirika moja la Marekani limefanikiwa kutengeneza gari la kwanza duniani ambalo lina uwezo wa kutembea barabarani na kupaa angani kama ndege.Gari-ndege hilo linalouzwa kwa dola 194,000 linatumia mafuta ya kawaida kama magari mengine na lina uwezo wa kubeba abiria wawili tu, gari hilo lina uwezo wa kwenda mwendo wa kilomita 82 kwa saa liwapo ardhini na lina uwezo wa kwenda kilomita 185 kwa saa liwapo angani.Mnunuzi wa gari hilo anatakiwa kuwa na leseni mbili, moja ya udereva wa gari na nyingine ya urubani na ukitaka utapewa mafunzo na urubani kwa watu wanaovutika kununua gari hilo. Gari hilo lina ukubwa sawa na magari mengine kiasi cha kuwa na uwezo wa kuingia kwenye depo ya magari bila matatizo yeyote. Ili kulitumia gari hilo kama ndege, kuna kitufe maalumu ambacho hubonyezwa na kufanya mabawa yachomoze pembeni na ukitaka kulitumia tena barabarani mabawa hujikunja na kuelekea juu.

Posted by BM. on Sunday, March 22, 2009


Posted by BM. on Sunday, March 22, 2009


Posted by BM. on Sunday, March 22, 2009

Magari kukuu yakiwa yamejaa dambo katika eneo la kati la jiji la Chongqing, nchini China. Ni kama Dambo la Vingunguti nchini China..Lingekuwa Dar sijui ingekuwaje!

Posted by BM. on Sunday, March 22, 2009

Jamaa analipia hapo karibu millioni moja na nusu za kitanzania Hongkong kwa mwezi hapo mahala ...

Posted by BM. on Saturday, March 21, 2009

Raisi Marc Ravalomanana akiwa na Raisi Kikwete Ikulu Dar Oct.6,2008..aliporudi kwao ndipo akaanza kupata chagizo hadi kumuondoa kitini...Fuatilia matukio ya huko Madagascar.
Marc Ravalomanana aliyezaliwa tarehe 12,Desemmba mwaka 1949 huko Imerinkasinina amekaa katika Ikulu za nchi hiyo tangu mwaka 2002. Alijichukulia madaraka ya urafiki baada ya kukataa matokeo ya Uchaguzi wa Uraisi mwaka 2001 akidai alimshinda Raisi wa wakati huo Didier Ratsiraka na hivyo kuingia Ikulu kwa mabavu lakini mwaka 2006 akashinda uchaguzi wa kidemokrasia na kuingia Ikulu kihalali kabla ya kuondolewa majuzi.

Posted by BM. on Saturday, March 21, 2009

Askari wakiwa nje ya makao makuu ya Raisi yaliyopo Lavoloha km 13 nje ya Madagascar anapoishi Raisi aliyeachia ngazi Marc Ravalomanana , wakati huu tayari alikwishatimka kutoka hapo.

Posted by BM. on Saturday, March 21, 2009

Raisi Marc Ravalomanana na Mkewe wakiondoka Ikulu baada ya mambo kuwa magumu...

Posted by BM. on Saturday, March 21, 2009

Kiongozi aliyetangaza kuwa Raisi wa Madagaska Andry Rajoelina ameapishwa kukamata madaraka kipindi cha mpito cha miaka miwili . Sherehe za kuapishwa zilifanyika katika uwanja wa mpira.Hii ni baada ya siku nne za kushika nchi kwa mapinduzi ya taratibu ambapo Raisi wa Nchi nchi hiyo Marc Ravalomanana amejiuzulu na kuachia madaraka kwa wakuu wa majeshi nao wakampa Rajoelina .Kijana huyo mwenye sura ya kitoto ana miaka 34 lakini ana kipaji kikubwa cha ushawishi wa kisiasa. Siku za nyuma alikuwa Dj Jijini Antananarivo katika kituo kikoja cha FM kabla hajawa Meya wa Jiji la Antananarivo.

Posted by BM. on Saturday, March 21, 2009

President Andry Rajoelina na V...