Mke wa raisi wa Marekani Bi Michelle Obama jana aliwashangaza waliombaini baada ya jana alhamisi kuingia kwenye supermarket moja akiwa amevalia mavazi ya kawaida ya kutokea, kofia inayovaliwa na wacheza baseball pamoja na miwani ya jua na kufanya manunuzi katika duka hilo linalofahamika kama Target Corp. store huko Alexandria, nje kidogo ya jiji la Washington.]...akiwa katika foleni ya kulipia vitu alivyonunua.
Timu ya walinzi ambayo haikujulikana na wateja waliokuwemo kwenye duka hilo kutokana na kuvalia nguo za kawaida walifika dukani hapo nusu saa kabla ambapo baadaye Bi obama aliingia katika duka hilo na kufanya manunuzi yake kwa dakika 40 , kisha akapanga foleni kwa keshia ili kulipia bidhaa zake.
Mtunza fedha alimgutukia baadaye alipoona jamaa mmoja akimpiga picha lakini vinginevyo zoezi hilo lingekwisha kimya kimya. Mwenyewe amichelle anasema kuwa anazikosa fursa hizo kutokana na wadhifa wake na kukaa katika white house.
Michelle anatajwa kuwa ni mke wa Raisi aliye wa kwanza kutoka nje kwa ajili ya manunuzi kwa mwonekano wa mwananchi wa kawaida ingawa Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton aliwahi kuonekana mitaani na mume wake wakati wa mwisho wa wiki.
...(AP Photo]
Ni hapa...
Namkubali sana huyu mwanamuziki ...naamini nawe utaufurahia mdundo huu!..
A Ghanaian woman has married her dog because it has qualities she had seen only in her late father. Emily Mabou, 29, of Aburi, married the 18-month-old dog in a ceremony attended by a traditional priest and local, curious villagers, reports the Daily Dose.
Her younger brother David Mabou said her family boycotted the wedding which they felt was “a stupid step to combat her loneliness”.But Ms Mabou said: “For so long, I’ve been praying for a life partner who will have all the qualities of my dad. My dad was kind, faithful, and loyal to my mum, and he never let her down.
“I’ve been in relationships with so many men…, and they are all the same… skirt-chasers and cheaters. My dog is kind, and loyal to me and he treats me with so much respect.”
In the ceremony, the priest warned villagers not to mock the wedding, but to “rejoice with her as she has found happiness at last”.
ananova.com
Headaches
Here’s the rundown of 10 things you may not know about headaches - and how to avoid them:
1. Sex Causes Headaches: Here’s a surprise: men are more likely to get these types of headaches than women. According to the American Headache Society, two types of headaches are related to sexual activity: a dull ache that develops as the sex act increases or a severe one that strikes as orgasm nears. Experts say it’s best to check with your doctor the first time you get one of these headaches. Hint: performance-enhancing drugs can bring on headaches in men who have migraines.
2. Sinus Headaches Are Rare: Nasal and sinus congestion, facial pain and pressure, and a headache usually don’t add up to a sinus headache. Headache specialists say that “true” sinus headaches are rare. In a study with almost 3,000 patients who had at least six “sinus headaches” in the previous six months, medical evaluations showed that 88 percent actually had migraines. In another study, 45 percent of migraine patients had either nasal congestion or watery eyes. Tipoff: it’s probably migraine if in addition to “sinus” symptoms, you’re nauseous, sensitive to light or noise and if the headache throbs and worsens with activity.
3. Processing 3D Images Causes Brain Strain: A Northwestern University ophthalmology professor warns that a large segment of the population may develop a headache and nausea while watching 3D movies. This is due to the brain strain involved with processing the three dimensional images - the more an image jumps out at you, the more effort your brain must make to fuse the pictures together, says Northwestern University's Michael A. Rosenberg, MD.
4. Take-Off and Landing Lead to Headaches: No, this has nothing to do with the aggravation of cancelled flights or long delays. Instead, sudden, severe, stabbing headaches during a plane’s ascent or descent are being reported. Doctors haven’t figured out yet what causes them. Luckily, the pain lasts only about 20 minutes.
5. Bug Spray Prompts Headaches: It’s not the bugs but exposure to insecticides used to kill them that causes these headaches (plus dizziness, trouble breathing, nausea and vomiting). According to the U.S. Centers for Disease Control and Prevention, most cases required no medical treatment, but one death has been reported and 18 percent of those exposed to the insecticides required medical attention.
6. High Cholesterol Causes Headaches: You may not have to worry unless you’re in your late 60s or older and have migraines with aura (the flashing lights, tingling and other signs of a headache’s approach that about one-third of migraine patients report). A recent study found a link between migraine with aura and high cholesterol in seniors. Migraine with aura has also been linked to a higher risk of heart disease and stroke.
Need to lower your cholesterol? Let's start with what's on your plate.
7. Headaches Might Be Genetic: Researchers have pinpointed three genetic variations linked to an increased risk of migraines. One is involved in sensing cold and pain, another is linked to several processes including signaling in nerve cells (neurons). The role of the third isn’t yet known. Each of the gene variations identified alters the risk for migraines by 10 to 15 percent.
8. Alcohol, As a Trigger, Is Overstated: Research from Italy suggests that the role of alcohol and some foods in triggering migraines has been overstated. Instead, the investigators found that stress, fatigue and in women, menstruation are most often the culprits. They suggested that migraine patients who want to drink alcohol could try small amounts of specific types to see what they can tolerate.
9. Botox Can Treat Headaches: Best known as a wrinkle remover, Botox also can put the brakes on chronic migraines (those that occur 15 days per month or more). The U.S. Food and Drug Administration has approved the use of Botox for migraine prevention. Injections seem to cut down on headaches, although studies suggest that Botox doesn’t work as well as some prescription drugs. Researchers still haven’t figured out how Botox staves off the headaches, but they do know that effects last only about three months before patients have to be re-injected.
10. The Battlefield Has Created a New Type of Headache: About one third of the soldiers returning from Iraq are bringing with them a new type of chronic migraine caused by nerve damage or the pressure from bomb blast waves. While these headaches are still being studied, treatments include rest, avoiding migraine triggers, stress management and changes of diet.
Learn more about different types of headaches and how to prevent them.
By Lisa Collier CoolGet the information you need to improve your health and wellness on Healthline.com.
Prof Wangari Maathai, Nobel Peace laureate and conservation heroine, has died in Nairobi after a long battle with cancer. She was 71. The environmentalist and politician died at the Nairobi Hospital at around 10pm on Sunday
Insh
President Kibaki said the world has not only lost a renowned environmentalist and but also a great human rights crusader. //Tanzania's President Jakaya Kikwete celebrates Maathai, describes her as a great woman and an inspiration for many women across Africa.
Jaji Mkuu wa Zambia Ernest Sakala jana Ijumaaa mchana alimwapisha Bw. Michael Satta kuwa raisi Mpya wa tano wa Zambia katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya mahakama kuu nchini humo.
Viongozi kadhaa walihudhuria pamoja na maelfu ya wananchi wa nchi hiyo, ambapo Raisi aliyeshindwa Rupia Banda wa chama cha MMD alikabidhi bendera na katiba ya nchi hiyo kwa mwenzake kama ishara ya kuiachia Ikulu..
Hasira nini nini, tunaweza kusema ni hali ya kuwa na hamaki au ghadhabu iliyovuk kiwango. Hasira yenyewe , ni jambo la kawaida tu linalostahili kuwemo ndani ya tabia ya binaadamu. Tunasoma kwenye vitabu vya saikolojia kuwa hasira inasukuma afya ya mtu, inaifanya akili ifanye kazi kwa kasi na kupata ufumbuzi wa jambo huku kukiwa na shindikizo kubwa. Lakini hali hiyo inapozidi kiwango na kufikia ukubwa ambao mwenye hasira hawezi kabisa kuidhibiti, linakuwa tatizo.
Unakuwa ugonjwa unaohitaji tiba . Hiki ni ‘kitabia’ kinachokera, kwake mwenyewe na kwa wengine. Inapofikia hapo hasira huvunja heshima, adabu na hata haiba ya mtu mwenye tabia hiyo. Watu wenye hasira na ghadhabu wakati wote , sura zao hukunjana na tabasamu hupotea kabisa. Kitabia kikikolea uwezo wa kuonyesha bashasha hupotea na huwa kituko mbele ya watu. Mbaya zaidi hali hii inapompata kijana au binti mdogo.
Watu wenye hasira iliyopindukia wanajenga visasi, makazini, majumbani kwa wenza wao na hata kwenye nafsi zao. Wakati mwingine hujikuta wakipiga ngumi ukutani au kwa kutumia viganja vyao na kutoa matusi yanayowakashifu wao wenyewe au wapendwa wao au kufyonya, wakijaribu kutusi wasichokiona.
Mtaalamu bingwa wa Saikolojia duniani Dr. Charles Spielberger anaielezea hasira kama hali ya mhemko inayoanzia kwenye hamaki ya kiwango kidogo kinachokubalika na kuishia kwenye ghadhabu inayoelezeka kama ugonjwa. Hali hii huambatana na mabadiliko ya kisaikolojia na kibailojia. Unapokuwa umekasirika, mapigo ya moyo na msukumo wa damu huongezeka na kiwango cha homoni za nishati ya mwili na adrenalini huongezeka pia. ‘Ugonjwa wa hasira’ usipopatiwa tiba hatimaye hukuletea janga lingine la shindikizo la juu la damu au kihoro…huu ni msononeko wa kupindukia na hata wengine huiona hii dunia si mahala pazuri pa kuishi. Kuna watu ambao matamshi yao ni ya ‘Kihasirahasira’, maneno yao ni ya mkato na muda wote huwa wamenuna, wakilaumu na kukunja uso. Watu hawa wanahitaji tiba. Wanahitaji tiba kwasababu ugonjwa huu ukiachwa na kujenga usugu, hauwezi tena kutibika na tiba iliyobakia ni kwa watu kukutenga na kukuadhibu. Unaweza kuanza kwa kujiangalia kwenye kioo , ili kuona ikiwa hiyo ndio sura yako halisi au imetokana na tabia uliyonayo ya hasira.. Pengine unajiuliza nifanye nini sasa;
Kwanza kabisa , unapojikuta katika hali kama hiyo, weka katika akili yako kuwa huhitaji kuendelea kuwa hivyo kwa muda mrefu. Jaribu kugawa lawama pande mbili, kwako na kwa mwenzako. ‘Nimekosewa ndio…na mimi nimekosea nini ?’, unahitaji kujiuliza. Kaa mahali palipo na utulivu , vuta pumzi ya kutosha na pumua na kisha tuliza mawazo yako. Hiyo ni hatua ya kwanza ya tiba.
Mara kadhaa jiambie kuwa ‘nataka yaishe’ , ‘nataka niyamalize’ na kwa wale wenye imani ya kidini warudishe mawazo yao huko Imani ya kidini huleta faraja katika nyoyo. Na kisha Karibisha wazo la kuomba msamaha, kusamehe, na kurejesha uhusiano na epuka visasi na maapizo yatakayo’kutafuna kila uchao’.
Kwa kawaida , watu wenye tabia za hasira huwa na maneno mengi ya kuhalalisha kile kinachoumiza nyoyo zao, wakitumia viapo na vineno vya ‘Kujiamini’. Badili sasa msamiati huona jiulize kama uko kwenye mwelekeo sahihi na salama au unaelekea ‘siko’ na penda kujutia. Hebu jaribu kutumia maneno, ‘Samahani, pole, kumradhi, asante, nahitaji badala ya ‘nataka’. Kuna watu walikwisha sahau maneno matamu katika msamiati wao. Yatafute na yaanze kuyatumia. Unahitaji kusikiliza zaidi badala ya kupayuka zaidi. Siku zote anayezungumza mwisho ‘anashinda’. Sidhani kama unahitaji kuwa na tabia ya hasira iliyopitiliza, badilika, au unasemaje!.
A simple initiative in the Philippines is bringing a bit of brightness into the lives of the country's poorest people.The project is called "Litre of Light", and the technology involved is just a plastic bottle filled with water. It's an environmentally-friendly alternative to an electric light bulb, and it's virtually free. The BBC's Kate McGeown reports from Manila.
Bofya; http://www.bbc.co.uk/news/world-asia-pacific-14967535
Polisi wamemkamata Mfanyakazi mmoja wa Shirika la Utangazaji la Japani –NHK akituhumiwa kutumia kamera aliyoificha kwenye kiatu chake kumpiga picha mwanamke mmoja bila ridhaa yake.
Polisi wametoa taarifa hiyo rasmi siku ya Jumatatu kupitia televisheni ya Asahi kuwa Daisuke Hayashi, mwenye miaka 33, alikamatwa katika duka la nguo huko Tamachi akitumia kamera yake kupiga picha blauzi ya ndani ya mwanamke mmoja mfanyakazi wa duka hilo. Kamera hiyo ilifungwa kwenye kamba za viatu vya hayashi.
Polisi walinukuliwa wakisema kuwa Hayashi alikamatwa aliwahi kukamatwa kwa kufanya kitendo kama hicho hicho siku zilizopita. Alijitetea kuwa vitendo vyake hivyo vina nia ya kujipunguzia msongo wa mawazo ambao unamkabili kila mara.
Source : Japantoday.com
Kimbunga kikali kimefika eneo la kattikati ya Japani leo mchana na kusababisha mvua na kuleta tishio la kutokea kwa maporomo ya udongo na kufurika kwa mito. Hadi sasa kimbunga kimeshapoteza maisha ya watu watano na wengine wawili hawajulikani walipo.
Shirika la utabiri wa hali ya hewa amesema kuwa hadi kufikia leo jumatano mchana , kimbunga hicho kinachojulikana kwa jina la Roke kilikuwa kikivuma kuelekea kaskazini Magharibi kwa kasi ya kilometa 35 kwa saa katika bahari , mashariki ya mkoa wa Wakayama. Upepo mkali wenye kasi ya kilometa 100 kwa saa umeshuhudiwa katika maeneo hayo.
Kimbunga hicho kimekuwa kikivuma kuelekea upande wa Kaskazini-Mashariki na kufanya mvua inyeshe katika maeneo ya kati na mashariki ya Japani wakati wa mvchana na mvua imerekodiwa kufika kima cha millilita 400 katika maeneo ya kati ya Japani katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Huku haya yote yakitokea Shirika la Utangazaji la Japani kupoitia Idhaa zake ilikuwa ikirusha matnagazo yake moja kwa moja kuwaeleza watu kile kinachoendelea wakati huo. Nasi idhaa ya kiswahili hatukuwa nyuma!
Polisi wamesema kuwa kimbunga kimewaua watu wanne na wawili hawajulikani walipo , wakati mtu mmoja alikutwa amekufa baharini karibu na bandari , magharibi mwa Japani , wengine wawili walikutwa wamekufa katika mito katikati na magharibi mwa japani na mwingine alianguka kutoka kwenye paa la nyumba alipokuwa akirekebisha paa lililokuwa likivija.
Inaelezwa kuwa hadi kufikia leo mchana nyumba zaidi ya 900 kote nchini Japani zilikuwa zimezingirwa na maji. Maelekezo ya watu kuhama au ushauri juu ya hatua za kuchukua imetolewa kwa watu takriban 340,000 katika mikoa 15 iliyopo magharibi na eneo la kati la Japani
Wakati huo huo, Wafanyakazi waliopo katika Mtambo namba moja wa nishati ya nyuklia wa Fukushima uliopigwa na mawimbi ya tsunami kufuatia tetemeko kubwa la ardhi , mwezi Machi tarehe 11 wanafanya kazi kubwa ya kuufanya mtambo huo usipate athari inayoweza kuleta tishio kwa maisha ya watu, wakati huu tufani ikielekea upande huo.
Tufani hiyo inayojulikana kwa jina la Roke inatarajiwa kulifikia eneo hilo leo Jumatano usiku hivyo vyuma katika mabomba ya kuingiza maji kwenye mtambo huo zinaendelea na kazi ya kutoa maji yaliyochafuliwa na mionzi ya nyuklia imesimama kutokana na upepo mkali na tufani.
Hata hivyo Shirika la umeme la Tokyo-TEPCO linalousimamia mtambo huo linasema kuwa hakuna hatari ya kuvuja kwa maji yenye mionzi kutoka kwenye majengo hayo ya mitambo.
Usafiri wa treni na mabasi ulisimama uanzia saa nane mchana, hadi saa mbili usiku ulipoanza tena .
Saa tatu na nusu hali ilianza kutengamaa..
Wanawake wamekuwa wakimiminika katika uwanja wa taifa wa Nyayo jijini Nairobi nchini Kenya kufanya ya kupata wapenzi, waume au wenza.
Ibada hiyo inaongozwa na mchungaji ambaye 'amebobea' kwenye uhubiri wa kikristo lakini hana kanisa maalum linalojulikana.
Mchungaji Chris Ojigbani raia wa Nigeria anafanya huduma ya kuondoa nuksi na kuwafanya akinamama 'kuonwa ' na kuolewa.
Source: Kenya's Daily Nation.
Timu ya watafiti wa kijapani jana Jumatano ilibainisha uvumbuzi wao wa chombo ambacho wanasema kuwa kinaweza kupima kile kinachofanyika kwenye ubongo na kuweza kukitumia chombo hicho kuimarisha kazi za ubongo madarasani au katika pilikapilika za kimichezo.
Mainjinia kutoka kampuni ya elektroniki ya Hitachi waliofanya kazi bega kwa began a wanasayansi wanasema kifaa hicho chepesi kinachovaliwa kichwani kina uwezo wa kupima kwa usahihi mabadiliko yanayofanyika katika kipindi ha dakika moja tu cha kiwango cha damu katika ubongo , kitu ambacho ni muhimu sana kujua ni kwa kiwango gani kiungo cha mwili kinafanya kazi.
Vifaa kadhaa visivyounganishwa popote vinaweza kufanya kazi wakati huo huo huku taarifa za ubongo zikijionyesha kwenye skrini pale pale na kuwafanya watafiti kufuatilia kazi zinazofanyika katika ubongo kwa watu wanaofikia 20 kwa wakati mmoja.
Kampuni hiyo kubwa ya kijapani ya elektroniki imesema kuwa kwa sasa haina mpango ya kukifanya kifaa hicho kuwa cha kibiashara ambacho kwa kawaida hutumia mwanga wa mionzi kubaini kiwango cha damu katika ubongo.
Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Fedha wa Kenya uhuru Kenyata... akieleza kuwa yeye ni mtu wa kawaida tu na ameishi maisha ya kawaida mitaani ...jina lake tu linamponza!
Tetemeko kubwa lililofikia ukubwa wa 6.2 kipimo cha richa kimetikisa pwani ya Kaskazini Mashariki mwa Japani leoAlhamisi jioni , lakini hakuna hatari ya kutokea mawimbi ya tsunami kama ilivyotokea siku zilizopita. Hadi sasa hakuna taarifa za majeruhi wala uharibifu wowote uliotokea kutokana na mitetemo hiyo.
Shirika la Utabiri wa hali ya hewa limesema kuwa tetemeko hilo lilitokea saa kumi na moja jioni kwa saa za Japani (Afrika Mashariki saa tano asubuhi) kitovu chake kikiwa Pwani ya Ibaraki , takriban kilometa 220 Mashariki mwa jiji la Tokyo, kilometa 1o chini ya bahari.
Bado watu wa Japani wanakumbuka vyema vifo vya watu takriban elfu 20 au kupotea katika pwani hiyo hiyo ya kaskazini Mashariki kufuatia tetemeko na mawimbi makubwa ya tsunami , machi 11 mwaka huu .
Katika maafa hayo , Mtambo namba moja wa Nyuklia wa Fukushima uliharibiwa na zaidi ya watu laki moja walilazimika kuyahama makazi yao kwasababu ya tishio la kusambaa kwa mionzi ya Nyuklia.
Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa nchini.Katika mabadiliko hayo, amewateua Wakuu wa Mikoa wapya 15, kuwabadilisha vituo vya kazi Wakuu wa Mikoa watano na wengine saba wamestaafu kwa mujibu wa taratibu. Mkuu wa Mkoa wa Singida amebaki kwenye kituo chake cha kazi wakati Wakuu wa Mikoa wengine wanne watapangiwa kazi nyingine.
Aidha, Wakuu wa Mikoa mipya minne ya Simiyu, Geita, Katavi na Njombe itakayoundwa baada ya taratibu kukamilika watatangazwa baadaye.Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Wakuu wa Wilaya 11 wamepandishwa Vyeo na kuwa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo: Bw. John Gabriel Tupa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara; Bw. Saidi Thabit Mwambungu (Ruvuma); Bi. Chiku S. Gallawa (Tanga); Bw. Leonidas T. Gama (Kilimanjaro); Dk. Rehema Nchimbi (Dodoma); Bw. Elaston Mbwillo (Manyara); Kanali Fabian Massawe (Kagera); na Bibi. Fatma Abubakar Mwassa (Tabora). Wakuu wa Wilaya wengine walioteuliwa ni Bw. Ali Nassoro Rufunga, (Lindi); Eng. Ernest Welle Ndikillo, (Mwanza); na Bw. Magesa Stanslaus Mulongo Mkuu wa Mkoa (Arusha).
(Bw. Mulongo , pichani , wapili kutoka Kulia)
Walioteuliwa nje ya nafasi hizo ni Eng. Stella Manyanya (Rukwa); Bibi Mwantumu Mahiza, (Pwani); Bw. Joel Nkaya Bendera (Morogoro) na Bw. Ludovick Mwananzila (Shinyanga).Waliobadilishwa vituo vya kazi ni Bw. Abbas Kandoro anayekwenda Mbeya akitokea Mwanza; Bw. Said Mecki Sadiki anayekwenda Dar es Salaam akitokea Lindi; Bibi Christine Ishengoma anayekwenda Iringa akitokea Ruvuma; Lt. Kanali Issa Machibya anayekwenda Kigoma akitokea Morogoro; na Kanali Joseph Simbakalia anayekwenda Mtwara akitokea Kigoma. Dk. Parseko Ole Kone ataendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Waliostaafu ni Bw. Mohammed Babu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera; Bw. Isidore Shirima aliyekuwa Arusha; Kanali (mst.) Anatory Tarimo aliyekuwa Mtwara; Bw. John Mwakipesile, aliyekuwa Mbeya. Wengine ni Kanali Enos Mfuru aliyekuwa Mara; Brig. Jen. Dk. Johanes Balele aliyekuwa Shinyanga; na Meja Jen. Mst. Said S. Kalembo aliyekuwa Tanga.
Wakuu wa Mikoa wanne waliostaafu ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi ni Bibi Amina Mrisho aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani; Dk. James Msekela aliyekuwa Dodoma; Bw. Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora na Bw. Daniel Ole Njoolay aliyekuwa Rukwa. (Pichani; Wastaafu Mh. Mohamed Babu aliyekuwa mkuu w mkoa wa Kagera , kushoto na katikati Gen. Yohana Balele. Kulia Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, mh.Ernest Kahindi)
Wakuu wote wa Mikoa waliopo sasa wameagizwa kuandaa Hati za Makabidhiano (Handing Over Notes) katika muda wa siku 14 kuanzia siku ya kuapishwa kwa Wakuu wapya wa Mikoa. Aidha Wakuu wa Wilaya ambao wamepandishwa vyeo kuwa Wakuu wa Mikoa nao wanapaswa kufanya hivyo hivyo kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya watakaopangiwa vituo vitakavyokuwa vimeachwa wazi kutokana na uteuzi wao.
Wakuu wa Mikoa ile minne mipya na Wakuu wa Wilaya watakaoteuliwa hapo baadaye nao watatakiwa kuandaa Hati za Makabidhiano ndani ya siku 14 tangu kuapishwa.
Makabidhiano hayo lazima yahusishe pia kutembelea kwa pamoja baadhi ya maeneo na miradi ambayo ni muhimu kama sehemu ya makabidhiano yao.Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa na Wakuu wa Mikoa minne mipya wakaoteuliwa pamoja na Wakuu wote wa Wilaya watakaoteuliwa baada ya zoezi kukamilika watatakiwa kuhudhuria mafunzo ya wiki tatu kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi wa kiuongozi na kiutendaji.
Wakuu hao wapya wa mikoa wataapishwa siku ya Ijumaa, Septemba 16, 2011 saa 4.00 asubuhi kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wakuu hao wapya wa mikoa; vituo wanavyokwenda na vituo walivyotoka ni kama ifuatavyo:
JINA LA MKUU WA MKOA KITUO AENDAKO KITUO ATOKAKO
1. Bw. Saidi Mecki Sadiki DAR ES SALAAM RC - Lindi
2. Bw. John Gabriel Tupa MARA DC - Dodoma
3. Bw. Saidi Thabit Mwambungu RUVUMA DC - Morogoro
4. Kanali Joseph Simbakalia MTWARA RC Kigoma
5. Bi. Chiku S. Gallawa TANGA DC - Temeke
6. Bw. Abbas Kandoro MBEYA RC Mwanza
7. Bw. Leonidas T. Gama KILIMANJARO DC – Ilala
8. Dkt. Parseko Ole Kone SINGIDA RC Singida
9. Eng. Stella Manyanya RUKWA Mbunge V/Maalum
10. Bibi Christine Ishengoma IRINGA RC Ruvuma
11. Dk. Rehema Nchimbi DODOMA DC - Newala
12. Bw. Elaston John Mbwillo MANYARA DC – Mtwara
13. Col. Fabian I. Massawe KAGERA DC - Karagwe
14. Bibi. Mwantumu Mahiza PWANI Mbunge/NW Mstaafu
15. Bibi. Fatma A. Mwassa TABORA DC - Mvomero
16. Bw. Ali Nassoro Rufunga LINDI DC - Manyoni
17. Eng. Ernest Welle Ndikillo MWANZA DC - Kilombero
18. Lt. Col. Issa Machibya KIGOMA RC Morogoro
19. Bw. Magesa S. Mulongo ARUSHA DC - Bagamoyo
20. Bw. Joel Nkaya Bendera MOROGORO Mbunge/NW Mstaafu
21. Bw. Ludovick Mwananzila SHINYANGA Mbunge/NW Mstaafu
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM
JUMATANO, SEPTEMBA 14, 2011.
Nakubaliana naye kwa kiasi kikubwa ...weye je? source France24..
Nimesukumwa na ahadi yangu ya kuandika kumuhusu Hayati Abisay Stephen. Huyu alikuwa bosi wangu , bosi wetu kwa hakika niliyefanya naye kazi kwa karibu, katika kipindi cha uhai wake. Mwanzo nilidhani lingekuwa jambo dogo kufikiri na kuandika , kumbe haikuwa hivyo hata kidogo.
Kwanza kwasababu nataka kuandika juu ya mtu aliyenitangulia kazini kwa zaidi ya miaka 20, mtu ambaye tangu nilipomuona kwa mara ya kwanza alikuwa tayari na nyadhifa za kiutendaji. Najua kuna watu waliofanya kazi kwa karibu zaidi kuliko mie, walikuwa wakifahamiana naye sana kuliko mimi , lakini naamini mie pia nina mambo naweza kuyadondoa kwenye tajiriba yangu kumuhusu.
Pili naandika nikijua kuwa watakaosoma simulizi hii chungu , wengi wao bila shaka ni vijana ambao kwao hawana habari za kutosha kumuhusu, hasa juu nafasi yake na tajiriba zake wakati wa uhai wake. Huyu Abisay ni wa kale kidogo kwao na kwangu. Aliingia RTD akiwa na miaka 19 tu, bado kijana na akaitumia Taasisi hiyo ya umma kwa miaka takriban 40 kabla kifo hakijakatisha maisha yake.kwa kifupi maisha yake yote na Redio tu, tena Redio ya taifa.
Mtu wa namna hiyo ni vigumu kumzungumzia kwa ukurasa mmoja. Ni kama kuwazungumzia wenzake ambao nao walikwishatangulia mbele ya haki. Hawa ni wafanyakazi wa iliyokuwa RTD kama vile , John Luwanda, Stephen Lyimo, Salim S. Nkamba, Juma Ngondae, Salama Mfamao, Siwatu Luwanda, Leonard Mtawa, Iddie Rashid Mchata, Idrissa Sadallah, Omari Jongo, Barnabasa Mluge, Hassan Nkumba, Chisunga Steven , Batty Kombwa na wengine .
Lakini sababu ya tatu, kati ya mwaka 2000 na 2008 nilikuwa nje ya jiji la Dar es salaam, niliondoka hapo kwa tiketi ya RTD. Mambo mengi yakabadilika , RTD ikawa TUT na baadaye TBC, miye nikiwa nawajibika mikoani .Niliendeleza utumishi wangu katika mikoa ya Mwanza, Arusha , huko Zanzibar (Unguja na Pemba) na baadaye Shinyanga. Na nilipohamishiwa tena Dar es salaam mwezi Mei mwaka 2008 nilikutana tena na Marehemu Abisay Stephen , tukafanya kazi kwa mwezi mmoja katika ofisi moja ya ‘taifa’kabla sijakuja hapa Tokyo , Japani kujiunga na Idhaa hii ya Kiswahili ya Redio Japani-NHK. Nahisi kipindi cha miaka tisa cha kuwa mbali na Abisay na watangazaji wenzangu wa makao makuu , mengi yamebadilika.
Tabia za watu , mienendo, mtazamo na hata harakati zao. Nimekuwa wa mikoani na wao wa makao makuu. Na huu ndio ukweli. Na sasa kuna channeli zaidi ya nne , TBC 1, TBC Taifa, TBC FM na TBC International…mabadiliko makubwa. Vijana wengi, wasomi wengi na vipaji vingi sasa kuliko pengine enzi hizo. Nilichelea , kama naweza kuwa na ujasiri wa kuandika. Lakini bado naaamini kuwa sitakuwa nje sana ya mstari, na kama itakuwa hivyo nastahili kusamehewa.
Nimemuona hayati Abisay Stephen mwaka 1989, nilipojiunga RTD . Rasmi nilianza kazi mwaka 1990, wakati huo ndani ya majengo ya RTD kulikuwa na mtindo wa uhamisho wa ndani wa kiidara ambapo watangazaji walikuwa wakihamisha kila viongozi wanapoona inafaa. Ilitokea tu, nilifanya kazi na Marehemu Abisay, katika Iliyokuwa Idhaa ya nje ya RTD, ‘External Service, Idhaa ya Taifa na baadaye Idhaa ya biashara. Kwa kawaida kila asubuhi mara baada ya kikao cha viongozi wa idara maarufu kama ‘Post Mortem’ , Idara na Idhaa zetu nazo zilikutana miongoni mwa watendajji wake . Hao ndipo nasi tulipata kusikia ‘maamuzi na maelekezo kutoka juu’ na wakati huu tukielezwa na Abisay.
Hayati Abisay , aliweza kueleza msimamo huo kwa lugha isiyokwaza , akidondoa moja baada ya jingine na kuhimiza utekelezaji. Alikuwa rafiki na bosi wa kila aliye chini yake. Alikuwa tayari kusikia changamoto za ‘vijana ‘ na mara zote aliishia kutupa moyo kuwa kwa kufanya hivyo tutafika tunakokenda. Ndipo nilipogundua uwezo wake mkubwa wa kupambanua mambo, kufuatilia masuala ya kihabari na kujenga mtandao utakaowezesha kufanikisha azima iliyopo. Mara kadhaa aliwahi kunipa majukumu na kunipa moyo kuyatekeleza. Hakuwa mtu aliyeogopa mabadiliko ya kimaendeleo na aliwahi kudokeza kuwa kuna wakati alioonekana kukengeuka alipopishana na ‘wenzake ‘ katika mambo Fulani na na kuwajiwajibishwa kwa ukengeukaji huo, kimya kimya’.
Nakumbuka aliwahi kusema kuwa ‘tunahitaji kufanya kazi kwanza , kabla ya kulalamika kwa masuala binafsi’ .
Nikiwa msaidizi wake katika Idhaa ya biashara… siku moja aliniita akaniambia kuwa amepata mwaliko wa kwenda Kenya kukutana na Wakuu wa Mashirika ya kibiashara yaliyokuwa yakileta matangazo yao RTD. Abisay akasema kuwa , wakati huo alikuwa na ndoto ya kuwaandaa vijana wa kizazi kipya kiuongozi, hivyo aliniteua niende safari hiyo kwa niaba yake. Naambiwa baadhi ya wakubwa hawakufurahia maamuzi hayo kwasababu walikuwa wakiamini mie ni mkembe bado kubeba jukumu hilo. Lakini Abisay alishikilia msimamo huo nami kweli nikafunga safari ya Nairobi na kurudi salama Dar baada ya wiki moja. Inasemwa kuwa safari ile ilileta neema ya kiasi kikubwa na imani ya makampuni hayo kwa RTD ilipanda .
Malalamiko ya makampuni hayo , zaidi ilikuwa RTD ya wakati ule ilikuwa haizingatii muda wa kupiga matangazo yao na taarifa zetu hazikuwa zinawiana na zile zilizokuwa zikitolewa na kampuni moja ya huko Nairobi iliyokuwa ikifuatilia matangazo yetu. Niliandaa ripoti na nikampa bosi wangu Abisay na akaiwakilisha kwa mamlaka ya juu , na kweli mabadiliko yalifanyika. Baadhi ya malalamiko yalikuwa kweli na mengine hayakuwa kweli lakini kimsingi tulijipanga upya na kufanikiwa kile tulichokikusudia.
(Ikumbukwe kuwa wakati huo watangazaji walikuwa wakifanya kazi za kibiashara kama majukumu ya ziada , wala hakukuwa na idara nzima ya biashara kama ilivyo hii leo.) Maamuzi yanayofanana na haya aliyafanya kwa watu wengi husussan vijana hasa alipopata fursa ya kufanya maamuzi magumu. Yatosha kusema tu, kizazi cha kati cha utangazaji kinalitambua hilo.
Pengine simulizi ni nyingi lakini itoshe kusema kuwa tumepoteza kiungo cha kizazi cha kale cha utangazaji kilichounganisha , cha kati na hiki kipya . Abisay amekufa akielekea kustaafu. Hakuwahi kuyapata mafao yake , huenda alipenda kuona akipokea kilicho chake na kukitumia kama mstaafu. Hakuwahi. Tunahitaji kuyaangalia mazuri aliyoyafanya katika utumishi wake na kumsamehe kama kuna mahali alijikwaa , kwa kujua kuwa binadamu kwa njia moja ni dhaifu.
Kwaheri bosi wangu Abisay.. nimeguswa kwakuwa umetangulia. Uliyoyafanya yanatosha , nimeandika kidogo tu na nimeshindwa kuendelea kuandika na kuandika , sina ujasiri huo kwa mtu ambaye nalazimika leo kumuita hayati. Najua maandishi haya hayataweza kubadilisha chochote , lakini itatanabaisha walimwengu kuwa kuna watu wanamkukumbuka kwa yale yaliyotokea miaka ile. Hayati Abisay ni mithili ya nyota iliyozimika ghafla. Familia ya marehemu Abisay inahitaji kujipa ujasiri kwa kujua kuwa ameondoka baada ya kulitumikia taifa hili kwa hali na mali. Yatosha kusema , kazi ya Mungu haina makosa. Buriani Abisay Uronu Stephen…mapenzi ya bwana yahimidiwe…
SOURCE: Kenya's Daily Nation:
Nation reporters have counted 73 badly burnt bodies at the scene of a huge fire at a slum in Nairobi's industrial area.Police sources say the toll of the dead is likely to breach 100 following fire triggered after a oil leaking from a pipeline spilled into the Sinai slum.
"We are putting the number of dead at over 100, we are waiting for body bags to put the victims into," said Thomas Atuti, area police commander. The Kenyatta National Hospital (KNH) confirmed that 112 people were admitted there with third degree burns as of 1.30pm.The Sinai slums sit on top of a pipeline that feeds a fuel depot off Lunga Lunga road in Nairobi’s Industrial Area. NTV reporter Kaara Wainaina told Nation.co.ke that the fire covered a wide area in the slum. A detachment from the paramilitary General Service Unit (GSU) have cordoned off huge area affected by the fire and nearby roads have been closed to traffic. Nearby buildings were evacuated and office workers asked to move away from the area. Several ambulances were seen leaving the area ferrying away victims. They were taken to Mater Hospital and Kenyatta National Hospital (KNH).Many residents were caught up in the blaze, and an AFP reporter at the scene counted sco
Over 100 dead in Nairobi slum fire
Jifunze...
Usiku wa kuamkia leo Tanzania imejipatia mrembo wake atakayelishikilia taji hilo kwa mwaka mmoja ujao. Sarha Israel (katikati) amejinyakulia ushindi huo unaojulikana kama MIss Vodacom Tanzania baada ya kuwaangusha wenzake katika kinyang'anyiro hicho.
Picha : Sarha akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa Pili,Tracy Sospeter (kulia) na mshindi wa tatu,Alexia William mara baada ya kutangazwa usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar.
Kwa ushindi huo Sarha Israel anakuwa Vodacom Miss Tanzania 2011-2012 na kunyakua gari aina ya Jeep lenye thamani ya shilinngi milioni 72 lililotolewa na wadhamini wakuu kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania na Kampuni ya kuuza magari ya CFAO MOTORS ya jijini Dar es salaam Shindano hilo limemalizika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka Uganda Juliana Kinyomozi ndiye aliyekuwa akiwaburudisha wageni waalikwa katika hafla hiyo...
Take 5 Sarha.