Polisi nchini India wakishughulika na mtu mmoja ambaye wanamuona kimbelembele katika maandamano kupinga uchaguzi nchini humo. Hebu fikiria hadi akifika huko anakopelekwa atakuwa katika hali gani!
Ni hapa...
Jumla ya watu 103 hadi leo(J3) wameshakufa kwa mafua ya ndege nchini Mexico na wengine 1500 wanaendelea na tiba . Ugonjwa umeleta taharuki kubwa . Nchini Marekani nao umeingia . Imeshakuwa tabu, Japani kila kona wamejiandaa kuzuia wakikumbuka mafua ya ndege ya Dec. 2008 na jan.2009 pale mashamba yab kuku na ndege wengine yalipoteketezwa ili kuokoa maisha ya watu. Dalili ni homa , kipandauso, mafua-yanayosakama na kujisikia ndivyo sivyo.
Jijini Tokyo katika Bustani za Yoyogi leo (J2) kulikuwa na maonyesho maalum kwa ajili ya huduma za mbwa. Mabanda yaliyokuwa yakiuza nguo na vyakula vya mbwa yalifunguliwa na kila mtu alijimwaga kuwafanyia shopping. Kwa Japani kama ilivyo kwa nchi nyingi za Ulaya Mbwa na paka ni sehemu ya familia na huwa ana bajeti yake. Kuna Saloon zao ambako huogeshwa , kuchanwa manyoya yao na kupata tiba...na nyumba nyingine huwa mbadala wa watoto..Upooo!
Mama mmoja nchini Ujerumani amefumaniwa akifanya mapenzi na mwanawe wa kumzaa jambo lililoleta gumzo kubwa nchini humo . Mtoto mwingine wa mama huyo ndiye aliyewafumania na kutoa siri hiyo hadharani . Katika kuonyesha kuwa hakubaliani na tabia hiyo aliamua kuwapandisha kizimbani mama yake na ndugu yake huyo aliyemzidi mwaka mmoja ambao walitishia kumuua iwapo atatoboa siri hiyo nje.Mkasa huo ulianza baada ya mtoto mmoja wa mama huyo alipomfumania mama huyo akifanya mapenzi na mtoto wake mwingine.Kijana wa mama huyo mwenye umri wa miaka 18 aliyejulikana kwa jina la Michael alipigwa na butwaa asijue la kufanya baada ya kumkuta kaka yake anayemfuatia mwenye umri wa miaka 19 akila uroda na mama yao mzazi nyumbani kwao.Mama wa kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Karin alimtishia mtoto wake huyo kuwa atamuua iwapo atatoboa siri ya uhusiano wake huo na kaka yake.Michael kwa hasira aliwafungulia mashtaka mama yake na kaka yake kwa uhusiano wao huo haramu pamoja na kumtishia kumuua.Uhusiano wa mama huyo na mwanae unasemekana ulianza miaka minne iliyopita baada ya mama huyo ambaye aliwaacha watoto wake wakiwa wadogo walelewe kwenye nyumba za kulelea watoto kuamua kuwachukua watoto wake baada ya miaka 15.Mtoto mkubwa wa mama huyo anayeitwa Mark alitokea kumpenda mama yake mzazi na matokeo yake walianza uhusiano wa kimapenzi kisiri hadi hivi karibuni walipofumaniwa.Fumanizi hilo lililopelekea Michael kuwapandisha kizimbani mama yake mzazi na kaka yake limekuwa gumzo sana nchini Ujerumani.Kesi ya kutishia kuua inayowakabili mama na mwanae inaendelea kusikilizwa katika mahakama moja nchini humo
Nchini Afrika ya kusini kuna mjadala hivi sasa juu ya nani kati ya wake wa Jacob Zuma atatambuliwa rasmi kuwa ndiye mama wa taifa ,First Lady. Idadi ya wake zake inatajwa kuwa ni sita na watoto 18. Mamlaka iko mikononi mwake kuamua nani awe First lady. Huyu ndiye mke mkubwa wa Zuma lakini nafasi yake ni finyu sana kupata nafasi hiyo.
Sizakele Khumalo...Mke mdogo wa Jacob Zuma huenda akawa First lady...Hatihati hii inakujaje..Hebu mwangalie Jacob Zuma mwenyewe...
Zuma ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 67 ni dhahiri atatangazwa rais mpya wa Afrika Kusini kutokana na matokeo ya awali ya uchaguzi wa Afrika Kusini yanavyoonyesha.Mjadala upo kwenye kujua je Zuma atamchagua mke wake yupi kuwa mke wa kwanza wa rais First Lady wa Afrika Kusini au kama atamchagua binti yake ambaye yuko naye kila kona kuwa First Lady wa Afrika Kusini."Nawapenda wake zangu na najivunia watoto wangu" ndilo jibu analolitoa Jacob Zuma anapoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na mjadala huu.
Taarifa zinasema kwamba Zuma ameoa wake sita na mke wake wa mwisho alimuoa mwezi january na idadi ya watoto wa Zuma inakisiwa kuwa kati ya watoto 13 na 22.Kutokana na Zuma kujulikana kama mpenda "dogo dogo" kuna uwezekano wa Zuma kuwa na wake wengine na watoto wengi ambao hawatambuliki rasmi.Zuma ambaye alitumia maisha yake ya mwanzoni kama mfugaji wa Ng'ombe na Mbuzi katika Zululand, anafaidika na mabadiliko ya sheria nchini Afrika Kusini ya mwaka 1998 ambayo yaliruhusu na kuzitambua ndoa za kijadi na ndoa za wake wengi.Zuma alishatamba awali kuwa yeye yuko wazi kwenye masuala ya ndoa sio kama viongozi wengine duniani ambao huwa na wake wengine kwa siri.
Ni wake wanne wa mzee Zuma wanaotambulika kisheria, mmojawapo alikuwa Kate Mantsho Zuma ambaye alijiua mwenyewe mwaka 2000. Mke mwingine wa Zuma alikuwa Nkosazana Dlamini Zuma ambaye ndoa yao ilivunjika lakini wamekuwa karibu sana kutokana na kwamba bi Dlamini ndiye waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini kwa sasa na inasemekana Zuma anaweza akamuacha aendelee na wadhifa wake huo.Nompumelelo Ntuli, 34, aliyefunga ndoa na Zuma mwaka jana na anayeishi katika nyumba yake ya asili mjini Zululand inasemekana kuwa ndiye atakayekuwa chaguo la Zuma kuwa First Lady wa Afrika Kusini.
Mke wa kwanza wa Zuma aliyefunga naye ndoa mwaka 1973 Sizakele Khumalo, hapewi nafasi kubwa ya kuwa First Lady pamoja na Zuma kumuelezea kama mke wake mpendwa anayemuona pia kama dada yake katika harakati za ukombozi.
Binti wa Zuma, Duduzile anaweza akanyakua majukumu ya First Lady kirahisi kutokana na kwamba muda wote yuko bega kwa bega na baba yake na anahesabika kama mdau mkubwa wa karibu wa Zuma.
Bibi mmoja nchini Australia mwenye miaka 83 ameuonyesha ulimwengu kuwa hata kama ana umri mkubwa unaweza kuumudu mwili wake.. Bibi huyu anayejipenda kimavazi huwaacha watu midomo wazi kwa uwezo wake wa kupiga pushap na kujipindapinda uwezo pamoja na kuwa na umri huo ambao wazee wengi wa umri wake hawawezi na hulalamikia maumivu ya viungo vyao kwa kisingizio cha umri . Bibi huyu ni mwalimu wa yoga na anaitwa Bette Calman. Anayoyafanya , hata baadhi ya vijana ..pengine hata wewe unayeisoma habari hii huwezi kufanya nadanganya? Hebu jaribu...
JZ…. ndilo jina maarufu kuliko jina lake la asili huko Afrika ya Kusini. Jacob Gedleyihlekisa Zuma Raisi wa ANC sasa anajiandaa kuingia Ikulu ya Afrika kusini. Hii inafuatia ushindi uliopatikana kwa Chama cha ANC katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika majuzi na kuwashinda kwa kiasi kikubwa wapinzani wake ; Bi Hellen, Mzungu raia wa Afrika ya kusini anayewakilisha chama chenye ushawishi na watu weupe nchini humo, Askofu Mvume Dandala kutoka chama kilichojitenga na ANC, Mangosutu Buthelezi, wa Inkata na vyama vingine zaidi ya 100 ambavyo havijulikani sana. Zumo pamoja na kusakamwa na kashfa ameibuka kidedea na sasa anauhakika wa kupitishwa na Bunge kuwa Raisi...Lakini Huyu Jacob Zuma ni nani hasa?
Zuma alizaliwa mwaka 1942 na alilelewa na mama wa kambo huko Kwazulu Natal na kwa hakika amejisomea somea tu hadi akafikia kuwa na elimu kubwa na wala si madarasa katika mfumo maalum.. Alijiunga katika ANC akiwa na miaka 17 kwa lugha nyingine kwa miaka 49 amekuwa mwanachama wa ANC na baadaye akajiunga na mapambano chini ya Umkhonto We Sizwe, mwaka 1962.
Makaburu walimkamata na akapatikana na hatia na akahukumiwa kwenda jela miaka kumi katika gereza la mateso kisiwa cha Robben akiwa na Mzee Nelson Mandela.
Alipotoka alitumia sauti yake na hamasa zake za kiukombozi kuwaweka sawa watu wa Afrika ya Kusini ili kujikomboa. Jacob Gedleyihlekisa Zuma; Kama walivyo viongozi wengine wa kabila la kizulu ana wake wengi ameshaoa mara nne rasmi . Alimuoa Sizakele Khumalo mwaka 1973 na baadaye akamchukua Nompumelelo Ntuli mwaka 2008.
Baadhi ya wake zake wengine ni Thobeka Mabhija , aliyewahi kuwa Waziri wa mambo ya nje wa Afrika ya kusini Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye waliachana mwaka 1998 na Bi. Kate Mantsho Zuma aliyekufa mwaka 2000 .Mtu huyu ni mpiganaji katika maisha ya kawaida na yale ya kisiasa. Ameshakabiliwa na kesi mbaya ya ubakaji ambayo ilikuwa dhahiri kumfanya achanganyikiwe, aone aibu , akate tamaa na kujitoa katika ulingo wa kisiasa lakini bila shaka alitumia kanuni za wapiganaji kuwa kukata tamaa wakati wa mapambano ni dhambi kubwa.
Jacob Gedleyihlekisa Zuma mwenye miaka 66 alihusishwa na ufisadi wa Dola za kimarekani Billioni 5 katika masuala ya ununuzi na usafirishaji wa silaha lakini hatimaye akatoka .
Mtu huyu ana sifa za kipekee sana katika medani za kisiasa. Anaweza kujichanganya katika makundi ya watu , akaimba na kucheza. Anazungumza lugha ya walala hoi na ana ushawishi mkubwa kiasi kwamba watu wanmuamini kuwa sasa ndio mwisho wa matatizo yao. Ameonyesha tofauti kubwa na mtangulizi wake Thabo Mbeki , kwani Mbeki ni mkimya na mwenye aibu kidogo na huchukua uangalifu sana katikamaamuzi yake.
Pengine kesi iliyokuwa na msisimko mkubwa ni ile ya ubakaji , akituhumiwa kumbaka menzi wake aliyekuwa na virusi vya Ukimwi. Lakini alijitetea kuwa walikubaliana na kwamba alijua kuwa ana virusi na ndio maana baada ya kitendo hicho akakimbilia bafuni kuoga …na kweli alipopimwa alikutwa mzima wa afya.. Sasa anajiandaa kuingia Ikulu…..baada ya safari ya mabonde na milima .Na kweli chochote kinaweza kutokea katika maisha.
Mzee mmoja wa Kichaga ambaye alikuwa mkali sana kwa binti yake anaamka asubuhi na kutaarifiwa kwamba binti yake ana mimba!
Mzee wa Kichaga: "Aisee we Manka,nakwenda kazini,nikirudi leo ni lazima uniambie ni nanikafanya uchafu huu"Akafoka na kuondoka kuelekea ofisini.Mchana anapigiwa simu na Mama Manka nakuambiwa kwamba yule jamaa aliyempa mimba bintiye yuponyumbani anamsubiri kwa mazungumzo!Mzee anachukua panga lake na kulinoakabisaaa kwa ajili ya kwenda kumteketeza mwanaharamu huyo.Kufika nyumbani mambo yanakuwa hivi:
Kijana aliyempa mimba binti: Mmmh!!, Mzee ni kweli mi ndiye nimempa mimba binti yako, na kusema kweli sina mpango wa kumuoa.Lakini akizaa mtoto wa kiume nitakupa Millioni hamsini na nyumba ya ghorofa eneo la Kariakoo kisha nachukua mtoto.Akizaa mtoto wa kike nakupa Millioni kumi na duka Sinza! Lakini je mzee, ikitokea bahati mbaya mimba hii ikaharibika itakuwaje?
Mzee wa Kichaga akajibu : Aisee babaangu itabidi tu umpe mimba nyingine,hakuna jinsi! Duh....
Milima ya uluguru mkoani Morogoro imekuwa vipara siku hizi , maji yaliyokuwa yakitiririka kutoka kileleni yameacha na ubaridi katika mji wa Morogoro umeanza kupungua ...ni uharibifu wa mazingira. Wataalamu wanasema kuwa Misitu ya milima ya Uluguru imepungua kutoka hekta 30,000 mwaka 1950 hadi hekta 20,000 mwaka huu na hii imetokana na vitendo vya uchomaji moto katika milima ya Uluguru. Amesema kupungua kwa misitu katika milima hiyo kunatokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchomaji moto, kilimo cha migomba pamoja na bangi na kwamba katika kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka huu zaidi ya hekta 200 za misitu katika milima hiyo zimeteketezwa kwa moto. Milima ya Uluguru ni muhimu hasa kutokana na kuwa na makazi ya viumbe mbalimbali ambapo wengine baadhi yao hawapatikani sehemu yoyote duniani. *(Picha na Int.P. Peter Omari)
Wananchi wa Afrika Kusini watapiga kura Jumatano ya tarehe 22 April na chama tawala cha African National Congress kimemsimamisha mgombea wake Jacob Zuma Zuma kiongozi mwenye historia ya kusisimua ,mpiganaji na asiyeogopa anatabiriwa ushindi pamoja na ushindani mkubwa uliopo. Ana sifa nyingi lakini kwa wapiga kura anaonekana kuwapa matumaini makubwa walalahoi na amekuwa akiwakosha sana wapiga kura kwa uimbaji wake wa tambo na kujionyesha kuwa ni mtoto halisi wa sauzi. Fuatilia uhamasishaji wake kwenye kampeni zake zilizokamilika leo Jumatatu , April ,20.
Hii ni hatari! Kuna tukio la kusikitisha limetokea hivi karibuni huko kaskazini mwa Texas , nchini Marekani . Mwanamama mmoja alikuwa katika boti jumapili moja , akachukua baadhi ya soda za kopo za Cocacola na kuweka kwenye friji iliyopo katika boti hiyo huku akila wikiend na baadaye akazinywa kwa raha zake.
Siku iliyofuata ya jumatatu alipelekwa hospitalini na kuwekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na siku ya jumatano akafariki dunia. Uchunguzi wa kitiba umeonyesha kuwa alikufa kutokana na ugonjwa wa Leptospirosis. Hii ilitokana na kunywa ile soda bila kutumia glasi na uchunguzi umeonyesha kuwa Alikula na mkojo wa panya uliogandiana juu ya mdomo wa kopo uliomsababishia ugonjwa huo wa Leptospirosis ambao unaua kama umeme. Mkojo wa panya una sumu inayoua na ndio maana inashauriwa kusafisha sehemu ya juu ya vyakula na vinywaji vya makopo kabla ya kula au kunywa. Makopo haya hujazwa kwenye maghala na kupelekwa madukani bila kusafishwa. Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa makopo ya soda yana mabaki ya sumu yaliyo hatari kuliko vilivyo vyoo vinavyotumika na watu wengi ambavyo vina germs na bacteria wengi tu. Kuwa mwangalifu…
Mwanamke mmoja nchini India amejipatia umaarufu na kuwa gumzo nchi nzima kutokana na hali yake ya kutoa machozi ya damu kila anapolia. Rashida Khatoon mkazi wa mji mmoja kaskazini mwa India, amewashangaza hata madaktari kwa hali yake hiyo ya kutiririka machozi ya damu kila anapolia.Kwa siku mwanamke huyo humwaga chozi la damu mara kadhaa. "Sisikii maumivu yoyote, badala ya machozi ya kawaida, damu zinapotitirika ni kitu cha kushangaza" alisema mwanamke huyo ambaye amekuwa gumzo sana nchini India.Viongozi wa dini wa India wanadai kwamba mwanamke huyo ni miujiza toka mungu. Kutokana na umaarufu mkubwa aliojizolea mamia ya watu wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa mwanamke huyo kujishuhudia wenyewe kwa macho yao. Wageni hao wamekuwa wakimmiminia mwanamke huyo na familia yake zawadi kadhaa kila wanapomtembelea nyumbani kwake.
Siku moja Miji ya Tanzania itakuwa kama hivi , hakuna kukatika umeme mwaka mzima. hapa ni Shijuku jiji lililo ubavuni mwa Shibuya jijini Tokyo. Nishati ya nyuklia haiongopi lakini inataka nidhamu ya maisha. Pengine wasiwasi wangu ni kuwa lini tutaacha kwanza kuiba mafuta ya transfoma kabla ya kufikiria mengine?