Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, April 30, 2010

Madaktari nchini India wanaumiza vichwa wakimfanyia uchunguzi babu wa miaka 83 ambaye anadai hajakula wala kunywa maji kwa zaidi ya miaka 70. Tangia wameanza kumfanyia uchunguzi babu huyo siku nane zilizopita babu huyo hajakula, hajanywa kitu chochote na wala hajaenda chooni.
Madaktari wa jeshi la India wanamfanyia uchunguzi babu mwenye umri wa miaka 83 ambaye inadaiwa hajakula wala kunywa kinywaji chochote kwa zaidi ya miaka 70.





Wanajeshi wanaamini kuwa wakigundua siri inayomfanya babu huyo awe hali wala kunywa chochote, wataweza kuwapa njia wanajeshi kukaa muda mrefu bila kula wala kunywa.
Babu huyo mwenye nywele ndefu na ndevu ndefu aliyejulikana kwa jina moja tu la Jani, amekuwa akifanyiwa uchunguzi masaa 24 na timu ya madaktari 30 katika hospitali ya mji wa Ahmedabad magharibi mwa India.Jani anafanyiwa uchunguzi kwa wiki tatu kuthibitsha kuwa hali wala kunywa kitu chochote na tangia uchunguzi huo ulipoanza aprili 22 mwaka huu babu huyo hajakula, hajanywa kitu chochote na wala hajaenda haja ndogo wala kubwa.Video kamera mbili zimewekwa kwenye chumba chake zikifuatilia miendendo yake yote huku kamera moja imekuwa ikimfuatilia kila anapoenda kwa masaa 24."Matokeo ya uchunguzi wa mwili wake yatatupa mwanga jinsi binadamu wanavyoweza kuishi bila chakula wala maji", alisema Dr G. Ilavazahagan, anayeongoza uchunguzi wa babu huyo."Hii itatusaidia kuvumbua njia za kuwasaidia watu kuishi muda mrefu bila kula wa kunywa wakati wa majanga makubwa ya asili kama vile matetemeko ya ardhi".
"Dhumuni la kumfanyia uchunguzi Jani ni kujua anawezaje kuzihifadhi energy zinazohitajika na mwili wake", alisema Dr Ilavazahagan.
Jani ambaye huvaa nguo nyekundu akiwa na hereni kwenye pua yake ameishi maisha yake yote kwanye kijiji cha Charod kwenye jimbo la Gujarat.Jani anaelezea siri yake ya kuishi miaka mingi bila kula wala kunywa ni baraka alizobarikiwa na miungu ya kihindi tangia alipokuwa ana miaka minne.

Posted by BM. on Monday, April 26, 2010

Jana ilikuwa siku maalum ya vivazi na bidhaa mbalimbali zinazohusiana na mbwa hapa Japani kwa mwaka huu wa 2010. Pitisha macho.!


Duka la nguo mpya za mbwa ...hapo kuna dizaini mpya zilizoingia mjini ...wenye mbwa shurti wawafikishe hapo kupata kivazi na bei yake si umeiona ...badilisha sasa (Tsh. 14,500/) na (Ksh.1500/)

Du Jamaa wako kwenye kibaiskeli wanapunga upepo...!

Sare Sare ....Jezi yetu...

Mapambo kichwani...

Posted by BM. on Monday, April 26, 2010

Maisha Kitendawili kweli....!Ukisha sikiliza hiyo

sasa sikiliza mfululizo wa mahojiano haya , bila shaka uatabakia na maswali ambayo majibu yake yatapatikana baadaye ...lakini bila shaka utajifunza kitu.

Posted by BM. on Saturday, April 24, 2010


Mahakama mjini Kigali imemwachia huru kwa dhamana mwanasiasa Victoire Ingabire aliyekamatwa Jumatano kwa tuhuma za kupinga kutokea mauaji ya kimbari na kushirikiana na makundi ya kigaidi.Mwanasiasa huyo alirejea nchini Rwanda kutoka ushamishoni kwa lengo la kugombea kiti cha urais katika uchaguzi utakaofanyika Agosti mwaka huu. Bi Ingabire ameagizwa kuripoti serikalini mara mbili kwa mwezi. Pia ametakiwa asiondoke mjini Kigali. Ingabire anaongoza chama cha kisiasa cha Unified Democratic Forces. Watetezi wa haki za binadamu wanailaumu serikali ya Rwanda, ingawa Rais Paul Kagame amekuwa akinukuliwa akisema serikali yake inaongoza kwa misingi ya haki na haitaruhusu baadhi watu kuvuruga amani.
Mjue Victorie; Victoire Ingabire Umuhoza born 3 October 1968 is a Rwandan politician. She is the Chairperson of the Unified Democratic Forces (UDF) a coalition of Rwandan opposition parties with a large base of active members in Rwanda, Europe, United States of America and in Canada.
Married and a mother of three, she trained in commercial law and accounting and graduated in business economics and corporate management in the Netherlands. Victoire worked as an official of an international accounting firm based in the Netherlands where she was in charge of its accounting departments in 25 branches in Europe, Asia and Africa. In April 2009, she resigned from her function to dedicate herself to a political career and to prepare her return to her homeland and, as the head of her political party, to contribute to rebuilding of her country.
On her arrival in the country, to honor the victims of Tutsi genocide, she visited the Gisozi Genocide Memorial Centre. In her speech, she stressed that those who committed Tutsi Genocide as well as those who committed other war crimes and crimes against humanity should be brought before the courts of justice .
However, her critics argue that her speech, condemning the Genocide committed against Tutsi and denouncing other serious crimes against humanity and war crimes, was perceived by some as minimizing or denying the Tutsi genocide

Posted by BM. on Saturday, April 24, 2010


Technical Difficulty
Pope Benedict XVI reads a speech during a welcoming ceremony at the Malta International airport in Luqa, Malta

Posted by BM. on Saturday, April 24, 2010


Mordor;

Lightning streaks across the sky as lava flows from the volcano on Iceland's Eyjafjallajokull glacier.

Posted by BM. on Friday, April 23, 2010

Mahojiano na Mwanamuziki Fresh Jumbe na Shirika la Utangazaji la Japani -NHK hivi sasa yanasikika kupitia mtandao wa http://www.nhk.or.jp/nhkworld/swahili
unaweza kuingia hapo na angalia Siku ya Alhamisi 2010-04-22. Hutajutia muda wako kufuatilia maelezo yake...karibu.

Posted by BM. on Thursday, April 22, 2010



Sikiliza kwa makini mawaidha ya Raisi Mstaafu Benjamini Mkapa...bila shaka utajifunza!

Posted by BM. on Thursday, April 22, 2010



Unasemaje mdau baada ya kumsikiliza President...

Posted by BM. on Thursday, April 22, 2010


Soreee; Swali lako halina jibu!

Posted by BM. on Thursday, April 22, 2010

Eneo la Harajuku katikati ya jiji la Tokyo kuna duka linauza bidhaa za utamaduni za Afrika mashariki hususan kutoka nchini Kenya. Tulitembelea duka hilo na kuzungumza na mmliki wake anayeonekana kwenye picha hapo juu.Muziki unaoburudisha dukani humo ni wa Kiswahili..imefurahisha kwa kweli.



Director wa Maasai Market , na watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani Bi. Fatma Mohamed na Bw. Edward Kadilo nje ya duka hilo lilopo jijini Tokyo...


Da Fatu, Mkurugenzi wa Maasai Marketi na miye...picha ya ukumbusho

Posted by BM. on Wednesday, April 21, 2010


Imekamilika...

Posted by BM. on Monday, April 19, 2010

Tumepokea mtu muhimu katika Ulimwengu wa Muziki , Fresh Jumbe Mwinyi katika studio zetu za NHK hapa TOKYO leo. Tuklikuwa na mazungumzo na baadaye mahojiano studio kwa ajili ya vipindi vya moja kwa moja na mtandao wa intaneti.Mwanamuziki huyu ana historia na hazina kubwa ya habari za muziki katika eneo letu la Afrika Mashariki hususan Tanzania. Kwa vijana wa zamani watakumbuka Enzi ya Dar International, Msondo , Sikinde, OSS , Bicco Stars ambako aliziimbia bendi hizo na kuacha tunzi zake.Mahojiano yetu pia yataanza kusikika kwa mfululizo kuanzia siku ya Alhamisi kwa wasilikilizaji wa Afrika Mashariki na kati na kwa njia ya mtandao pia wa; www.nhk.or.jp/swahili . Unaweza pia kumtembelea katika mtandao wake binafsi kupata habari za karibuni kwa kubofya neno Fresh Jumbe hapo kulia kwako kwenye orodha ya mitandao rafiki ama bofya; www.freshjumbe.com


Ndani ya studio za NHK jijini Tokyo leo Jumatatu kabla ya mahojiano....

Kiongozi mwandamizi wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani Yuko Asano (Kushoto), Mwanamuziki Fresh Jumbe (kati) na nami Kulia mara tu baada ya mazungumzo yetu studioni.


Bi. Yuko asano, Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili Redio Japani aliyejiunga wiki hii kutokea KBC Kenya Mr. Kadilo na Fresh Jumbe Mwinyi (Kulia)


Nje ya studio tukakumbana na flash...Pwaaa!


Nukta chache kabla Fresh hajaondoka B/H.

Posted by BM. on Monday, April 19, 2010


Kocha Mchezaji Nico Nyagawa akipokea kombbe la Ubingwa wa Vodacom -Bara baada ya kuiburuza Dar Young African Magoli 4-3. Mkabidhi Kombe Prof. Juma Kapuya, Waziri wa Kazi na ajira. Kulia Raisi wa TFF.Habari ndio hiyo...


Machozi ya furaha; Mwenyekiti wa Simba Hassan Dalali . Alihemewa.


Mchezaji Hillary Echessa akishangilia baada ya kufunga goli la nne la ushindi. Pembeni kulia ni mchezaji Emmanuel Okwi.
(Picha zote na wanalibeneke waandamizi.)

Posted by BM. on Sunday, April 18, 2010

Nimesoma kwenye ; www.wavuti.com post hii nikagushwa sana na kumbukumbu nyingi zimenijia kichwani. Si mbaya tukajikumbusha tulikotoka. Siku moja nami nitaandika kile ninachokikumbuka nilipoingia kwa mara ya kwanza RTD kwenye Jengo la "Utangazaji barabara ya Nyerere jijini Dar Es salaam.", enzi hizo. Asante sana Da Subi na Issa Michuzi na mdau Monsignor. Wenye shauku ya kusoma habari za watangazaji wa zamani wanaweza kubofya hapa ; www.issamichuzi.blogspot.com


(Picha kwa Hisani ya Kiluvya Pub, Kibaha)Hapo ni studio za BBC Bush House London, Bro. Charles Hillary Nkwanga akiwa na mtangazaji Waziri Hamsin wakiwahoji wadau masuala ya soka . Karibu yako upande wa mbele (Kushoto) ni Mwenyekiti wa Kiluvya Pub kibaha(www.kiluvyaspub.blogspot.com) na mdau mwingine wa soka Israel Saria katika kipindi cha Ulimwengu wa soka -BBC

Posted by BM. on Saturday, April 17, 2010


Jana Ijumaa katika miji mingi ya Japani kulikuwa na kibaridi kikali sana. Ilishangaza kidogo kwani kipindi hiki kinatarajiwa kuwa cha uvuguvugu kuelekea kwenye joto lakini jana mambo yakabadilika. Kama unavyoona kwenye picha mkazi mmoja wa Hakone-machi, mkoa wa Kanagawa akiondoa barafu iliyoanguka mbele ya nyumba yake. Barafu ilidondoka maeneo mengi kwa viwango tofauti.kibaridi lawama , naongopa?

Posted by BM. on Saturday, April 17, 2010


Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro akimuangalia mtoto mdogo akijitahidi kutembea kwa kutumia mguu bandia katika mji Mkuu wa Haiti ,Port au Prince ambako alikwenda huko kwa ziara fupi.

Posted by BM. on Saturday, April 17, 2010


Askari wa jeshi la Marekani huko Marjah , kusini mwa Afghanistan wakiwa katika mazoezi ya asubuhi kabla ya kupata chai. Jeshi si lelemama.

Posted by BM. on Saturday, April 17, 2010


Bi. Imelda Marcos alipokuwa akiwa mbele ya jeneza lililo na mwili wa mumewe Dikteta wa zamani Ferdinand Marcos aliyekufa mwaka 1989 na mwili wake kuhifadhiwa vizuri katika jeneza la kioo , huu ni mwaka wa 21 sasa. Ni utamaduni wa aina yake.

Posted by BM. on Saturday, April 17, 2010


Waziri Mkuu wa Uingereza Godown Brown (katikati) , mkewe Bi Sarah kushoto na Mkurugenzi wa huduma za Afya leeds Yeadon huko Uingereza Sam Prince wakifunguliwa mlango kiaina kuingia katika ofisi za Afya. Aina hii ya ufunguaji mlango imenifurahisha.

Posted by BM. on Saturday, April 17, 2010

Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.1 kwenye kipimo cha Richter limetokea hivi majuzi huko Yushu katika jimbo la Tibeti mkoani Qinghai, China. inasemekana takriban watu 800 wamefariki na maelfu wamejeruhiwa.
Sehemu zilizokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi ziko kwenye mashariki ya Uwanda wa juu wa Qinghai na Tibet wenye mwinuko wa zaidi ya mita 4400 kwenye usawa wa bahari, hivyo kazi ya kuwatafuta na kuwaokoa watu waliofunikwa chini ya vifusi inakabiliwa na taabu nyingi kubwa.Fuatilia hali ilivyokuwa na ilivyo sasa kwa njia ya picha.


Makasisi wa dini za kijadi wakiwa mbele ya jengo la bweni lao katika mji wa Jieng, eneo la Yushu , Qinghai huko China.

Hali halisi ndio hii...

Picha iliyopigwa muda mfupi baada ya tetemeko hilo.


Maafa makubwa.


Utafutaji wa manusura ; kazi inapokuwa ngumu.


shughuli za uokozi zinaendelea kufanywa na vikosi mbalimbali kikiwemo hiki cha wanajeshi.

Posted by BM. on Saturday, April 17, 2010


Moja ya neema iliyopo Tanzania ni huu mlima Kilimanjaro. Au unasemaje mdau!

Posted by BM. on Thursday, April 15, 2010


Kundi la Al-Qaeda limetishia kuwaua mamia ya watu watakaohudhuria mechi kati ya Kundi la Al-Qaeda linaloongozwa na Osama Bin Laden limetishia usalama kwenye kombe la dunia nchini Afrika kwa kuahidi kufanya shambulizi la kigaidi litakaloua mamia ya watu wakati wa mechi kati ya Marekani na Uingereza Marekani na Uingereza kwenye kombe la dunia nchini Afrika Kusini mwezi juni mwaka huu.Kundi linalojiita Al-Qaeda in the Islamic Maghreb, limetoa taarifa kwenye website likisema kuwa watu wa kujitoa mhanga wakiwa na mabomu ambayo si rahisi kugundulika kwenye mitambo ya ulinzi, wako tayari kujilipua kwenye mechi kati ya Uingereza na Marekani kwenye uwanja wa Rustenburg juni 12 mwaka huu.Kundi hilo liliweka taarifa hiyo kwenye tovuti inayoitwa "Mushtaqun Lel Jannah" (Njia ya kuelekea peponi).
"Al-Qaeda watakuwepo kwenye mechi za kombe la dunia", ilisema taarifa hiyo ya Al-Qaeda."Litakuwa ni jambo la kufurahisha sana wakati wa mechi kati ya Marekani na Uingereza ikirushwa live kwenye luninga wakati sauti ya mlipuko itakaposikika kwenye majukwaa na kuugeuza uwanja mzima juu chini", iliendelea kusema taarifa hiyo ya Al-Qaeda.Uingereza na Marekani zipo kwenye kundi moja la C pamoja na Algeria na watapimana ubavu juni 12 kwenye uwanja wa King Bafokeng mjini Rustenburg unaochukua watazamaji 44,500.Maafisa wa Marekani wamesema kuwa vitisho hivyo vya Al-Qaeda vinachukuliwa kwa uangalifu mkubwa katika kuhakikisha usalama kwenye fainali hizo za kombe la dunia zitakazochukua mwezi mmoja.Maafisa wa usalama wa Uingereza wamekataa kusema chochote.Mwezi oktoba mwaka jana, maafisa wa usalama wa Afrika Kusini walisema kuwa wamefanikiwa kulizima jaribio la shambulizi la kigaidi lililokuwa limepangwa lifanyike wakati wa fainali hizo.Iliripotiwa kuwa maafisa wa Afrika Kusini kwa kushirikiana na maafisa wa Marekani walifanikiwa kuwatia mbaroni watu wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa Al-Qaeda nchini Somalia na Msumbiji ambao walikuwa wakijiandaa kufanya shambulizi wakati wa fainali za kombe la dunia.Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kuwa jumla ya polisi 44,000 watalinda usalama kwenye fainali hizo.

Posted by BM. on Sunday, April 11, 2010


Waziri Mkuu mstaafu John Malecela na Mkewe Anna Kilango Malecela..

Posted by BM. on Sunday, April 11, 2010


Halafu...

Posted by BM. on Friday, April 09, 2010


Vijana wawili wa Kijapani , Hideki Ozawa (Kulia kwangu ) Na Nishiyama (Kushoto)wamerejea majuzi kutoka Tanzania. Wamenipa simulizi za kusisimua zinazohusu Nyumbani hasa kwetu Masasi. Wakanidokeza kuwa hata Samaki nchanga walimla. Ukitaka mahojiano kamili ingia kwenye mtandao wa NHK -swahili service uone jitihada za wenzetu na wanavyoizungumzia nchi yetu;
www.nhk.or.jp/nhkworld/swahili

Posted by BM. on Friday, April 09, 2010



Mzee Mabula, mwenye miaka 76,Akionyesha kaburi la mjukuu wake lililo chini ya kitanda chake ambaye aliuwawa kikatili kutokana na ulemavu wake wa ngozi. Mjukuu wake huyo albino aliyeuwawa Mariam Emmanuel, katika chumba kilichopakana na chake alimzika ndani ya nyumba kutokana na tishio la kurudi kwa wauaji hao kuja kumalizia viunga vingine vilivyobakia , pamoja na ukweli kuwa tayari alikwishauwawa na kuzikwa. Inauma sana.. (kwa hisanai ya Getty Images)

Dada mmoja mwenye ulemavu wa ngozi akiwa nyumbani kwa bibi yake Ukere Mkoani Mwanza , Tanzania. Eneo hilo lina matukio machache ya mauaji ya albino ikilinganishwa na maeneo mengine.

Posted by BM. on Friday, April 09, 2010
Labels:BM

Hapa ni shibuya , Katikati ya Jiji la tokyo nilikopata mlo wangu wa mchana leo. Nyama za kuchomwa kiaina..



a href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXnLNb2I-XRS6tsF75qQe-JfnhboJ18XHBB5_1m7Oik-cFmSlTKs_Ytq7aVCBQeqJA6fDjZvfZaJ5AihJ2n7RdH5EZ7K7sw69iXFc3n7iV6opby9oz10xRJKx7vfiag15TG3k-TOXmBpU/s1600/PICT0013.JPG">a


Waturuki na Wa-Syria wamechangamkia sana biashara ya vyakula hapa Tokyo. Leo "J1" nilivinjari katika eneo la Shibuya nikakutana na menyu hii maarufu. yale maandalizi tu ya nyama yamenifurahisha. Ila nimechukia kitu kimoja "No Mfupa" Why???



Mmmh ntamu. JIna la msosi huu silijui lakini bila shaka kuna nyama, mkate , wali Mayonaiz ,nyanya na viambato vingine

Posted by BM. on Friday, April 09, 2010

Afrika Kusini iko katika maandalizi ya mwisho mwisho tayari kuanza kwa fainali kombe la dunia juni mwaka huu 2010, takriban miezi miwili kuanzia sasa. Kwa viwanja wamejiandaa vilivyo. Hebu tuchungulie walichokifanya.

Jiji la Pretoria ...linalotazamiwa kupokea wageni zaidi katika mashindano hayo.

Moses mabhida Stadium, Durban , Kwazulu Natal.

Nelson Mandela stadium Port Elizabeth...


City Soccer Stadium , Johannesburg.

Posted by BM. on Friday, April 09, 2010


Hebu tumia dakika moja tu kubaini hapa wapi...?

Posted by BM. on Friday, April 09, 2010


Waziri Mkuu wa tanzania Mh. Mizengo Pinda akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili nchini Vietnam akitokea hapa Japani. tayari PM na ujumbe wake wamesharejea nyumbani.