Katika hatua inayoonekana wa rushwa inaogopewa nchini Japani kwa kiasi kikubwa ,Mwenyekiti wa Baraza la mji wa Kawasaki, mkoani Fukuoka amejiua juzi jumapili na kuacha kijikaratasi kikilaumu uchunguzi uliofanywa na Polisi kuhusiana na tuhuma za ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi unawahusisha wafuasi wake, kwamba kulikuwa na harufu ya rushwa .
Kulingana na taarifa za Polisi wa eneo hilo, Hidemi Morimoto mwenye miaka 67, dhahiri anaonekana amejiua mwenyewe kwa kuchoma mkaa fulani bandia katika gari lake katika jiji la Tagawa Fukuoka, akakosa hewa na kufa.Hidemi amekuwa akihojiwa na wachunguzi kuanzia siku ya Jumatano iliyopita hadi Ijumaa baada ya wafuasi wake wawili walikamatwa kwa tuhuma za kuwapa chakula wapiga kura kinyume cha sheria wakati wa kampeni za baraza la halmashauri ya Tagawa mwezi wa April.
Kulingana na familia yake , katika maandishi aliyoyaacha nyumbani kwake , Morimoto alikabiliwa na mahojiano makali na alilazimiswa kuwatambua watuhumiwa. Aliamua kujiua kabla ya kuhojiwa tena juzi Jumamosi. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo hapo nyumbani kwake…
Katika tukio jingine Mwili wa kijana mmoja wa kiume umepatikana chini ya jengo alilokuwa akiishi katika eneo la makazi ya watu huko Kobe juzi Jumapili. Polisi wanasema leo jumatatu kuwa kuwa kijana huyo anaonekana amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani. Mtu mmoja aliyepita katika eneo hilo aliwataarifu polisi jana Jumapili baada ya kuhisi kuna kijana mmoja amelala fofofo chini ya jengo la nyumba hiyo iliyopo eneo la Suma jana jumapili saa 11 alfajiri . Polisi walifika hapo na kuuchukua mwili wa kijana huyo hadi hospitalini na madaktari wakathibitisha kuwa alishafariki dunia.
Kijana huyo mwenye miaka 16 ambaye jina lake linahifadhiwa alikuwa anasoma katika shule ya sekondari ya juu ya gakuin hapo Kobe.Kulingana na maelezo ya Polisi , hakuna dalilizozote katika mwili wake zinazoonyesha kuwa alishikwa au kusukumwa na mtu yoyote na inakisiwa kuwa alijirusha kutoka ghorofa ya tano ya jengo alilokuwa akiishi na wala hajaacha ujumbe wowote.Ndugu wa kijana huyo waliokuwa wamelala wakati tukio hilo linatokea wamesema kuwa hawajui sababu yoyote iliyomsukuma kijana huyo kujiua na hakuna kilichobainika , shuleni wala nyumbani, polisi wamewaambia waandishi wa habari.
Ni hapa...
Kizazi cha Lwambo Makiadi...Kijana wa zamani vipi unasemaje!
Hayati Madilu..
Leo katika studio za Shirika la Utangazaji -NHK tulikuwa na mwanamuziki wa kijapani Bi. Erico Mukoyama,maarufu kwa jina la Anyango ambaye hucheza chombo cha kiasili cha kijaluo kwa kuchanganya na muziki wa kisasa.
Mdada huyu aliwahi kukaa nchini Kenya na anaongea kwa ufasaha Kijaluo na Kiswahili. Alikuwa akinipa taarifa ya safari yake ya Ufaransa na maandalizi ya Albamu yake yenye nyimbo 15 na pia tulirekodi kipindi cha Sauti ya Anyango pamoja.
Anyango ni mtayarishaji mwenzangu wa kipindi hicho kinacholengwa kuwachambua wanamuziki wa Kijapani hususan ambao wana mapenzi na bara la Afrika. Unaweza kumuangalia Anyango mwenyewe akiwa mzigoni .
Kipindi cha sauti ya anyango husikika kupitia Idhaaa ya Kiswahili ya Redio Japani kila jumamosi ya wiki ya pili ya mwezi na unaweza kuvisikiliza vipindi hivi na vingine vinavyotangazwa na NHK -Swahili kwa kubofya hapa:
www3.nhk.or.jp/nhkworld/swahili au kuia kwako kuna maneno NHK WORLD Swahili ...column ya Marafiki . Bonyeza hapo utaingia kwenye ukurasa huo.
Baada ya kazi tulipiga picha ya kumbukumbu....
Mmoja wa wawakilishi wa Tanzania katika jumba la bigbrother huko Afrika Kusini, bibie Locus amejikuta akitolewa nje baada ya kushindwa kuzuia ghadhabu yake kwa kumzaba kibao mshiriki mwenzake kutokafrika Kusini, baada ya kutupana maneno kwa dakika kadhaa. unaweza kusikiliza hapo na kuamua nani mkosaji!
Mdada huyu nchini Marekani amefanya ukatili zaidi kwa kumuua kwa kumbanika kwenye Microwave mtoto wake mchanga wa mwezi mmoja eti kwakuwa mpenzi wake alikuwa haamini mtoto huyo ni wake.
China Arnold mwenye umri wa miaka 31 wa Ohio nchini Marekani amenusurika kuadhibiwa kunyongwa lakini amehukumiwa kutumikia maisha yake yote yaliyobakia jela bila ya kupewa nafasi yoyote ya kupata msamaha wa rais. China alikuwa na mzozo na mpenzi wake ambaye alikuwa akihoji mtoto mchanga aliyezaliwa na China kama ni wa kwake kweli au mwanaume mwingine.
Mzozo huo ulipopamba moto China alimchukua mtoto huyo aliyekuwa na umri karibia mwezi mmoja na kumweka kwenye Microwave na kuiwasha kwa dakika zaidi ya mbili.Waendesha mashtaka walisema kuwa kwa kukusudia kumuua mtoto huyo, China alimweka kwenye Microwave mtoto huyo mchanga wa siku 28 na alipoiwasha Microwave hiyo mtoto huyo alifariki kwa kuungua vibaya sana.
Ripoti ya madaktari ilisema kuwa mtoto huyo wa kike aliyepewa jina la Paris Talley alifariki ghafla baada ya joto la mwili wake lilipofikia kati ya nyuzi joto 43 Celcius. "Alifariki kwasababu aliwekwa kwenye joto kubwa sana, alikuwa kama amebanikwa", alisema daktari mstaafu Dr. Marcella Fierro.
Akitoa hukumua ya kesi hiyo jaji wa kesi hiyo alimhukumu China kwenda jela maisha akisema kuwa ukatili alioufanya ni zaidi ya ukatili wa mtu aliyeua kwa risasi au kwa kutumia kisu.
Chanzo; mtandao wa Nifahamishe
Mwishoni mwa vita ya pili ya dunia...1945, Majeshi ya Marekani yalidondosha mabomu ya nyuklia katika miji ya Hiroshima na Nagasaki... Picha hiyo ya juu inaonyesha sehemu ya jengo bomu hilo lilidondoshwa , nami nilibahatika kufika hapo!....inatisha ...Wajapani wamejitahidi kuhifadhi kumbukumbu ya tukio hilo!
Aliyekuwa mkuu wa shirika la fedha duniani, Dominique Strauss-Kahn, amepewa dhamana na jaji katika mahakama moja mjini New York. Hii ni baada ya kushtakiwa rasmi kwa kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli moja, kwa jina la Nafisatou pichani.
Strauss-Kahn hatimaye apewa dhamana
Awali, Strauss-Kahn alijiuzulu kutoka kwa wadhifa wake kama Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF).Mawakili wa Bw Strauss-Kahn walisema yeye ni mtu mwenye heshima na kwamba hawezi kutoroka.Mawakili wake wamemwambia jaji kuwa mkuu huyo wa zamani wa shirika la fedha duniani (IMF) yuko tayari kuwekwa chini ya kifungo cha saa 24 nyumbani na pia avalie kifaa cha elektroniki kitakachochunguza mienendo yake.Mke wa Strauss-Kahn ambaye alikuwa mahakamani wakati wa kesi hiyo, alijitolea kutoa dhamana ya dola millioni moja.
Baada ya kipindi kifupi cha mapumziko jaji alikubali dhamana hiyo, lakini pia akapendekeza kutolewa kwa bima ya dhamana yake ya dola millioni tano.Bali na kutoa dhamana, jaji aliamuru awekewa mlinzi mmoja aliyejihami wakati wote na pia asalimishe stakabadhi zake za kusafiri.Strauss-Kahn sasa ameshtakiwa rasmi baada ya kikao cha baraza la uchunguzi, kilichohudhuriwa na mwanamke mwenye umri wa miaka 32 anayemtuhumu.Baraza hilo liliamua kuwa Strauss-Kahn ana kesi ya kujibu.Mwanamke aliyemfungulia mashataka ni raia wa Guinea, Magharibi mwa Afrika. Strauss-Kahn amekanusha mashtaka yoke dhidi yake.Anatarajiwa kufika tena mahakamani Juni sita, ambapo atatarajiwa kusema kama anakubali mashtaka dhidi yake au la.Ikiwa, Strauss-Kahn, mwenye umri wa miaka 62, atapatikana na hatia, atahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela.
Mke wa Strauss-Kahn ni mwandishi habari na mtangazaji wa televisheni, Anne Sinclair. Ana watoto wanne kutoka ndoa zake mbili za mwanzo. Ukiacha lugha yake ya Kifaransa, anazungumza pia kwa ufasaha Kiengereza na Kijerumani na pia ana ujuzi mzuri wa Kihispania na Kiarabu.
Tayari albamu ya mwanamuziki wa siku nyingi Mbilia Bel iko mtaani...moto wa kuotea mbali kwa wale wanaopenda muziki wa Rhumba ya kiafrika...moja ya nyimbo zilizopamba album hiyo ni huu hapa... Bofya hapo chini:
Baada ya hapo unaweza kusikiliza nyimbo zinazotamba huko DRC kwenye video kwa kubofya kwenye vi-box vidogo vinavyojitokeza.
Umeiona tofauti na za kwetu!, Zetu zinafaa bila shaka na hizi pia zinafaa au!
Maelfu ya wakazi wa dar es salaam leo walishiriki katika mazishi ya Shekhe Yahaya Hussein aliyefariki jana . Mazishi yalifanyika katika makaburi ya Tambaza .
Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Sheikh Yahya Hussein aliyezikwa katika Makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Sheikh Yahaya Hussein alifariki dunia katika hospital ya Mount mkombozi iliyopo maeneo ya kinondoni.
Vyanzo mbalimbali vya habari vinasema kwamba Sheikh Yahaya alipelekwa hospitalini hapo ghafla leo asubuhi ktokana na tatizo la moyo na amefariki mnamo mida ya saa tano kasoro asubuhi ya leo.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu huyu peponi, Ameen.
Unaweza kuona kazi alizokuwa akizifanya wakati wa uhai wake kwa dakika kama saba hivi hapo chini:
Bingwa wa Olimpiki katika mbio za masafa marefu za Marathon Mkenya Samuel Wanjiru aliyeaga dunia ameacha kizungumkuti kwa kile alichokifanya akatika uhai wake.
Wanjiru alikumbana na mauti baada ya kuruka kutoka kwenye chumba chake cha ghorofa moja eneo la Nyahururu, mkoa wa Kati wa Kenya.
Idara ya polisi imethibitisha kifo hicho na kusema uchunguzi umeanzishwa ili kubainisha sababu za kifo hicho.Mwanariadha huyo alishinda medali ya dhahabu katika mbio za Olimpiki mwaka 2008 mjini Beijing, kwa kuweka muda wa 2:06:32. na kuandikisha rekodi ya kuwa Mkenya wa kwanza kushinda mbio za marathon kwa upande wa wanaume .Wanjiru pia alikuwa bingwa wa ulimwengu katika misururu ya mbio za marathon maarufu kama world marathon ,ajors kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2010.
Wanjiru pia aliweka rekodi ya mbio za kilomita 21 kwa kuandikisha muda wa dakika 58:33.Mwezi DeSemba mwaka uliopita Wanjiru alifikishwa mahakamaNI, kwa mashtaka ya kutishia kumwuua mkewe, kumjeruhi mlinzi wake wa nyumbani na pia kumiliki bunduki aina ya AK-47 bila idhini ya serikali.
Mapema mwaka huu Wanjiru alipata ajali mbaya katika barabara inayotoka Nairobi kuelekea Nyahururu, hatua iliyomfanya kujiondoa kutoka kwenye mbio za London Marathon
Mkuu wa fuko la fedha la kimataifa -IMF ,Domonique Strauss-Kahn amekamatwa New York
tayari kukabili mashtaka ya kumsumbuwa na kutaka kumbaka mhudumu mmoja wa kike wa hoteli mjini New-York. Mkuu huyo umri wa miaka 62 alikamatwa akiwa ndani ya ndege ,katika uwanja wa ndege wa John F. Kenndy,muda mfupi kabla ya kuondoka kuelekea Paris.Mhudumu huyo wa kike wa hoteli ndie aliyetowa malalamiko kwamba Dominique Strauss-Kahn alitaka kumbaka. Duru zinasema Dominique Strauss-Kahn aliondoka haraka hotelini na kusahau simu yake ya mkono na vitu vyake vyengine.Mfaransa huyo,aliyekuwa akipewa nafasi nzuri ya kukiwakilisha chama cha kisoshalisti uchaguzi wa rais mwakani ,alipangiwa kukutana na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani hii leo mjini Berlin kuzungumzias mgogoro wa fedha wa Ugiriki.
Wakili wa Domonique Strauss-Kahn William Taylor amewataka watu wasitaharuki kuhusiana na kisa hicho cha kukamatwa mkuu huyo wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF. Jana jumapili Dominique Strauss Kahn alipangiwa kufikishwa mbele ya jaji mjini Manhattan.
Duh!
Unaweza kujifunza kitu ,hebu sikiliza!
Katika mitaa ya Kinshasa , Kongo DRC , Kuna vikundi vinavyofanya vyema katika muziki lakini havijajulikana sana nje ya nchi hiyo . Leo navitambulisha vikndi viwili. Kikundi cha kwanza hapo juu kimetunga wimbo wa kulaani wanaobaka wanawake nchini humo. Kumbuka kuwa vitendo hivyo vimetapakaa sana hasa maeneo yenye vita.
Kundi jingine hapo chini likiwa kwenye mazezi ya nguvu kabla hawajaibuka na bendi...unaweza kubofya hapo ukapata spices za Kikongo !shughuli ni watu!
Msanii mmoja mwenye jina kubwa nchini Japani, Miyui Uehara, mwenye miaka 24, amefariki dunia juzi alhamisi asubuhi baada ya yeye mwenyewe kujinyonga katika nyumba anayoishi katika eneo la Meguro jijini Tokyo.
Polisi amesema kuwa jirani yake aliuona mwili wake mlangoni kwake akiwa aejifunga skafu na kamba shingoni wkati wa saa nane usiku na ndipo tu aliita watu wa huduma za dharura. Uehara alikimbizwa hospitali ambako madakari walidhitisha kuwa alikwishakufa.
Kwa mujibu wa mtandao wa kihabari wa japantoday , Uehara ni mmoja wa watoto 10 waliozaliwa nyumba moja anayetokea mkoa wa Kagoshima, jambo ambalo si la kawaida sana hapa Japani( Watototo wengi katika familia moja) na kipaji chake kilijibainisha wakati alikuwa akifanya kazi ya uhudumu katika klabu moja ya starehe , wakati huo alikuwa na miaka 18.Hapo alianza kuonekana kwenye majarida ya wanaume akiyapamba kwa picha zake zilizowafanya wanaume wengi hususan vijana kuyanunua kwa wingi na baadaye alifahamika kama “Malkia” miongoni mwa mashabiki wake.
Uehara anamiliki blogi kama hii ya Mirindimo ambamo aliweka picha zake 'Bila kificho' na uchunguzi wa kipolisi unaonyesha kuwa aliutembelea mtandao huo mara ya mwisho saa 2 asubuhi siku ya jumanne ambapo alielezea huzuni kubwa aliyonayo kwa kutoweza kulipata penzi la Kweli.
Tukio la kushangaza na kusikitisha limetokea ndani ya Kanisa katika Parokia ya Vugu mkoani Kigoma, mwishoni mwa wiki iliyowaacha waumini na butwaa, baada ya Padri kumpiga makofi Bibi Kizee katikati ya ibada ya misa ya pili, akimtuhumu kuondoka na Sakramenti aliyoipokea madhabahuni.
Padri aliyefahamika kwa jina moja la Sabas, alifikia hatua hiyo wakati wa ibada ya Sakramenti, ambapo bibi huyo aliungana na waumini wengine kwenda kushiriki, lakini alipopewa kipande cha mkate, aliondoka nacho na kwenda kukila akiwa ameketi. Inaripotiwa kuwa kitendo hicho kilisababisha Padre Sabasi kusimamisha huduma hiyo ghafla, na kumfuata bibi huyo na kuanza kumpiga makofi.Waumini waliohudhuria ibada hiyo wameeleza kuwa ni mara ya kwanza kitendo hicho kutokea mkoani humo.
"Huyu ni mtu mzima, hivyo hakuweza kuvumilia kusimama na kukila kipande cha mkate na kuamua kukaa chini, Padri alitakiwa kumuonya kama alikuwa amekosea na siyo kumpiga, " alisema muumini mmoja mara baada ya kumalizika kwa misa hiyo.Padri Sabas alipohojiwa kuhusu kitendo hicho alidai kuwa alifikia uamuzi huo kutokana na muunini huyo kwenda kinyume na utaratibu wa kanisa hilo na kuongeza kuwa, alimwona muumini huyo akikiweka kipande hicho kwenye ziwa (titi) kwa imani za kishirikina.
Bi. Kizee huyo aliondoka mara moja baada ya ibada hiyo.
Kampuni moja ya vifaa vya elektroniki nchini Japani ya Pioneer hivi sasa inauza Spika za aina mpya kabisa ambazo hazihitaji kufungwa waya zinazojulikana kama -Kai-Tele-kun VMS-700-K.
Wireless speakers hizo zinazopokea mawimbi ya sauti kutoka kwenye Televisheni moja kwa moja zina uwezo wa ufanya kazi hata zikiwa katika umbali wa mita 30.
Kampuni hiyo inasema kuwa spika hizo zitawasaidia akinamama wanaotaka kusikiliza matangazo ya Redio ama ya TV wakiwa jikoni bila kulazimika kutandaza waya.Spika hizo kwa sasa zinauzwa hapa apani Yeni Elfu 20 ambazo ni takriban Shilingi Laki tau na Elfu 60 kwa pesa za kitanzania. ( I Yen~Tsh.18.00). Mauzo hayo yameanza hivi karibuni tu…
Alassane Ouattara has been sworn in as Ivory Coast president in a ceremony after months of political violence in the world's leading cocoa producer followed his victory in last November's elections.
Ouattara, 69, was sworn in at the presidential palace on Friday by the head of the Constitutional Council, Paul Yao N'Dre, watched by members of his government, the armed forces and the diplomatic community.
"It's the start of a new era of reconciliation and unity between all the daughters, and all the sons of our dear Ivory Coast," Ouattara said in a brief speech after taking the oath of office.
Ouattara has spent most of the last five months barricaded inside a hotel because Laurent Gbagbo, the country's longtime ruler who had lost the election, refused to cede office.He was surrounded by troops loyal to Gbagbo, who used the army to oppress the population. More than 1,000 civilians are estimated to have died in violence before Gbagbo was removed militarily last month.He is now under house arrest in a remote town 700km north of the country's largest city, Abidjan.
It was N'Dre who had refused to confirm Ouattara's win in the November 28 election.
N'Dre invalidated results from Ouattara strongholds in order to hand victory to Gbagbo. But on Thursday he said the court now accepted Ouattara had won the election.
Miyee nimeikubali, kazi nzuri...au unasemaje mdau!
Rais Barack Obama wa Marekani amekielezea kifo cha kiongozi wa al-Qaeda, Osama Bin Laden, kuwa ni "siku njema kwa taifa la Marekani," na kusema sasa dunia imekuwa mahala salama na pazuri zaidi.Nyumba ambako Osama bin Laden alikutwa na kuuawa huko Pakistan.
Bin Laden aliuawa katika shambulio lililofanywa na vikosi maalum vya Marekani kwenye nyumba moja ndani ya mji wa Abbottabad nchini Pakistan.Anaaminika kuwa ndiye mtu aliyeagizwa kufanyika kwa mashambulio yaliyotokea New York na Washington, Septemba 11 mwaka 2001, pamoja na mashambulio mengi kadhaa ya mabomu yaliyosababisha vifo.
Ilikuwa ndiye mtu anayesakwa zaidi duniani. Lakini maelezo yake katika orodha hiyo yamebadilishwa na sasa kuna sehemu inasomeka: "Amefariki".Vipimo vya DNA vilivyofanywa baada ya harakati hiyo vinaonyesha kwa uhakika wa asilimia "99.9%" kuwa mtu aliyepigwa risasi ni Osama Bin Laden, maafisa wa Marekani walieleza.
Maafisa wa wizara ya ulinzi wanaeleza kuwa alizikwa baharini baada ya kuswaliwa kwa mujibu wa taratibu za kiislamu kwenye meli ya kubebe ndege katika bahari ya Arabuni.
Marekani imeweka ofisi zake katika hali ya tahadhari kote duniani, ikiwaonya raia wake kuhusu uwezekano wa mashambulio ya al-Qaeda kulipiza kisasi kwa kifo cha Bin Laden.Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la CIA, Leon Panetta, amesema al-Qaeda kuna uwezekano mkubwa kujaribu kulipiza kwa yaliyotokea