Kwa hisani kubwa ya NTV-Kenya..
Ni hapa...
Tetemeko lenye ukubwa wa 6.9 kwa kipimo cha richa limetikisa pwani ya kusini ya jiji la Tokyo nasi katika jengo la utangazaji limetutikisa kwa muda wakati tukiendelea kurusha matangazo.Majengo yalitikiswa katikati ya Tokyo lakini kutokana na kuwepo kwa teknolojia ilionekana kama vile yakiyumba hivi.
Hakuna majeruhi wala uharibifu ulioripotiwa hadi sasa na idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa hakuna tisho la kuwepo kwa mawimbi ya tsunami kwahiyo hali inatarajiwa kuwa shwari.Mtetemo huo ulitokea saa sita na dakika 25 mchana huku kitovu cha tetemeko hicho kikitajwa kuwa kilikuwa karibu na visiwa vya Ogasawara takriban kilometa 800 na lilitokea kilometa 480 chini ya ardhi . Ingawa vipimo vya idara ya hali ya hewa ya Japani inasema kuwa tetemeko lilikuwa na ukubwa wa 6.9 , ile ya Marekani ilisema ilikuwa na ukubwa wa 6.6.
Polisi wa Yokohama katika mkoa wa Kanagawa wametoa taarifa rasmi kuhusiana na taarifa za kukamatwa kwa watanzania na madawa ya kulevya . Wamesema kuwa wamewakamata watanzania wawili baada ya kuthibitika kuwa walimeza dawa za kulevya aina ya Heroin katika matumbo yao.Wakwanza aliyetajwa kuanguka kwenye mikono ya wajapani ni Machenga Machenga Ally mwenye umri wa miaka 33 na Ally Mohamed Husein (37) ambao wanadaiwa kumeza kilogram 1.3 za heroin zenye thamani ya fedha za Japani zipatazo Millioni 78 kulingana na Polisi wa mkoa wa Kanagawa. Yeni Millioni 78 ukitaka kujua kwa fedha ya Tanzania zidisha (78,000,000 x 17.1)'hesabu zangu'.
Polisi hao wa Mkoa wa Kanagawa walisema kuwa Watanzania hao walikamatwa jumanne iliyopita ya Nov.23 wakiwa na kapsuli 5 kila mmoja zikiwa na gramu 13 za heroin zikiwa nyuma ya gari walilokuwemo. Awali Machenga Ally alimeza Kapsuli( capsules) 25 zenye ukubwa unaofanana na huo na tarehe 24 siku ya jumatano walilazwa hospitalini ambapo Machenga Ally alivitoa kwa njia ya haja kubwa kapsuli 10 na Husein kapsuli 40 Polisi wamesema kuwa watuhumiwa hao ambao wamekiri makosa yao waliondoka Tanzania tarehe 19 Novemba siku ya Ijumaa na kuingia Japani Novemba 22. Kilichowaponza kulingana na maelezo ya Polisi ni kuwa wenyeji wao katika eneo walilofikia alitoa taarifa Polisi katika mkoa huo wa Kanagawa kuwa jamaa zake walikuwa wakilalamika kuwa wanaumwa sana tumbo jambo liliwatia mashaka, hatimaye kila kitu kikawa hadharani.
Hata hivyo kuhusika ama kutohusika kwao kutafahamika pale watakapofikishwa mahakamani na ukweli ukabainika. Kwa sasa wanabakia kuwa watuhumiwa...Magazeti mengi ya Japani hii leo yamekuwa yakitoa fursa watu kutoa maoni yao na mmoja alikuwa akiulizia Tanzania iko wapi....huyu vipi!
Je huu ni Uungwanaaa?
LAHASHA huu si uungwana.
Ni hapa.....
Picha ya kumbukumbu; (L-R) Mh. Balozi Sijaona, msikilizaji wetu kutoka Tanzania Ras Franz na Kulia Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania hapa japani Mr. Francis Mossongo
Mapenzi kwa taifa langu...
Ilikuwa bahati na fahari kubwa kumtembelea balozi wa Tanzania hapa Japani Mh. Salome Sijaona ofisini kwake...sote tulioenda tulifarijika...ni mtu watu kwa taarifa...
V-alama ya amani pembeni mwa mnara ambao ni kumbukumbu ya mtoto aliyefariki dunia kutokana na minunurisho ya nyuklia aliyedhamia kutengeneza sanamu za ndege Korongo 1300 kwa kutumia karatasi kuhimiza amani....alikufa kabla hajatimiza lengo lake. ukionyeshwa V maana yake amani siyo nanihii!
Safari ya kisiwa cha Miajima ambako kuna hekalu la Kibudda lilijengwa tkriban miaka 1400 iliyopita , watoto walikuwemo na alama yao ile ile.
Urithi wa somo la amani kwa kizazi kipya.
Askari wa miamvuli wa JK..
1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mathias Chikawe
2. Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu: Stephen Wassira
3.Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia
4. Ofisi ya Makamu wa Rais – ( Muungano): Samia Suluhu
5. . Ofisi ya Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa
6. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi
7. Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu
8. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Huruma Mkuchika
Naibu: Aggrey Mwanri
Naibu: Kassim Majaliwa
9. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo
Naibu: Gregory Teu
Naibu: Pereira Ame Silima
10. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha
Naibu: Balozi Khamis Suedi Kagasheki
11. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani
12. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi
13 . Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi
14. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu: Benedict Ole Nangoro
15. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Naibu: Charles Kitwanga
16. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka Naibu: Goodluck Ole Madeye
17. Wizara ya Maliasili na Utalii Ezekiel Maige
18. Wizara ya Nishati na Madini William Mganga Ngeleja 1. Adam Kigoma Malima
19. Wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli
Naibu: Dr. Harrison Mwakyembe
20. Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu
Naibu: Athumani Mfutakamba
21. Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami
Naibu: Lazaro Nyalandu
22. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa
Naibu: Philipo Mulugo
23. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Hussein Mpanda
Naibu: Dr. Lucy Nkya
24. Wizara ya Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga
25. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba
Naibu: Umi Ali Mwalimu
26. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Emmanuel John Nchimbi
Naibu:Dr. Fenella Mukangara
27. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel John Sitta
Naibu Dr. Abdallah Juma Abdallah
28. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe
Naibu: Christopher Chiza
29. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya
Naibu: Eng. Gerson Lwinge
Asubuhi ya saa mbili na robo August 6, mwaka 1945 ilikuwa siku mbaya sana kwa wajapani pale majeshi ya Marekani yalipoamua kudondosha bomu la maangamizi katika miji ya HIROSHIMA na NAGASAKI hapa Japani. Hii ikiwa ni mara ya kwanza na haijafanyika tena katika dunia hii. Bomu hilo limedondoshwa mita 600 tu kutoka kitovu cha Jiji la Hiroshima ambalo wakati huo uchumi wake ulikuwa ukikua kwa kasi...Fuatilia picha chache za kuanzia juu ya tukio hilo...
Safari na mgeni wetu Bw. Franz Ngogo ya kwenda Hiroshima iliendelea tena . Tulitumia usafiri wa treni ziendazo kasi zinazojulikana hapa japani kama Shinkasen(Pichani) Kilometa 300 kwa saa ...
Safari imeanza ....
'V' Alama ya 'Amani' kwa Wajapani, tulikutana na wanafunzi hawa waliokuja kutembelea eneo hili.
Inaelezwa kuwa watu takriban 140,000 walikufa kutokana na bomu hilo lililodondoshwa na Majeshi ya Marekani mwishoni mwa vita ya pili ya dunia.
Mabaki yanayohifadhiwa kwa ajili ya kumbukumbu ya kizazi kijacho....
Mbele kabisa mwa Jengo lililoteketezwa na bomu hilo ...
Bomu hilo lilikuwa na uzito wa tani nne liliangamiza eneo hilo kwa sekunde chache tu, na inaonyesha kuwa joto lililotokana na kuangushwa kwake lilifikia sentigredi elfu tano. Hebu fikiria ...kila kitu kiligeuka vumbi...Watu waliokuwa umbali wa Kilometa mbili kutoka hapo walipata madhara makubwa na ni wachache tu waliendelea kuishi na kufa baadaye...wachace mno wapo hivi sasa lakini wanaulemavu wa kudumu...
Paleeee ndipo tulipotoka palipodoswa bomu...
Jengo la makumbusho ya amani ya Hiroshima...
Mji wa Hiroshima kabla ya bomu kudondoshwa
Mji wa Hiroshima baada ya kudondoshwa kwa bomu la Nyuklia...
kwa kawaida Safari inaanzia katika jengo la makumbusho ili kupata maelezo ya kutosha kabla hujaenda pale lilipodondoswa... Mnara huu ni kwa ajili ya watu wote waliokufa katika tukio hilo...na wale wanaende;lea kufa hadi sasa kutokana na mnunurisho (radiation) ya bomu la atomiki... Chini hapo kuna box la jiwe lililohifadhi majina zaidi ya Elfu tano. Eneo hili watu walitapatapa kabla ya kukata roho kutokana na kiu...na ndio maana ukawekwa mfereji wa maji kama ishara ya kuwapumzisha katika makazi yao ya milele bila kiu.
Baada ya pilika pilika za mchana tulikwenda katika Chuo Kikuu cha Fukuyama kusakata Kabumbu , ikanikumbusha enzi zangu nilipokuwa stricker hatari sana na hapo pia nilikutana na mashabiki wenzangu wa 'Wekundu wa Msimbazi' hapo chuoni tukapiga picha ya Ukumbusho... a< href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgl_cIUPahbQTOR9PjnRgqxE723sM5Q7dhLgB7Nzl6q5tdM07GsmSS_WPs7vdAE-jM4d4_12t2j14wsQhxOzGPlDGS4WrthwQIoJ4otgCccDBl8bKOSZVrq9BRhvPknDiFBlOIV4j7RAUc/s1600/DSC01138.JPG">
Mgeni wetu naye akakumbukia enzi yake...yeye ana miliki timu huko Tarime ...timu ya watoto wa kijijini kwake..ilikuwa movuu nzuri...
Penalti....Nilipanchi ukatoka nje ..lakini du, mwili mzito kiwango kimeshuka na umri tena. Imenikumbusha enzi zangu ya UMISETA wanaokumbuka nilikuwa nikitinga nane na golini wakati fulani...
Nilipopiga ngumi mpira na kutoka nje tukawa marafiki....
Hii ni crew nzima ya wanahabari wa Redio na TV , chini ya NHK World tunaoambatana na msikilizaji huyu kila mahali ...Mteja ni mfalme...
Mmoja wa wasikilizaji wa Redio Japani -Idhaa ya kiswahili Franz Manko Ngogo , mkazi wa Tarime kule Tanzania amepata fursa ya kutembelea Japani baada ya kushinda shindano la insha ya maadhimisho ya miaka 75 ya NHK World. Yeye ni miongoni mwa washindi watatu kati ya 1300 walioandika insha hiyo kote ulimwenguni. Washindi wengine wanatoka Indonesia na Iraq. Jana tulikuwa katika jiji la Yokohama ambako alimtembelea Prof. Akira Miyawaki wa kituo cha kimataifa cha Ikolojia na baadaye akatembelea maduka yanayouza bidhaa kwa bei moja tu ya Yeni mia moja ambayo ni sawa na shillingi elfu moja za Tanzania.
Tupo njiani tunakwenda Hiroshima kuona sehemu bomu la atomiki lilipodondoshwa na nitakuletea picha zaidi ya ziara yake hiyo hapa. Anatarajiwa kuondoka J2 kwenda nyumbani. Unaweza pia kufuatilia ziara hiyo kwa kubofya hapo kwenye mtandao wa NHK WORLD kulia kwako .
Franz katika mahojiano na wanahabari..Kulia ni mmoja wa wakuu wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK Kaori Noteakirekodi matukio.
Pozi katika moja ya viunga vya Yokohama...
Tafakur jadidi...
Pozi na prof. Akira Ofisini mwake ...Mtu huyu ni maarufu sana duniani , habari zake za kina nitakuandikia baadaye...
Mwanamuziki wa kizazi kipya Mwanafalsafa anatamba na kibao chake hicho Unanitega! ambacho kinavuma hivi sasa. Ukisikiliza kwa makini utasikia gitaa linalofuatiza taratibu mashairi , hilo linapigwa na Pauline Zongo (pichani)
...mwanamuziki mwenye sauti tamu sana ambaye awali aliwahi kupigia TOT. Fuatilia wimbo huo , au mdundo maana umri ndio kigezo cha ladha...Take 5...Mwanafalsafa...
Serikali ya Tanzania inajiandaa kujenda barabara ya lami itakayopita katikati ya hifadhi ya taifa ya Serengeti. Baadhi ya wanamazingira wanasema kuwa hiyo itaharibu uasili wa hifadhi hiyo na kuvuruga utalii ingawa wengine wanasema kuwa hiyo itaongeza kipato cha utalii na kuinua maisha ya watu wa eeo hilo na mikoa ya Mara na Arusha inayohitaji sana barabara ya lami katika eneo hilo.
Mdau Charles Ngereza...anaungana na wanaosema barabara hiyo ni muhimu...mie niko kati kwa kati weye je?
Kiongozi wa upinzani nchini Myanmar, Aung San Suu Kyi ameachiwa huru leo na uongozi wa kijeshi wa nchi hiyo. Uongozi wa kijeshi nchini Myanmar umemuachia huru kiongozi wa upinzani nchini humo, Aung San Suu Kyi. Magari maalum leo yaliwasili katika nyumba ya kiongozi huyo iliyoko pembezoni mwa ziwa na polisi waliondoa vizuizi pamoja na senyenge.
Katika kipindi chake cha kukaa Kizuzini Suu alilazimika kuzunguka ndani ya Seng'enge na kukaa chini ya mti nje ya nyumba yake hadi wakubwa walipoamua kumtoa nje kwa shinikizo la jumuia ya kimataifa.
Suu Kyi aliusalimia umati wa wafuasi wake wapatao 1,000 ambao walikuwa wamekusanyika katika lango la kuingilia kwenye nyumba hiyo. Mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel, ametumikia kifungo cha nyumbani kwa takriban miaka 21. Akiwa katika hali ya kujiamini Bi. Suu aliongea na waandishi wa habari;
Haijajulikana bado nini anakipanga kukifanya kiongozi wa kijeshi nchini humo Generali Than shwe (Pichani )kwa mara nyingine tena , ambaye kila kukicha humzulia jambo Suu na kumuweka kizuizini.
Wimbo huo ukisikika siku imeanza..Kila asubuhi ....RTD, KBC ya enzi hizo Lazimaa waanze nao!
Mh. Free Man Mbowe amechaguliwa na chama chakle kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni....
Zito Kabwe Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni...(CHADEMA). Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo ni Mh. Tindu Lisu. CUF wamesema kuwa nao wanaanzisha kambi yao Bungeni, tutasubiri ufafanuzi wa Mh. Makinda, Spika juu ya jinsi kambi hizo zitakavyofanya kazi..
Mh. Anna Makinda(Pichani)amechaguliwa na kuwa Spika Mpya wa Bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo kuvivaa viatu vya Mh. Samweli Sita ambaye alipunguzwa na Kamati kuu baada ya kura za wajumbe wa kikao hicho kutotoshelezwa. Makinda amemshinda Marando kwa kura nyingi kama ilivyotarajiwa .
Mh. Sita akiapishwa na Mh. Makinda..kuwa mbunge mwaminifu wa bunge hilo.
Katika bunge lilopita Bi Anna Makinda alikua Naibu Spika ambapo Mheshimiwa Samwel Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki alikua Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyu ni spika wa kwanza Mwanamke tangu Tanganyika na hatimaye Tanzania ilipopata uhuru...
KAMATI KUU LEO IMEPENDEKEZA MAJINA MATATU YA WANA CCM WATAKAOGOMBEA NAFASI YA USPIKA KATI YA WAGOMBEA 13 WA CHAMA HICHO WALIOJITOKEZA. MMOJA WAO NDIYE ATAYETEULIWA KUSIMAMA KUGOMBEA BAADA YA KUPITISHWA NAO NI MH. ANNA ABDALLAH,MH. KATE KAMBA NA MH. ANNA MAKINDA.
Kamati Kuu ya CCM ikijadili majina ya watu wanaowania Uspika ...
Wagombea wakisubiri zamu ya kujieleza kwenye Kamati Kuu ya CCM...
Mh. Samweli Sita akitoka baada ya kuhojiwa na kamati Kuu ya CCM...
Mh. Anna Makinda
Mh. Anna Abdallah...
Mh. Kate Kamba...
MAJINA YA WANAOWANIA UNAIBU SPIKA YANATAKIWA YAFIKE OFISI ZA BUNGE KESHOKUTWA NOVEMBA 15, 2010.
KATIBU MKUU WA CCM YUSUF MAKAMBA AMESEMA SASA HIVI KWAMBA KAMATI KUU YA CCM IMEAMUA KWA MAKUSUDI KUMPA NAFASI MWANAMKE KUONGOZA MOJA WA MIHIMILI MITATU YA NCHI KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA JAMHURI YA MUUNGANO.