Wadau...
Tafadhani baada ya picha mbili tatu za matukio mbalimbali , Nimekuandalia toleo maalum la mkutano wa watanzania na Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda kwa njia ya Picha. Hivyo teremka chini Taratibu ukutane na picha hizo.
Bofya hapo kwenye ARCHIVE mwezi March uone picha zote kwa wakati mmoja.
Ni hapa...
Mamlaka za usafiri wa treni nchini Japani imeanzisha kampeni za kuwakataza watu kujipodoa wakiwa ndani ya treni kwakuwa pilika pilika hizo zinawakera watu wengine.Nchini Japani ni kawaida ndani ya treni kukuta wadada wakijipura kwa kupaka wanja, kunyoa nyusi , kupanga rangi za mdomo na nakshi nyingine sasa mabango yamewekwa kwenye vituo vya treni kuwa ni; "NO".
Muziki wa vijana wa zamani; Enzi za Och. First Moja One . Enzi hizo ukiingia ukumbini kila mtu anaimba kwa sauti wimbo unaopigwa ; hii sijui ilikuaje hisia au wepesi wa kushika maneno. Unasemaje ? Sec.Gen.Tanzanite -Mwombeki Jnr; upo?
Waziri Mkuu wa Japani Yukio Hatoyama akimkaribisha Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda Ofisini kwake tayari kufanya mazungumzo rasmi.(Life network)
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amemaliza ziara ya siku tatu nchini Japani ambapo Pamoja na mambo mengine alikutana na Waziri Mkuu wa JP, Yukio Hatoyama na Waziri wa mambo ya nje Katsuya Okada na kujadiliana nao masuala mbalimbali ya ushirikiano katika sekta za Miundo mbinu na Kilimo.Katika upande wa miundombinu Viongozi hao wametia saini mkataba wa mkopo ambapo Japani itaipatia Tanzania Yeni Billioni 7 kuimarisha mtandao wa miundombinu ya nyumbani, kama anavyoainisha Mh. Pinda.
Kwa hakika hapo alikuwa anamalizia kwa kuomba usaidizi wa ujenzi wa barabara kati ya Dodoma na Babati mkoani Manyara.
Baada ya hapo alijumuika na wananchi waliopo hapa katika mkutano uliofanyika kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku. Kwa WaTz-waliopo JP walio na picha za matukio ya ziara hii wanaweza kuzituma kwa njia ya email kwa; brmsulwa@yahoo.com ili ziwekwe ili wengine wapate kuona kilichojiri...karibu.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amesema kuwa Serikali ya Tanzania imewekeza kwa kiasi kikubwa katika jitihada zake za kubadili kilimo Tanzania na ndio lengo kubwa la ziara hii. PM pamoja na wajumbe wengine ameambatana na Waziri wa Kilimo Mh. Stephen Wasira na Katibu Mkuu Wizaraya Kilimo Zanzibar Dr. Mohamed.Katika kueleza imani ya Tanzania juu ya Mpango huo uliopewa jina la "Kilimo Kwanza, Mh. Pinda"........
Ilikuwa fursa pia ya kumkabidhi Waziri Mkuu Mh. Pinda zawadi za nyaraka na vipeperushi kutoka kwa Uongozi wa Shirika la Utangazaji la Japani-NHK.
href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjW_q3yc6fos-GhGI9o57huaDSxiOpIgGzWgdKAmhc13tIB0DFtUSWlXrjFmqicfjBFEKwAL5i9n9KNrhQgbxGoGInLJVbQwsCIN90BPwIY6jAT5vsk_2FeyVLFbTbqgeZk632qnN3lsTQ/s1600/PICT0032.JPG">
MEZA KUU; Kutoka Kushoto; Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Zanzibar Dr. Mohamed, Mh. Mwakipesile Rc Mbeya, Balozi wetu hapa Japani Mh. Salome Sijaona, Mwenyekiti wa Jumuia ya watanzania JP, Dr. Ally Simba , Mh. Mizengo Pinda PM, Mh. Stephen Wasira, Waziri Kilimo, Balozi Seifu Iddi Naibu Waziri Mambo ya Nje na Mkurugenzi wa Asia wizara ya Mambo ya Nje mwisho Kulia.
Da Mariam Yazawa na wadau wengine waliwakilisha...
Umakini mkubwa ulikuwepo mkutanoni...
Mawili matatu kutoka kwa Mwandishi wa Waziri mkuu Saidi Nguba, Ilikuwa kujuana hali.
Camera zinapogongana! take 5 da Matilda.
href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhGut3t_NKZDQ-YdEM_CxgZ66cBd8OXUvzeKlreHB7gxUd4yEPdeMaZ2_-BcN7Nb0AHY5yP5GIPkDTac_Ea9acXGWp7oS5ZotcEHvxyPix52_KBVL_y0j82FhV1GLvu8AQesAjtWWCTLsA/s1600/PM">
"Victory"
Uso kwa uso na Balozi mpya wa Tanzania hapa Japani Mh. Salome Sijaona...Tumefurahi kukutana naye...!
Comrade RNdesika
Ukumbi wa mkutano na Mandhali yake!
Waandamizi" Kila kitu kinaenda sawa"
href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjokiGRMtsrnOsIVfV355Gr-patMmXNM15qz6jPOaYQ6_9eBhSAqhQCvvyrIGQOoLIXZp9irDsu92FKDiDiA526O077l_4vNCcJSFnJ1Gq2JKxaBrk-TE8NO_maLQvqD9gCZkP0nIFSsQo/s1600/DSC_1560.jpg">
Benchi la ufundi"Mambo shwari hapa"
Shughuli watu "Imependeza "!
Tafakari ya wajumbe"Maswaliii!"
Tupamoja, wanachama !
Shwari tu!"Hakuna malalamiko"
Mkabala na kamera ya Mirindimo"Pwaa!"!
teh teh!"Kwakweli"
Nilikuwepo."Shahidi jicho"
Mkutano wa kimataifa ulio chini ya Umoja wa Mataifa unaozungumzia spishi zilizo katika hatari ya kutoweka umekataa maombi kutoka Tanzania na Zambia kufanya mauzo ya mkupuo mmoja ya pembe za ndovu.Hebu bofya hapo uangalie ujangili huu unavyofanyika , halafu rejea kwenye mada . Jee wewe ungekuwa na kura ya turufu ungeamuaje kuhusu suala la kuruhusu au kutoziruhusu Tanzania na Zambia kuuza shehena zake za pembe za ndovu? Kwanza fuatilia suala hili lilivyochukuliwa nchini Kenya , nchi iliyoishikia bango Tanzania na kuwezesha ruhsa hiyo kukosekana bofya hapo.
Uamuzi huo umetolewa Jumatatu kwenye mkutano wa mataifa 175 huko Doha, Qatar. Biashara hiyo ingelikiuka marufuku ya kitaifa iliyowekwa mwaka 1989 juu ya uuzaji wa pembe za ndovu ili kuwalinda tembo kutokana na uwindaji haramu. Jason Bell-Leask, afisa wa mfuko wa kimataifa wa wanyama pori alisema tamko hilo ni ushindi nadra kwa tembo.
Tanzania na Zambia walisema idadi ya tembo wao imeongezeka kufikia kiwango ambacho wanaharibu mazao na kuuwa watu. Wapinzani walisema nchi hizi mbili zimeshindwa kuzuia uwindaji haramu wa tembo na uuzaji haramu wa pembe za ndovu. Tanzania iliomba kibali cha kuuza hifadhi iliyopo ya pembe za ndovu zenye thamani ya dola milioni 20. Zambia pia iliomba ombi kama hilo kisha ilijitoa na kupendekeza uuzaji wa sehemu zingine za tembo. Lakini meno hayo yanapatikanaje/ Bofya hiyo video hapo chini'
Eneo la Shibuya , katikati ya Tokyo hapa Japani.
Kuna aina hii ya uvukaji wa barabara baada ya kuwaka taa za kijani ambapo pande zote huwaka taa za kijani kwa pamoja na magari husimama hivyo watu huvuka . Inasaidia kuepusha ajali kama zinazotokea nyumbani ambapo mtu anavuka huku kule nyekundu mara puuuu...hivi hii haiwezi kutekelezeka kule kwetu..?
Barabara inayopita katikati ya majengo ya Chuo Kikuu cha kilimo Tokyo...sehemu ninayokwenda.
Leo hapa kulikuwa na mahafali nami nilipita hapo na kufyatua chache kwa ajili ya mirindimo...
Chuo Kikuu cha Kilimo cha Tokyo hapa Japani
Kwa ndani..muonekano wake..
Wasomi hawa wametoka kuchukua Shahada zao mbalimbali za Kilimo , nikajipenyeza kupata picha ya Ukumbusho...ilikuwa safi ..tulifurahi na mabwana shamba wa Kijapani.
Shamba la mfano katika maandalizi ya mwisho mwisho , hapo utaalamu unazingatiwa kwa kiwango kikubwa...
Eneo la utafiti na Kilimo "shambani" hapa Tokyo ambapo uzalishaji unazingatia kanuni ya "mazao Mengi katika eneo dogo"
"Hodi zumbe!" Tafsiri yake ...Karibu katika makumbusho hayaya Chakula na Kilimo ya Kilimo. Maswaliiii..hamna!
Unapofika katika kituo cha Makumbusho ya kilimo "SUA" Tokyo utakutana na kitoweo hiki cha Picha.
Pembezpni wa "Jongwe" alama ya Makumbusho ya kilimo ya Chuo kikuu cha Tokyo.
Mkutano wa viongozi waandamizi wa Afrika unaohusu uongozi na vyombo vya habari.
Kwa hakika msimamo wa viongozi wetu hawa ungehamishwa kivitendo bila shaka Afrika ingekuwa mbali hii leo. Hebu msikilize Raisi Paul Kagame wa Rwanda, Waziri Mkuu wa Kenye Raila Odinga, Raisi Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa na mjumbe mwingine wa mkutano huo.
Mnyama duma (Jamii ya chui) aitwaye Reyna akipata matibabu ya meno katika kliniki ya wanyama huko Envigago, Colombia
Nancy Pelosi, Mwanamke shupavu nchini Marekani ambaye ana wadhifa wa Spika wa Bunge la Congress la nchi hiyo.
Victoria , Mke wa Mwanasoka maarufu duniani David Beckham (Picha ya chini) akitoka katika kliniki ya michezo ya Turku, nchini Finland ambako alimpeleka mumewe aliyeumia mguu siku chache zilizopita
David Beckham
Koffi Antonio Olomide na mwanamuziki ninayemkubali sana kwa ubunifu wake wa kutumia michanganyiko ya sauti na vikorombwezo vingi katika mirindimo ya muziki wake. Hebu fuatilia muziki huu unaokisifia kinywaji cha SKOL , amebadili muziki mara saba huku akifungamana na sauti tamu ya kike. Kwa wale wenye taste hii wata-enjoy wengine najua...wala!
Eneo la kihistoria la makaburi ya kifalme yameteketea kwa moto katika mji mkuu wa Uganda , Kampala. Jengo la nyasi eneo la kasubi linaloonekana katika picha limeteketea likiwa na kumbukumbu mbalimbali za kijadi pamoja na makaburi wa wafalme wa Buganda waliotawala katika himaya hiyo kwa karne kadhaa zilizopita. Hili pia ni eneo lilitumia kama nyumba ya ibada kwa wa buganda
Raisi Museveni alikwenda katika eneo hilo na akakumbana na watu waliojaribu kumzuia na ndipo Pilisi walipoanza kupambana nao kumpa njia Museveni na ndipo watu watatu walikufa hapo hapo. wanaoipinga serikali wanadai Serikali ya Museveni inahusika na kuchomwa moto kwa eneo hilo.
Polisi wa kutuliza ghasia kwa kufyatua risasi..
Historia inaonyesha kuwa Ufalme wa Buganda ulisitishwa mwaka 1963 wakati Uganda ilipopata uhuru wake lakini ulirudishwa tena mwaka 1993 ingawa sasa kwa ajili ya kumbukumbu ya kiutamaduni na wala si kisiasa.