Wakati huu dunia inabadilika na kiwango cha ufahamu kinakua kwa kasi sana wale jamaa wanaojiingiza kwenye hiyo inayoitwa Comedy , Masanjas, Jottyies na wenzake waangalie hii wanaweza kuambua kitu. Na wasomi wenye shahada za uzamifu na uzamili nao wasijiweke nyuma , hii inalipa...acha tu....haya angalia !
Maoni ....!
Ni hapa...
Vyakula vya kijapani vina ladha nzuri na za kipekee. Napenda leo nikuelezee staftahi au kifungua kinywa cha kiasili cha wajapani. Kwa mjapani halisi kabla hajatoka kwenda kwenye kazi zake, lazima apate mlo wa asubuhi uliotimia. Menyu hiyo huwa na vitu vifuatavyo;
1.Bakuli la wali lililo na ujazo wa wastani
2.Mnofu wa samaki wenye rangi nyekundu , samaki anayeitwa salmoni ambaye kwa kawaida ana chumvi kidogo na baadhi ya wajapani wanaondoa ngozi yake wakidai hawaipendi.
3.Achali yenye mchanganyiko wa matango, figili na bilinganyi. Huwa nhaivurugwi inakuwa vipande vidogoX2 , zinachovya tu kwenye maji ya moto.
4.Matunda yanayofanana na zambarau yakiwa katika hali ya uchachu..
5.Bakuli la supu ya miso . Supu ya miso hutengenezwa kwa njia mbalimbali lakini ile miye ninayoijua ni mchanganyiko wa mboga za majani na nyama inayowekwa kwenye mchuzi wa uyoga, karoti, viazi mviringo na samaki.
Miso
Viambato hivi huwa katika hali ya vumbi, huchanganywa katika maji. Mabamia yanaweza kuonekana yakielea juu ya supu hiyo na kuleta hali Fulani ya kupendeza. Kwa wageni wanaweza wasiielewe…inakuwa kama miti shamba hivi lakini wenyewe wana-injoiii!
6.Bakuli la maharagwe ya soya yaliyochachushwa
7.Na Kibakuli cha mwani (Maarufu kule Zanzibar) unavuliwa baharini . Huwa unawekwa na kuelea kwenye kibakuli chenye maji moto
Mlo umetimia….Maswalii!
Vipi! unawaza nini!
Kila fani ina undani wake. Nidokeze tu kitu....Ukiwa mwandishi wa habari na ukapewa jukumu la kupiga picha matukio yanayofuatana na yanayofanana , na picha hizo pengine unahitaji kuzichapisha kila siku ili wasomaji wazione unahitaji ubunifu na umakini wa hali ya juu. Pia yule anayefuatiliwa na kamera lazima naye ajue jinsi ya kukurahisishia kazi yako kwa kukupa kitu kipya...Hivyo ndivyo anavyofanya Dr. Jakaya Kikwete.Na si upande huo tu hata kwenye utangazaji pia. Hotuba ikiwa ni ile ile , pozi ni zile zile , Maikrofoni yako utaihamisha ili kupata kitu kipya...
Nakupa picha zilizonifurahisha katika msafara wa JK , (Kitaaluma na si kiitikadi, japo nami pia nina upande kama mdau)
Amekaa chini na mlemavu bi. Sara Mageni wilayani Makete , Iringa pale bibie huyo alipomuomba amnongoneze kitu fulani...
Tete tee na Bi. Halima Abdallah, mwenye miaka 102 mkazi wa kata ya Kerege wilaya ya Korogwe...
Na Mlemavu Bi. Jacquline Paulo , eneo la Rusahunga akitokea Ngara akitokea Kibondo...
Na mwanafunzi Nicholaus Haba wa Shule ya sekondari Dongobesh , Arusha...
Akiwa na wananchi wa Lupembe huko Ludewa...
(Shukrani waandishi katika Msafara)
Mdau wa MIRINDIMO kama una picha unayotaka tuiweke humu tafadhali nitumie kupitia email hii; brmsulwa@yahoo.com )
Ushuhuda kwa Mchungaji...
A PRETTYGIRL WENT TO CHURCH, TO MAKE A CONFESSION TO A PASTOR. THE PASTOR ASKED HER WHAT THE MATTER WAS. SHE THEN SAID 'MY BOYFRIEND DID SOMETHING BAD TO ME.' THE PASTOR NOW KISSED HER AND SAID 'DID HE DO THIS TO U"?
SHE SAID NO,
THE PASTOR HUGGED HER AND SAID 'DID HE DO THIS TO U"?
SHE SAID NO,
THE PASTOR NOW PULLED OFF HER CLOTHES AND SAID 'DID HE DO THIS TO U"?
SHE SAID NO,
THE PASTOR NOW MADE LOVE TO HER AND SAID 'DID HE DO THIS TO U"?
SHE SAID NO,
THEN THE PASTOR SAID 'WHATT IS THE THING HE DID THAT IS MAKING YOU TO BE CRYING'?
THEN THE GIRL SAID 'HE GAVE ME AIDS.'
Ai wewe...
Wakati wa uhai wake ..
Kuna ubunifu...
Japani leo Jumatatu ni siku ya mapumziko kuwaenzi wazee. Nataka tuangalie wastani wa umri wa kuishi hapa Japani na maeneo mengine duniani.
Huyu bibi alikwishavunja rekodi ya kuwa mwanamke mwenye umri mkubwa duniani baada ya kutimiza miaka 114 . Bahati mbaya amefariki hivi karibuni.Jina lake ni Yone Minagawa, na hati mauti alikuwa ana fahamu zake na alikuwa akiongea na waandishi wa habari akiwa na uelewa tu wa historia yake.
Wastani wa miaka ya kuishi kwa wanawake wa kijapani sasa umefikia miaka 87 huku akinababa wamefikia miaka 80 na kwa wanawake ni umri mkubwa kuliko wowote duniani, huku akinababa wakishika nafasi ya tano.
Washauri wa kitiba na saikolojia hawachezi mbali na wazee hawa hapa Japani...ndio maana wameendelea kuwepo...
Ofisi za takwimu hapa Tokyo zinasema kuwa watoto waliozaliwa mwaka jana wanatarajiwa kuishi hadi mwaka 2095 au 2096. Kwa miaka 25 wanawake wa kijapani wamekuwa wakiongoza kuishi maisha marefu duniani wakifuatiwa na wenzao wa Hongkong miaka 86.1, Ufaransa 84.5, Uswisi 84.4 na Uhispania miaka 82.27.
Kwetu Afrika
nchi yenye wastani mdogo kabisa wa kuishi watu wake na inaongoza pia duniani kwa hali hiyo ni Swaziland 33.2 wakifuatiwa na Botswana miaka 33.9 Lesotho wao wastani ni miaka 34.5 Ukivuka umekopa..
Waswaziland katika ngoma ya asili...
Tanzania wastani wa kuishi wanaume ni miaka 55 na wanawake 56. Mtu akivuka hapo atakuwa amekwepa mishale mingi ya maisha au siyo!
Boma la kimasai kule kwetu 55 kwa 56 ...du!
Mkoa wa Kanagawa nchini Japani si sehemu inayofaa kwa mtu anayevuta sigara . Mkoa huo ambao unajumuisha jiji la Yokohama una sheria inayowazuia watu kuvuta sigara hadharani , mitaani na katika majengo ya umma.
Mji Mkuu wa Mkoa wa Kanagawa , Yokohama.
Ikikulazimu kuvuta inabidi uende kwenye vibanda maalum ama kwenye migahawa inayoruhusu kuvuta. Mtu akipatikana na hatia faini yeni Elfu hamsini sawa na Fedha za Ki-Tz Millioni nane na ushee. Maeneo ambayo ni marufuku kabisa ni pamoja na hospitali, shule na kadhalika. Wadau napendekeza sheria hii ianze kutekelezwa katika majiji ya Dar na Mara ..mnasemaje!
Iliyokuwa REDIO TANZANIA(RTD)...
Watangazaji wa kitambo wa RTD; Kulia Ahmed Kipozi katikati Mkewe Sango Kipozi na Kushoto Betty Mkwasa ambaye sasa ni Mkuu wa wilaya ya Bahi kule Dodoma. Kipozi na Mkewe sango walikuwa watangazaji hapa NHK Japani miaka ya nyuma. Ni hazina kubwa ya taifa katika tasnia ya Utangazaji...
Hebu fuatilia kisa hiki kutoka Kenya ....ujue usichokifikiria kipo!
Kwahiyo sasa baada ya kuangalia umetoka na lipi mdau!
Nimeona niiweke picha hii japo haikuswihi sana ili muone kinachofanyika humu duniani…huyu mama wa Kiafrika anamnyonyesha nguruwe, baada ya mama wa mnyama huyo kufa. Hii unaionaje. Unahisi ni ridhaa yake , ni mabavu ya Fulani…au huruma kwa huyo mbnyama! Wapi na nani inabaki kwenye faili la mirindimo. Mi naona tofauti kabisa … , weye je!
KIDUM... ni mwanamuziki aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufikisha ujumbe wa mapenzi kama ulivyo...unaweza kuusikiliza wimbo huo halafu bofya hapo chini mjue kidum ni ni nani hasa...namkubali
Mjue sasa kidum...
INAELEZWA huko China kuna shule na madarasa yanayofundisha aina mbali,bali za teknolojia hatari kwa afya za watu ikiwa ni pamona na kutengeneza mayai feki kwa kutumia michanganyiko ya kemikali. Hebu fuatilia kiwanda hiki uone mayai yanavyotengenezwa maabara , inatisha mkubwa….
Step 1 modulation of raw materials
Using 7 kinds of chemical materials, Fake egg was made from calcium carbonate, starch, resin, gelatin, alum and other chemical products.
Step 2 egg production
Raw egg into the mold to 2 / 3 full, put calcium chloride, colouring die, the egg appears on the film been announced. The 'yolk' is shaped in the round mould. 'Magic water' containing calcium chloride is used.
By adding a yellow pigment and become raw egg yolk..
Step 3 fake egg shape
In the mold into 1 / 3 raw egg white, like the first package, like dumplings into the egg yolk, egg white into another, into the magic water, a shell eggs will come slowly. Naked egg shape to 1 hour to dry after washing with water, at shells ready.
Step 4
Sewing lines through the use of eggs, immersed in paraffin wax, calcium carbonate, such as modulation of the eggshell into a solution, repeated several times until the shell a little dry, immersion in cold water pumping line shape, this point, the egg has been put on a false cloak , You're done. Hard shells are formed by soaking in paraffin wax onto the egg, which are then left to dry.
Oh yeah The Egg is ready. The artificial egg shell is very fragile and break easily but who cares!! Look so real
Many small bubbles is formed during frying the egg but not many people can tell the difference. The egg look exactly the same, and the eggs taste better than real but you are adding to the statistic of food poisoning person.
Why make fake eggs ?Because of money. The cost of fake egg is only 0.55 Yuan/kg, while the true [WINDOWS-1252?]eggs’ market price is 5.6 Yuan/kg.
Cases of problem foods and food poisoning are widely reported in Mainland China over the last few years. In 2001, there were 185 cases of food poisoning, affecting about 15,715 people and causing 146 deaths. The cases doubled in 2002. In 2003, the number of reported cases was ten times more than that in 2001, and the number of people suffered was as high as 29,660, including 262 deaths Now In Sept 2008 Nearly 53,000 Chinese children sick from contaminated milk; 4 have died...
Waziri Mkuu wa Japan, Naoto Kan leo jumanne amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa chama tawala cha Democratic, baada ya kukabiliwa na ushindani kutoka kwa mpinzani wake, Ichiro Ozawa, mtu mwenye nguvu kubwa ndani ya chama hicho.
Ozawa alijiondoa katika wadhifa wa Naibu mkuu wa chama mwezi Juni, kutokana na shutuma za kashfa ya fedha za ufadhili wa kisiasa. Bwana Kan(Pichani anayetabasamu), ambaye amekuwa katika wadhifa huo kwa miezi mitatu, ameahidi kupunguza madeni na kubana matumizi.
Chama cha Democratic cha Japan kimekuwa kikijitahidi tangu kiingie madarakani mwaka mmoja uliopita, kikipoteza wingi katika baraza kuu la bunge katika uchaguzi wa mwezi Julai. Wakati huo huo, sarafu ya Japan, Yen imepanda kwa kiwango cha kuwahi kuonekana kwa miaka 15 iliyopiata, dhidi ya Dola ya Marekani.
Kwa ushindi huo sasa Kan ataendelea kukalia kiti cha Uwaziri Mkuu , na sasa Baraza la Mawaziri linasubiriwa kutangazwa na Bw. Kan mwenye miaka 63.
Kama angeshindwa maana yake Japani ingelikuwa na Mawaziri wakuu sita katika kipindi cha miaka mine, rekodi ambayo ni ya kipekee kwa nchi zeye chumi kubwa kama Japani. Kan mwenyewe amekuwa Waziri Mkuu kwa miezi mitatu tu basss.
Ozawa akikubali kushindwa..
Jumla ya kura zilizokuwa zikigombaniwa zilikuwa 1,222 ambapo Kan alipata kura 721 na Ozawa kura 491. Kipindi cha wiki moja hapa Japani kiliwanya watu wahemee juu juu kutokana na kampeni kupamba moto, na hasa kutokana na ukweli kuwa watu hao wawili wanatofautiana sana mtazamo wao wa kiongozi, Ozawa akionekana kuwa mkali na Kan akionekana kufuata mkondo wa kidiplomasia zaidi…Yao yameisha tusubiri ya kwetu…
Umenuna tu eeh...
Kijana kutoka Tunduru , Mustapha Abdallah amekamilisha ziara yake hapa Japani siku za karibuni baada ya kufanya maonyesho kadhaa ya michoro ya Tingatinga hapa Japani.
Nilibahatika kuongea naye na wafadhili wake waliomleta hapa...
ukitaka kusikiliza mahojiano hayo unaweza kubofya hapo kulia kwenye kolamu ya MARAFIKI....chini hapo kuna neno NHK WORLD Swahili. Nenda kwenye picha yake, Bofya na msikilize...
Kwa hisani kubwa ya NHK World..
Jiji la Niigata katika picha!
A woman fatally stabbed her two children and then tried to kill herself at their home in Kayam, Niigata Prerecture, on Thursday, police said.
Police said they discovered two children bleeding from multiple stab wounds to their heads, chests and backs at their home after receiving an emergency call from the mother just after 6 a.m.The children, a girl aged 12, and and a boy, 15, were rushed to hospital where they later died. Their 47-year-old mother had also sustained cuts to her chest and wrists. She was quoted by police as saying: “I did it,” but did not give any motive.According to police, the boy was found near the front door and his sister was found on her futon in her room. There was evidence of extensive bleeding and a kitchen knife had been dropped. All three were found in their pajamas.
Their father, 56-year-old company employee, had not yet returned home from a night shift.
Waislamu kote ulimwengu leo wanakamilisha funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani baada ya kufunga na kujizuia kufanya mambo yanayomchukiza Mungu kwa kipindi cha mwezi mzima. Waislamu walio wengi kesho Ijumaa watafanya ibada ya Eid el fitri ingawa baadhi ya madhehebu walisherekea sikuu hii leo.
MIRINDIMO inakupa mkono wa Eid , Eid Mubarak......
Qasda...Kama ingelikuwa kule kwetu ...Dufu hapo ndio mahali pake..
Au unasemaje mdau wa songs.
Genge la watu sita likiongozwa na kijana mmoja wa Ki-Nigeria Nyenche Obenene limekamatwa katika jiji la Tokyo likituhumiwa kuhusika na wizi wa fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia mitandao ya kibenki.
Polisi jijini Tokyo wamesema kuwa watu hao wamejipatia takriban Yeni Millioni 570 kutoka benki ya Marekani katika jitihada zinazotajwa za kuziingiza katika mkondo halali wa kifedha. Fedha hizo na matrilioni kadhaa kwa fedha za Tanzania.
Mtuhumiwa Nyeche Obeneme, ana miaka 36 na mmoja wa wakurugenzi waandamizi wa Kampuni moja inayosafirisha magari iliyopo Mkoa wa Saitama hapa Japani , eneo la Okegawa ambaye ameshirikiana na Wa-Nigeria wenzake wawili, mwanamme mwingine wa Ki-Ghana na wajapani wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanaume.
Fedha hizo zinaaminika kuwa ni sehemu ya YENI Billioni 2.8 zilizosambaza kwa njia ya mtandao kwenye mataifa saba zikiwemo Japan, Korea Kusini, China na Australia na hii ni kwa mujibu wa dodoso kutoka kwenye akaunti ya Citibank iliyopo New York ikiwa na jina la National Bank of Ethiopia in the autumn of 2008.
Fedha zilizoletwa Japani Yeni Millioni 570 zimekwishachukuliwa Benki na sasa Polisi wanahaha kujua nani kapitiwa na fedha hizo. Habari zinasema kuwa Wa-Nigeria watatu wamekamatwa huko Korea Kusini walipokuwa wakijaribu kuchukua sehemu ya fedha hizo na Mnigeria Mwingine amekamatwa alipokuwa akijaribu kughushi nyaraka bandia za kusafirishia pesa kwenda kwenye Benki ya Citibank. Polisi wameapa kuwa hata yule aliyekula yeni moja atanaswa tu . ……Kazi kwelikweli!